Nikubali kuolewa?

Prettinho

Member
Joined
Sep 22, 2014
Posts
48
Reaction score
2
Jamani naombeni ushauri wenu, mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 20, naenda chuo mwaka wa kwanza Mzumbe University.

Nimepata mchumba toka nilipomaliza form four, kutokana na vishawishi vya rafiki zangu, ila namshukuru Mungu nimeweza kudumu na huyo mvulana mpaka sasa naenda chuo.

Alikuwa akinifundisha mapenzi mdogomdogo mpaka sasa nimezoea, mimi ni halfcast wa kiarabu na kipemba, mchumba wangu kaniambia niende chuo nikasome mazingira mwakani anioe, me nimekubaliana na hilo kwasababu nampenda sana na naogopa dhambi ya kuzini kwasababu siwezi acha nishaionja asali.

Ila namuogopa mama yangu nahisi hatokubali kwa sababu mimi ni mtoto wa kwanza kwetu, na upande wao ni waarabu wasomi ila kwa upande wa babu yangu ruksa kwa sababu elimu yao ni simple na niwapemba waliobase kwenye biashara wakawin halafu pia naogopa zile kauli za watu kwa mume husomi.

Sasa me nataka kuolewa niache kuzini mana nikirudi likizo nitaendelea kuspend na mchumba wangu, halafu nahisi hatoweza kuningojea mpaka nimalize chuo mana ana hamu ya kuoa nifanyeje?
 
mwambie anywe dawa ya kupunguza hamu ya kuoa, na miaka 20 soma kwanza, halafu kaongeze uzoefu chuo kuna vijana watakutongoza unaweza badilisha mawazo.
 
Hahaha..yani hayo maelezo yako yamenichekesha jinsi unavyojieleza
 
mwambie anywe dawa ya kupunguza hamu ya kuoa, na miaka 20 soma kwanza, halafu kaongeze uzoefu chuo kuna vijana watakutongoza unaweza badilisha mawazo.

me pia naogopa hivyo vikwazo vya chuo cz kuna rafiki yangu alinambia chuo unaweza kumsaliti mchumba wako,,, matamanio mengi,,,
 
olewa tu, waambie wazazi wako kuwa umempenda huyo
 
laiti ungeijua ndoa zilivyo ungesoma kwanza.angekua mwema sana kwako kama angekushauri usome coz yote ingekua faida kwenu.poteza nafasi ya kusoma ili baada ya miaka michache urudi tena jf kuimba ushauri baada ya kuchakazwa na kuachwa.
 
Shule nini bana.......wacha aolewe kwanza........kufeli shule sio kufeli maisha........eg Bill Gates........:A S wink:

Heheheh Preta acha binti asome.....

Dushe limemchanganya anasahau kesho
 
Last edited by a moderator:
Dada uko sahihi kabisa cha msingi n kua waz kwa wazaz wako usihofie ukweli wako utakuweka huru
Waambie uko tayar kusoma ila kwanza watambue una mtu
 
Acha shule haina maana ni mbinu za watu weupe kutukosesha mambo mazuri kwa haraka..sasa wewe olewa tu achana na mambo ya shule,kwani unasoma ili uje uwe nani si mke wa mtu au?
 
Olewa mama equivalent wamejaa tele na wanawatoto wengine zaidi ya watano. Wapo wadogo wanaolewa na kufaulu vizuri sana. Nakumbuka binti mmoja alijifungua wiki kabla ya mtihani na akafanya mtihani akafaulu vizuri sana. Kwa mawazo hayo hata usipoolewa bado kusoma kwako itakuwa ni shida tuu na wasiwasi tele. Bora ungesema baba ataelewa tu. Sema kama kaboyfriend kako ni mmakonde hapo patachimbika.
 
Olewa bwana...kama hutaki mwambie huyo mchumbako anioe mie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…