Jamani naombeni ushauri wenu, mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 20, naenda chuo mwaka wa kwanza Mzumbe University.
Nimepata mchumba toka nilipomaliza form four, kutokana na vishawishi vya rafiki zangu, ila namshukuru Mungu nimeweza kudumu na huyo mvulana mpaka sasa naenda chuo.
Alikuwa akinifundisha mapenzi mdogomdogo mpaka sasa nimezoea, mimi ni halfcast wa kiarabu na kipemba, mchumba wangu kaniambia niende chuo nikasome mazingira mwakani anioe, me nimekubaliana na hilo kwasababu nampenda sana na naogopa dhambi ya kuzini kwasababu siwezi acha nishaionja asali.
Ila namuogopa mama yangu nahisi hatokubali kwa sababu mimi ni mtoto wa kwanza kwetu, na upande wao ni waarabu wasomi ila kwa upande wa babu yangu ruksa kwa sababu elimu yao ni simple na niwapemba waliobase kwenye biashara wakawin halafu pia naogopa zile kauli za watu kwa mume husomi.
Sasa me nataka kuolewa niache kuzini mana nikirudi likizo nitaendelea kuspend na mchumba wangu, halafu nahisi hatoweza kuningojea mpaka nimalize chuo mana ana hamu ya kuoa nifanyeje?