Nini chanzo cha kuumizwa na huyo aliyekuwa Mzazi mwenzio?Wapendwa
Sio mara nyingi nimekuwa nikipost hapa...nimekuwa msomaji mzuri tu wa mabandiko mbalimbali na nimejifunza mengi kupitia post na michango yenu.
Kiukweli niko njia panda ndugu zangu,Niko na historia ya kuumizwa na mzazi mwenzangu mpk ilifika mahala nikamuacha na kuendelea na maisha yangu..
Nilitamani sana kama ningelikuwa na uwezo nibaki single siku zote nisiwe na mahusiano but kama unavyojua tena ujana maji ya moto..Of coz nikisema nitaishi bila dyudyu milele najidanganya...
Niliona kuliko kuangaika ni heri kuwa na mtu mmoja ninayemuamini na kupima ambaye ataendelea kunipoza mpk pale nitakapo amua kuingia katika serious relationship...
Mwanzoni kabisa wakati tunaanza mahusiano nilimwambia msimamo wangu akaniambia ...Mungu ndie mpangaji tuendelee tu nitakufundisha kunipenda..nikaona isiwe tabu tukaendelea na mahusiano yetu ni mwaka sasa.
Kiukweli mwaka umepita...mwanaume ananipenda na kunijali japo hayuko kamili..but sio shida sababu hakuna aliyemkamilifu...shida ni kwamba bado hajaujaza moyo wangu...najitahidi sana kujifunza kumpenda lkn nahisi kuwa naidanganya nafsi yangu ili hali yeye kila siku anazidi kudata na penzi langu na anazidi kunipenda.Imefika mahala mpk na mimi nimeamua kupretend kuwa nampenda ili asiumie.
Mwishoni mwa mwaka jana aliniomba nimpeleke kwa wazazi wangu na kwamba ananipenda sana so anataka kila kitu kiwe formal...nikamjibu kuwa nahitaji muda zaidi kujiridhisha na hayo maamuzi lakini niliona ni mapema sana coz nilishaumizwa na sikutaka kukurupuka tena katika maamuzi
Kiukweli sitoficha sijui ni bahati nzuri au mbaya ila nimekuwa nikitongozwa sana na wanaume katika kipindi hicho kigumu na najua wengi walitaka kutake advantage na situation niliyokuwa nayo but maamuzi ya kuwa kwenye mahusiano yanilisaidia kuendelea kuwa na misimamo yangu....
Lakn kama mnavyojua mapenzi wakati mwingine ni upofu...nimetokea kumpenda mkaka mmoja ambaye ni rafiki yangu tu wa kawaida...na kiukweli alishanitongozaga nikwambia nina mahusiano na kwa vile ni mtu mwenye kuheshimu hisia zangu aliomba tuendelee kuwa marafiki tu kama ilivyozamani..But kila kukicha naona moyo wangu unamwelekea na and I never felt like this before....Kiukweli nimejikuta nashindwa kucontrol hisia zangu kwa huyo mkaka.
Sasa nikija katika vigezo vya husband material kiukweli da first guy anavyo sababu ana Hofu ya Mungu.. ni matured...kashafanya starehe mpk kaamua kuacha...Sio mlevi..Anajali....sio tajiri ila anapambana na maisha kufikia ndoto na malengo yake na amekuwa akinishirikisha kila jambo na pia ameonesha nia dhahiri na kutaka kufunga ndoa na mimi.
About second Guy kiukweli bado anaujana,anakunywa pombe kiasi,kwa tabia siwezi comment sana sababu bado sikumpa nafasi kama mpz ni rafiki yangu tu...so sijapata nafasi kumsoma kiundani zaidi.
Sasa Dilemma inayokuja ni kuwa niolewe na anayenipenda na kunifeel sana nikajifunze kumpenda nikiwa kwenye ndoa au au nisubiri kwanza mpk nijiridhishe na maamuzi yangu coz sitaki kamwe kuchepuka...na me sina haraka sana kusubiri wakati utakaompendeza Mungu but mwenzangu kwa kweli kwa age yake na malengo yake amekuwa akitamani sana tufunge ndoa mwaka huu
Sasa wandugu pamoja ya kuwa niko kwenye maombi nikiendelea kumwomba Mungu anioneshe mwelekeo wa maisha yangu..Natamani mnishauri kama ni sahihi kuendelea mbele na maamuzi ya kuolewa na huyo mkaka au nisubiri..najua ndoa ni kitu chema lkn sitaki kuja kumuumiza mume wangu mtarajiwa kwa kuwa na mahusiano nje ya ndoa na kwa state niliyopo now mpk naanza kufall kwa mwingine inatosha kuonesha danger zone kuwa inawezekana ikatokea kama nikiwa kwenye ndoa
Naomba nieleweke wazi kuwa sina nia ya kuwa na huyo mkaka wa pili na msimamo wangu ni kwamba aendelee kuwa rafiki au ndugu kama walivyo wengine na ameaccept ila kupitia yeye nimeona bado kuna gap katika moyo wangu juu ya huyu niliyenae na hofu yangu ni kuwa sitotaka hilo lije kujirudia katika maisha yangu ya ndoa sababu sitopenda kuisaliti ndoa yangu huko mbele.
Naombeni mnishauri..
Mbarikiwe sana
Maneno yenye hekima kwa mwenye kutanabahi.Dada pole sana ila wapaswa kuwa mwangalifu sana, ndoa sio maigizo bali ni maisha halisi ya kufa na kuzikana hivyo usifanye maamuzi kwa hisia tu. Mwanaume uliyenae humpendi kwa kuwa kishakupenda na kakuonyesha anakupenda sana na pia humpendi kwa sababu bado unasikiliza drama za mlevi wako unayemwita rafiki. Mlevi humpendi ndo maana ulimkataa alipokutongoza awali ila kwakua wanaume tu wajanja huyo kakubali kuwa rafiki akiamini adhima yake itatimia na wewe kwa ujinga wako utamtimizia tu. Mlevi anajitahidi sana kufanya mbwembwe kwakua anajua kuna mpinzani hivyo anataka akuvutie but the first guy anafanya anachokufanyia kwakua anajua yuko peke yake.
Ushauri: Kupenda siyo tabu ila kupendwa mama ni shughuli nzito, ndoa mara nyingi hulindwa na mambo mema anayokutendea mwenzi wako na hivyo huweza jenga hisia hatimae ila ukiendekeza hisia kwa sasa zitakuja kupotea siku ambapo mlevi ataanza drama na madada poa.
Naiona pointi yako, mimi pia nilikuwa namtafakari huyu binadamu katika mweleleko huo huo. Ukimsoma katikati ya mstari unaweza kuhitimisha kuwa ni mwanamke asiye na utulivu katika mahusiano, na ni hatari kuwa naye!Nini chanzo cha kuumizwa na huyo aliyekuwa Mzazi mwenzio?
Kwa maelezo yako sina shaka kwamba huenda ulikuwa chanzo cha kuumizwa kwako.
Huwa najiuliza kwanini single mother wengi wanavitu vinafanana!Nini chanzo cha kuumizwa na huyo aliyekuwa Mzazi mwenzio?
Kwa maelezo yako sina shaka kwamba huenda ulikuwa chanzo cha kuumizwa kwako.
Wazungu husema apertite comes as you eat! kikubwa unatakiwa uolewe na anae kupenda kuliko kuolewa na unae mpenda kwasababu utakuwa salama zaidi kwa anaye kupenda.Anaye kupenda hatakubali kukupoteza lakini ukienda kwa uliye mpenda sana wewe huwezi jua wangapi wanampenda kama wewe ulivyo zimia na pengine hataona shida kukupiga chini akaenda kwa mwingine.Nilichojifunza hapa ni kuwa huyo jamaa wako wa kwanza ambae anataka kukuoa humpendi!...... Swali ambalo sina jibu nalo kwa sasa ni kwamba je inawezekana kuolewa na mtu ambae humpendi? (Somebody help me to answer this question please! )
Rubi michango bado inanisumbua, vipi nataka tufungue letu mi na wewe ziwe zeeeeeetu.Rusha roho taratibu hiyo shoga
Angalia usijekuwa story
Usijekuwa mfano
Usijekuwa tukio bidada
Penda unapopendwa utulizane....
Rubi michango bado inanisumbua, vipi nataka tufungue letu mi na wewe ziwe zeeeeeetu.