mahirtwahir
JF-Expert Member
- Jan 12, 2013
- 614
- 322
Nauliza mujuao, Mulio na nyingi fani
Watu na elimu zao, Magwiji na Magogeni
Nimekwama hadi leo, Mebaki mushkelini
Unaopenda ni moyo, Au akili kichwani?
Wengi niwasikiao, Kila kona mitaani
Husema mioyo yao, Meingia mapenzini
Sisikii wasemao, Yamengia akilini
Naulizia Ni Moyo, Au akili kichwani?
Hodari wasifiwao, Madarasa na Shuleni
Hutajwa akili zao, Moyo haujulikani
Naufikiria moyo, Hapa una kazi gani
Ndio kweli upendao, Au akili kichwani?
Moyo ndio upigao, Damu ikenda mwilini
Kama tasimama leo, Ni kuzikwa kaburini
Nakubaliana nao, Hapo sina upinzani
Unaopenda ni moyo, Au Akili kichwani?
Fikira na mengineyo, Hapo ndio mtihani
Kila Ucha na Uchao, Siuoni ulingani
Sijui undani wao, Wamekusudia Nini?
Unaopenda ni moyo, Au akili kichwani?
Sio watu Peke yao, Bali hata vitabuni
Kila ncha uendayo, Ulaya na Arabuni
Kauli ndo hiyo hiyo, Moyo kitiwa kinywani
Naulizia ni moyo, Au akili kichwani?
Masuali ndio hayo, Jibuni Mlo Makini
Msikimbilie mbio, Kuna mteno wa ndani
Kuyajua yasemwayo, Kunataka Umakini
Unaopenda ni Moyo, Au Akili kichwani?
Niliyouliza hayo, Kabisa sio utani
Mimi nina shida nayo, Niondoke utatani
Ka Bakari na wenzio, Jama Nisaidieni
Naulizia ni moyo, Au akili kichwani?
Watu na elimu zao, Magwiji na Magogeni
Nimekwama hadi leo, Mebaki mushkelini
Unaopenda ni moyo, Au akili kichwani?
Wengi niwasikiao, Kila kona mitaani
Husema mioyo yao, Meingia mapenzini
Sisikii wasemao, Yamengia akilini
Naulizia Ni Moyo, Au akili kichwani?
Hodari wasifiwao, Madarasa na Shuleni
Hutajwa akili zao, Moyo haujulikani
Naufikiria moyo, Hapa una kazi gani
Ndio kweli upendao, Au akili kichwani?
Moyo ndio upigao, Damu ikenda mwilini
Kama tasimama leo, Ni kuzikwa kaburini
Nakubaliana nao, Hapo sina upinzani
Unaopenda ni moyo, Au Akili kichwani?
Fikira na mengineyo, Hapo ndio mtihani
Kila Ucha na Uchao, Siuoni ulingani
Sijui undani wao, Wamekusudia Nini?
Unaopenda ni moyo, Au akili kichwani?
Sio watu Peke yao, Bali hata vitabuni
Kila ncha uendayo, Ulaya na Arabuni
Kauli ndo hiyo hiyo, Moyo kitiwa kinywani
Naulizia ni moyo, Au akili kichwani?
Masuali ndio hayo, Jibuni Mlo Makini
Msikimbilie mbio, Kuna mteno wa ndani
Kuyajua yasemwayo, Kunataka Umakini
Unaopenda ni Moyo, Au Akili kichwani?
Niliyouliza hayo, Kabisa sio utani
Mimi nina shida nayo, Niondoke utatani
Ka Bakari na wenzio, Jama Nisaidieni
Naulizia ni moyo, Au akili kichwani?