Niko chini ya miguu yako muheshimiwa Raisi Magufuli tuondolee watanzania waliopo SA(tahadhari picha zinaogofya)

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
8,098
9,994
Wana Jamvi... Namuomba raisi Magufuli awaondoe wenzetu SA. Leo asubuhi wa SA wanetangaza kuwa walengwa wa kupigwa Ni wa Tanzania.. jamani nchi yetu ni Donour country kwanini wasirudishwe raisi wetu?
Kuna video imewekwa humu kwenye thread furani ya raisi buhari kutuma ndege SA, nimeiangalia huku mikono ikiwa kichwani huku ninatetemeka kwa maumivu... Jamani sisi Ni ndugu kwanini tufanyiane hivi... Eee Buhari mtukufu wapeleke hata Nigeria sisi Ni ndugu jamani. Mtu kuponda kichwa bila kosa mpaka mauti jamani huu sio utu, huu sio uafrica
Jamani nalia mimi
Screenshot_20190906-090101.png
Screenshot_20190906-090101.png
Screenshot_20190906-220245.png
 
Kweli Serikali ingefanya mpango wa kuwarudisha hata mimi jana nimeona picha za vijana wamechinjwa na kutenganishwa vichwa na viwiliwili alafu wakachukua vichwa vyao na kuvining'iniza. Inauma sana kwakweli ee Mwenyezimungu tusaidie
 
Serikali ya SA yabidi ifanye home-work yake vema.Wajue kuwa,nchi yao japo ni kati ya nchi yenye uchumi mkubwa sana Afrika na hata kuzidi baadhi ya nchi nje ya bara la Afrika,wakumbuke huo uhuru walisaidiwa kwa jasho,damu na misaada mingi.Si ajabu kizazi cha sasa hakijajuzwa vya kutosha kuhusu hili.Na hata bila misaada waliyopata isingekuwepo,dunia ya sasa na miingiliano sana katika tasnia za kiuchumi.Kama hawakutaka,wawe na sheria za kuzuia wananchi toka nchi nyingine kuingia huko nchini kwao.

Pia wajuzwe kuwa,dunia ya sasa ni ya miingiliano kikazi/ajira,biashara n.k. Ilimradi wananchi walio huko toka nchi tofauti kama wapo kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi yao,si sahihi haya wanayofanya,si sifa na wanajitafutia laana,kutoeleweka na hata kuja kutengwa na kuchukiwa.Wajue pia kuwa,wapo raia wenzao toka kwao SA wamezagaa katika nchi kibao Afrika na kwingineko.Huu ulimbukeni na roho mbaya wanazotuonyesha,labda kumbe walishabihiana na kustahiliana wao na makaburu wao na wameambukizwa ukaburu.

Ni dhahiri wa kuamua waondoke huko ama la,ni waTz wenyewe.Wakiona hapafai kabisa na hapavumiliki tena,ama watakimbia na kurudi wenyewe ama vinginevyo,ubalozi wa Tz upo huko.Hii ni dharura ambayo si ajabu hata wao hawakuitarajia LABDA.Natumai watajua nini cha kufanya, wao au/na ubalozi.

Aibu kwa hao waliotenda na wanaotenda haya maovu huko SA.
 
natabiri anguko kubwa la kiuchumi sa kama mambo yataendelea namna hii.
 
naona kuna sheria mpya inavunjwa hapa

jeeeefuuuuu wakipigwa fine kwa kuruhusu hivi vitu kurushwa kwenye platform yao bado tuuu watalalamika na kuona wanaonewa

 
Back
Top Bottom