Niko njia panda mwenzenu

Mazingaombwe ya ndoa sijui yataishaga lini?
 
unajuaje kama hawana miaka 5 ya mahusiano?na wewe ndo mwizi uliyejibebesha mimba?
Wanawake wengine bana!!Tena mkome tabia ya kusingizia watoto kushikilia uhusiano.

Umeona eeh yeye Ana uhalali gani hapo
 
jipange kulea mwanao bila baba yake couse uliamua kuzaa bila kuwa kwenye ndoa anaweza kuchagua wa kuoa kati yenu utafnyaje?
 
Mpaka muje muoane atakuwa amepitiwa mara ngapi?? Wew una mmoja, utakuja kumkuta mwenzako ana watatu nje
 
Nani alikutuma uzae kabla ya ndoa? Nyie wote hapo mmekosea na yeye yuko huru maana hajafungwa popote na anaweza kuoa mwingine kabosa mbali na nyie.
 

kwanza kakuzalisha ww kabla ya kukuoa, haitoshi kampa mimba mtu mwingine tena kabla ya kukuoa, huyo ni muoaji kweli? Pole zako
 
ukimpend kicheche usiwe mchunguzi... Na hapa duniani, acha kabisa kuchunguza mambo ambayo huwezi kuyafanyia uamuzi... Utaishia kuumia na kujisemesha....'namwachia Mungu'
 
nimemuuliza kuwa amejuaje kama yeye si mwizi

unajuaje kama hawana miaka 5 ya mahusiano?na wewe ndo mwizi uliyejibebesha mimba?
Hili ndio swali.

Wanawake wengine bana!!Tena mkome tabia ya kusingizia watoto kushikilia uhusiano
. Hili hujamtendea haki.
 
jamani Annie una jina zuri kama roho yako ilivyo!

we ni mvumilivu... nimekupendea hicho tu!

sasa kwenye ushauri, naomba tu kama hili limeshatokea, kubaliana nalo tu,

kwa sababu hata kama ukiendelea kulia lia, hautoweza kumrudisha tumboni mtoto huyo aliyezaliwa nje ya tumbo lako!

we kubaliana na matokeo kwamba umechezewa faulo, ila sasa mwambie asirudie kosa! Mpe yellow card ya kwanza....!!!

we si ndo refa bana!!!!
 
Last edited by a moderator:
hiyo waweza ita bahati mbaya eh,ww una mtoto na wenzio ana mtoto,kwahyo nyie wake wenza mkutane na mshauriane jins gan ya kumlea mme wenu mtarajiwa na watoto wenu,maana kama ww ulitongozwa pia mwenzio na yy alifanyiwa hvohvo,so tulizana kama unampenda baba watoto wako usiwe na pupa na uwe mvumilivu mamie
 
Huyo jamaa namuunga mkono ...he is a pure african man....thats bravo charlie.........kwa wewe mama mie sikupi pole ila nakupa hongera kwa kuwa na mtoto na yule mwanamke mwenzio pia nampa hongera kwani nae kazaa vile vile.......(wote mlikosea hamna ndoa).......ushauri ongeza mtoto ......mwingine kwa huyo huyo... Na mwingiene...... Na mwingine.......kadri utakavyo jaliwa........
 
Ni afadhar ukamlea mwanao peke yako kuliko kung'a'ngania ndoa mkamuacha mtoto yatima magonjwa mengi..
Kama huyo dada alijibebesha ujauzito kuna uwezekano akatokea mwingine na mwingine.
Kama alipitiwa kipi kinakuhakikishia kua hatopoitiwa tena?
Mwisho kapime kwanza afya yako coz upo kwenye risk
 
Amu na Usungilo wamenena kwa haki, Dada kwa nn unazaa nje ya ndoa???? huo ni uzinzi na ni chukizo mbele za Mungu na hapo bado sijui kama mlipima kabla hamjaamua kuzaa huyo wa miezi kumi na mbili au ndiyo kuamiana kwa kutazamana. Umeishayavulia nguo hayo maji jiloweke tu usirudi nyuma tena:clap2:mfuate huyo aliye na kachanga muulize na yeye asije kuwa ameahidiwa ahadi kubwa zaidi yako au amemrubuni Mumeo mtarajiwa
 

ni PM nikupe ushauri utakaokuliwaza dada yangu!
 

Unapojiweka kwenye nafasi ya ushauri jitihidi kuwa mtu mwenye akili timamu. Inaonekana huna habari kabisa na maisha ya ndoa, bali unatoa ushauri wa gengeni kwa kutumia uzoefu wa kisela. Wewe mwenyewe hujitambui utamshauri ni nini mwenzio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…