Niko njia panda

Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,137
4,122
Dada yangu alinitumia sms kuwa yu mjamzito nikaenda kumuona,nikajaribu kuhoji baba wa mtoto ni nani na kwa nini hawafungi ndoa? Akadai wanamipango hiyo. Juzi akanitumia sms kuwa jamaa ni mume wa mtu! Namchukia mwanaume yeyote anaye-cheat hata kama ni kaka yangu na dada anajua hilo. Nimemwambia sitaki kumuona huyo jamaa lakini mimi ndio dada pekee hivyo anahitaji msaada wangu akijifungua maana ndio mtoto wake wa kwanza(mimi nina wa 3). Nitawezaje kumu assist dada yangu bila kuwasiliana na baba wa mtoto aliyemsaliti mkewe? Sitaki hata kumuona!
 
Ilikuwaje dada yako aka hook up na married man?

Unapomchukia mtu aliyemsaliti mkewe, vipi na yule aliyemwezesha kumsaliti mkewe, i.e. dada yako?
 
Nimeshamweleza kuwa sijapenda alichofanya ila anahitaji sana msaada wangu atakapojifungua.
 
Basi hata baba mtarajiwa naye mweleze kuwa hujapenda walichofanya halafu utende tu wema kwa kuwasaidia. Kwa sababu kama utamsaidia mama na mwanae ujue pia unamsaidia baba pia.
 
msaidie tu dada yako huna ujanja na haswa kama atahitaji msaada wako
hayo ndo maisha aliyochagua
kwani ameahidiwa kuolewa mke wa pili?
dada yako ana makosa mana alijua yule ni mume wa mtu, na huyo mume ndo kabisaa, kilichomtoa kwa mkewe?
ila kwa sasa si wakati wa kumlaumu sana utasababishia stress tu na mtoto atakuwa stressed as well si nzuri
as long as ye yuko poa na huo ujauzito we msupport kwa mawazo na ushauri kuhusu ujauzito wake na baada ya.
Kila la heri
 
there is nothing you can do now. Kubali na toa msaada istoshe hayo ni maamuzi ya maisha ya dada yako japo hubaliani naye yeye kaamua na huwezi kusems si ndugu yako tena. pia huyo mume usimchukie sana kwani kosa lake na la dadako nisawa na unaweza kukuta dada yako alichangia zaidi katika hili. samehe na sahau ndivo maisha yalivo
 
msaidie tu dada yako huna ujanja na haswa kama atahitaji msaada wako
hayo ndo maisha aliyochagua
kwani ameahidiwa kuolewa mke wa pili?
dada yako ana makosa mana alijua yule ni mume wa mtu, na huyo mume ndo kabisaa, kilichomtoa kwa mkewe?
ila kwa sasa si wakati wa kumlaumu sana utasababishia stress tu na mtoto atakuwa stressed as well si nzuri
as long as ye yuko poa na huo ujauzito we msupport kwa mawazo na ushauri kuhusu ujauzito wake na baada ya.
Kila la heri

Yet you consider yourself A GREAT THINKER! too low!
 
wewe msaidie kama dada,hakuna asiekosea.yeye mwenyewe anayajua kama ni makosa,ila pengine ana sababu zake.
 
Dada yangu alinitumia sms kuwa yu mjamzito nikaenda kumuona,nikajaribu kuhoji baba wa mtoto ni nani na kwa nini hawafungi ndoa? Akadai wanamipango hiyo. Juzi akanitumia sms kuwa jamaa ni mume wa mtu! Namchukia mwanaume yeyote anaye-cheat hata kama ni kaka yangu na dada anajua hilo. Nimemwambia sitaki kumuona huyo jamaa lakini mimi ndio dada pekee hivyo anahitaji msaada wangu akijifungua maana ndio mtoto wake wa kwanza(mimi nina wa 3). Nitawezaje kumu assist dada yangu bila kuwasiliana na baba wa mtoto aliyemsaliti mkewe? Sitaki hata kumuona!

Ennie kwanza nikupe pole na dada yako

Lakini pia nahitaji unisaidie jambo moja hapa kabla sijasema lolote nisije kosea....

Wewe hutaki kumuona huyo baba wa mtoto wa dada yako, je dada yako anahitaji kumuona? Wasiwasi wangu ni usije mbana kwa asichotaka then ikazaa tatizo kubwa kuliko hili

Just help me kujua mtazamo wa dada yako juu ya mzazi mwenzake (mtazamo wako nimeshaufahamu natarajia wa kwake) then nitakuambia jambo
 
Hivi inakuwaje unatembea na mume wa mtu hadi unazaa naye. Ni bahati mbaya au makusudi?
Au ndio ishakuwa fashen.
B2T: Msaidie tu dada yako. Maji yashamwagika hayazoleki. Wala usiwe na kinyongo. Ila mwambie asirudie.
 
Dada yako amekosea sana. Kutenda haki pande zote ikiwa lazima mwanamume ahusike ni vizuri mke wake pia ajue tatizo hili na kulimaliza kwa maridhiano. yaani huyo baba mtoto alazimike kumweleza mke wake na dada yako awe tayari kumwomba msamaha mwenye mume. Kisha mpange mipango ya jinsi ya kumsaidia mtoto. Kwa vyovyote haya yote hayawezekani katika mkupuo mmoja lakini mimi nakupa overview ya jambo zima. Ili mtoto asikuishi kama invisible being akifichwa fichwa. Kama ni kumsaidia shule au matunzo mengine yule mwanamume asilazimike kuendelea kujificha ili kufanya hivyo. Mazingira ya kificho yanaweza kuzaa balaa jingine la mtoto wa 2
 
Ennie kwanza nikupe pole na dada yako

Lakini pia nahitaji unisaidie jambo moja hapa kabla sijasema lolote nisije kosea....

Wewe hutaki kumuona huyo baba wa mtoto wa dada yako, je dada yako anahitaji kumuona? Wasiwasi wangu ni usije mbana kwa asichotaka then ikazaa tatizo kubwa kuliko hili

Just help me kujua mtazamo wa dada yako juu ya mzazi mwenzake (mtazamo wako nimeshaufahamu natarajia wa kwake) then nitakuambia jambo

yeye anahitaji kumuona maana affair yao inaendelea. Mimi ndio siafiki. Nishauri please.
 
Pole sana, hapo huna ujanja inabidi kumpa msaada ila mshauri aache affair na huyo jamaa(hapa inabidi uwashirikishe ndugu wengine kumshauri)
 
Kwanza nianze kwa tahadhari mimi ni mwanamke.

Lakini kuna ujinga mwingine hauzuiliki, unawezaje kuzaa na mume wa mtu??? Hata kama ni uzembe huu umepitiliza, kwanza kwa dini ni dhambi, sasa mpaka unapata mimba, simkatazi na wala sina uwezo wa kumzuia lakini kama unatembea na mume wa mtu kwanini usiwe makini na uwe na tahadhali ya hali ya juu??? Mimi naona kajitakia mwenyewe matatizo.

Kama mimi ningekuwa wewe nisingemuingilia katiak maamuzi yake kwa sababu ni mtu mzima huyo
 
Asante Dena,

Kuna mtu hapo juu kanambia am not a great thinker kwa comment niliyotoa in between the lines
nikajua niko mwenyewe mwenye mtazamo huo.
Nahkuru umeliona hili pia..

Na mimi nilimuuliza aliahidiwa kuolewa mke wa pili kwa sababu mwanzo alimwambia dada yake kuwa wana mipango ya kuoana.
ngoja nikugongee senks hapo...
 
Dada yangu alinitumia sms kuwa yu mjamzito nikaenda kumuona,nikajaribu kuhoji baba wa mtoto ni nani na kwa nini hawafungi ndoa? Akadai wanamipango hiyo. Juzi akanitumia sms kuwa jamaa ni mume wa mtu! Namchukia mwanaume yeyote anaye-cheat hata kama ni kaka yangu na dada anajua hilo. Nimemwambia sitaki kumuona huyo jamaa lakini mimi ndio dada pekee hivyo anahitaji msaada wangu akijifungua maana ndio mtoto wake wa kwanza(mimi nina wa 3). Nitawezaje kumu assist dada yangu bila kuwasiliana na baba wa mtoto aliyemsaliti mkewe? Sitaki hata kumuona!

Mimi nafikiri ujinga umeshafanyika kati ya dada yako na mume wa mtu
Sasa usifikirie walipoangukia, angalia walipojikwaa ili wasirudie tena
in the meantime, concentrate na huyo malaika wa Mungu, kabla na baada ya kuzaliwa
Huyo mtoto hana makosa, makosa ni ya wazazi
 
Pole sana, hapo huna ujanja inabidi kumpa msaada ila mshauri aache affair na huyo jamaa(hapa inabidi uwashirikishe ndugu wengine kumshauri)

nimemwambia aachane na huyo jamaa,anadai hawezi kumnyima mwanae haki ya kulelewa na wazazi wa2 hata kama mmoja atakuwa anamuona kwa ku-beep na hatomtoa alelewe na mama wa kambo
 
Kwanza nianze kwa tahadhari mimi ni mwanamke.

Lakini kuna ujinga mwingine hauzuiliki, unawezaje kuzaa na mume wa mtu??? Hata kama ni uzembe huu umepitiliza, kwanza kwa dini ni dhambi, sasa mpaka unapata mimba, simkatazi na wala sina uwezo wa kumzuia lakini kama unatembea na mume wa mtu kwanini usiwe makini na uwe na tahadhali ya hali ya juu??? Mimi naona kajitakia mwenyewe matatizo.

Kama mimi ningekuwa wewe nisingemuingilia katiak maamuzi yake kwa sababu ni mtu mzima huyo

Nimekuelewa Dena nami sitaki kuwaingilia kwa walichoamua. Kinachonikwaza ni kuwa sitaki kumtambua kama shemeji na kushirikiana nae kuhudumia mzazi maana dada anataka aje kwangu baada ya kujifungua mpaka atakapo recover.
 
Asante Dena,

Kuna mtu hapo juu kanambia am not a great thinker kwa comment niliyotoa in between the lines
nikajua niko mwenyewe mwenye mtazamo huo.
Nahkuru umeliona hili pia..

Na mimi nilimuuliza aliahidiwa kuolewa mke wa pili kwa sababu mwanzo alimwambia dada yake kuwa wana mipango ya kuoana.
ngoja nikugongee senks hapo...

Wala hawaoani,alinijibu vile ili kuanua ngoma juani.
 
Hivi inakuwaje unatembea na mume wa mtu hadi unazaa naye. Ni bahati mbaya au makusudi?
Au ndio ishakuwa fashen.
B2T: Msaidie tu dada yako. Maji yashamwagika hayazoleki. Wala usiwe na kinyongo. Ila mwambie asirudie.

mwenyewe unajua jinsi mlivyo waongo, huenda ikawa alimdanganya kuwa yupo single, lkn badae akaja kugundua kuwa ana mke, ila chamuhimu tuwe waangalifu!!
 
Back
Top Bottom