Michael Scofield
JF-Expert Member
- Jul 30, 2011
- 1,225
- 473
Mkuu,Ndio ni LEAH. Ukiniuliza ni kipi hasa sitaweza kukisema hasa na hata mimi sikijui ni kipi hasa.Kwa sababu kama ni uzuri wa sura huyu wa saivi kamfunika,tabia jibu sina kwa aliyoyatenda.Lakini moyo wangu unakuwaga na amani na furaha ya pekee ninapokuwa nae hata kabla sijafanya nae mapenzi.Ndo hivo mkuu
So kama amemake up her mind still you want to return back to her
bado hujafunguka mkuu kuwa huyo dada hakupendi
After four years still u want her back in your life
tena baada ya kuona mambo sio mambo huko alikoenda
Je kama amepata ngoma ndo anataka aje akupatie kidogo
Je kilichomuondosha kwako kipindi kile ni nini mpaka aje arudi kwa kuonewa huruma
na je akikipata na akakudump tena utajiua kwa sasa au utafanyaje
Mkuu duh wewe mgumu
Kumsahau mtu ni uamuzi mkuu na tena unaouchukua baada ya kuona kuwa hakuna kinachowezekana kwa mtu kama huyo
Umetumia mali zako na resources zako kumnenepesha punda ambaye sana sana at the end of the day hata nyama huwezi kumla
Ulimsaidia na kumfikisha kwenye kilele cha mafanikio na akakudump kwa kukuona huna mlpango na akapata mtu aliyemuona wa maana kuliko wewe huku akifikiria kuwa mambo yatakuwa safi milele sasa ameona mambo sio mambo anakutafuta tena na still bado unataka kurudi
Funguka mkuu
Mkuu Asante,nimekusoma.Signature yako pia imenifundisha kitu.Okay huyu hanipendi nisimfuate .Je huyu niliyenaye ambaye simpendi kivile lakini yeye ananipenda sana? Wasiwasi wangu katika ndo sitakuwa fair kwake in long term ,kwa mwanzoni naweza ku pretend
Pamoja ya kuwa sio ushauri wa maana! kwa sasa lakini naamini huyo Leah ungekuwa umemmega, wala asingekusumbua akili yako. roho inakuuma kwa kukupotezea muda wako, pesa zako ulizokuwa unajibana kwa kumtimizia mahitaji yeye.
Lakini mkuu hawa viumbe maadam bado unaivuta pumzi ya m/mungu na mishemishe za kupata pesa ziko palepale, hawa hamna kitu, atatokea mwenye mapenzi ya kweli kuliko huyo Leah wako.
Piga kimya na namba yake ifute kabisa, yaani mpotezee, mpende ulienae na muonyeshe mapenzi ya kweli Leah hakuwa riziki yako mkuu!
Mkuu Asante,nimekusoma.Signature yako pia imenifundisha kitu.Okay huyu hanipendi nisimfuate .Je huyu niliyenaye ambaye simpendi kivile lakini yeye ananipenda sana? Wasiwasi wangu katika ndo sitakuwa fair kwake in long term ,kwa mwanzoni naweza ku pretend
Hii ndio tabu ya mapenzi ya ukubwani ungekuwa umecheza kombolela hawa viumbe wasingekusumbua kabisa
Mkuu Michael,
Hilo linawezekana? na kama ndo hivyo dalili zake ni nini? kama lipo tiba yake ni nini?
Unapretend and u still having her na kumake love nae
Mkuu mbona unajiumiza sana kufanya kitu ambacho hukitaki
Hebu fanya kama mwanaume ambaye anatakiwa kuwa in love na mwanamke na onyesha kuwa unajali hisia za mwenzako
Kwa nini kujitesa wakati u can make it kaka
Umeshajua kuwa ulitoswa na Leah na umepmapata mtu mwingine anayekupenda
Jifunze kupenda na jifunze kumpenda huyu uliye nae na jifunze taratibu kuyarudisha mapenzi kwake na hata wakati uko nae muone kama malaika aliyetuma kuja kurudisha upendo uliopotea na kuponya jeraha ulilolipata la kukimbiwa na Leah
Alafu mpaka mida hii ushukuru tunakupa ushauri wanaume watupu ngoja waje wale kina naniiii.....? utaona ushauri wao fyongooooo! wamekimbia kwa kuwa wanajua mwanamke mwenzao kakutenda.
Mr Rocky,
Really,Great thanks.KUJIFUNZA-Another terminology,wewe unaweza kujifunza kupenda?
Wana jamvi'
Napiga hodi Jukwaani'
Nina tatizo la kimapenzi la mda mrefu ambalo naamini humu JF ndo mahala naweza kupata ufumbuzi wa tatizo langu.
Inahusu maisha yangu ya kimapenzi, Miaka minne iliyopita (2009) niliingia kwa mara ya kwanza katika ulimwengu wa mapenzi,Nikakutana na Leah akiwa mwaka wa kwanza chuoni mimi nikiwa mwaka wa pili.Huyu binti nilimpenda sana naye alionesha kuwa ananipenda,tukakubaliana kwa pamoja kuwa wapenzi,tukaweka misingi ya kutofanya mapenzi hadi tukioana,tukafanya mambo mengi pamoja,tukawa pamoja mda mwingi,fedha kidogo niliyokuwa nayo nilijibana kwa ajili ya kumtimizia mahitaji yake madogo madogo.Tulitambulishana kwa ndugu zetu wa karibu,kweli tukawa wawili.Mimi binafsi nilimpenda sana kuliko mnavyoweza kudhani.
Nikiwa mwaka wa tatu na yeye akiwa mwaka wa pili nikaanza kuona mabadiliko kidogo,lakini siku namaliza mtihani wa mwisho chuoni na kumaliza degree ya kwanza akaniacha rasmi bila sababu ya msingi.Aliniathiri sana mambo yangu mengi wakati huo nilikua na scholarship ya masters UK nikashindwa kwenda kwa sababu nilimiss deadline kwa sababu nililazwa hospitali kwa muda wa mwezi mzima na ushee.
Nilikua na bahati kwani mara tu baada ya kumaliza shule nilipata na ajira wakati huo nikiwa nimelazwa.Nikaanza kazi lakini nikiwa bado siwezi kukaa bila kumfikiria Leah,efficiency yangu kazini ikawa sio nzuri.Bosi wangu akaniita akanisihi nimwambie nini kinanisibu,ilinibidi nimweleze.Kwa busara zake akaamua kunipa likizo ya mwezi mzima na leave allowance hapo nikiwa na miezi miwili tu kazini.
Nikarelax kidogo.Baada ya miezi mitano nikapata msichana mwingine,huyu ndiye alikuwa msichana wangu wa kwanza kufanya nae mapenzi.Lakini nikawa bado simpendi kutoka moyoni.Hakuna siku wala saa inapita bila kumuwaza Leah.Nikawa nashindwa kum care huyu msichana kwa sababu moyo wangu hauko kwake.Tukaamua kuvunja uhusiano.
Mwaka 2011 Februari nikawa na msichana mwingine ambae niko nae hadi sasa,huyu ananipenda kwelikweli hadi mimi hua naogopa.Lakini moyoni mwangu nalazimisha kumpenda.Ukweli nampenda Leah.Bado siwezi bila yeye.
Naomba mnisaidie;
1.Huyu wa sasa ananipenda sana lakini moyo wangu haupo kwake,nifanyeje?
2.Leah anaonesha kutonipenda kabisa kwa sababu hata nikimpigia simu hapokei,lakini nampenda kulikoni,nifanyeje?
3.Naogopa kuja kuwa mume msumbufu kwa familia pale nitakapooa nisiyempenda kwa dhati,nifanyeje?
afadhari umelitambua hili usije ukamtesa mdada wa watu bure