ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,418
- 9,599
- Thread starter
- #21
Me maoni yangu ni kama ifuatavyo,Ze kokuyo wewe kwa upande wako unamaoni gani, mim toka nimepata akili na kujua propaganda na world political economy, marekan amekuwa akitumia propaganda zaid kwa russia na hata kutishiana na kuwekeana vikwazo miaka nenda rudi, lakin ajawah kuingia kijesh had leo, na kama kutakuwa na mgongano wa masirah mahali kama syria lazima watatute njia ya mazungumzo ili isije kuwa balaaa.
Lakin nchi zote ambazo US amekuwa na uwezo nazo na anajua hata jiwe haliwez kusa aridh yao au maslah yao atavamia na majadiliano yanafuta badae, naamin hili utakuwa na mifano hai mingi sana. Lakin leo NK US anaitreet kama Russia kwa kuweka vikwazo kila kukicha maana yake awez kuingia.
Mtazamo wangu hapo kwamba US anatafuta njia ya kuficha haibu ya kauli zake na kutaka kuaminisha dunia kuwa anaweza fanya hivyo huku nafsi yake imejawa na uwoga mkubwa, na pia kuweza kulinda soko lake la siraha ambazo ni ghari sana na zinaonekana hazina kitu. Mataifa mengi yataanza nunua siraha za NK huko mbele maana ameweza kulihakikishia dunia kuwa yupo vizur na hana gharama maana kaweza kumudu kilakitu hata mbele ya vikwazo (low running cost, or cheap running cost)
Pia bwana @koyuko unajua kuwa ukichukua gdp ya china na us interm of PPP ( purchasing power parity) bas china anakuwa na Gdp kubwa hii unajua inamaanisha nin mkuuu?
Kwanza Marekani sidhani kama atakua mjinga kuanzisha vita na Urusi hata siku moja,SIDHANI.
Na si kweli kwamba eti Marekani nchi zote zenye uwezo nazo anashindwa kuzivamia,mfano mzuri ni Iran. Kumbuka Marekani sio mjinga anacheza michezo yake kwa akili kubwa sana.Hizo nchi zenyewe hasimu wa Marekani, marekani anafaidika nazo. Kivipi
Kwanza,
Kibiashara
Marekani amekua akiuza silaha nyingi sana za mabilioni ya shilingi mashariki ya kati kwa mahasimu wa Iran..Anatumia mwanya hyo kuifanya Iran ionekane tishio kwa nchi hizo ili tu kukuza biashara yake ya silaha. Mfano, tumeona miezi michache iliyopita Marekani ilisaini mikataba mbalimbali ya kijeshi ikiwa ni mikubwa haijawahi kutokea na Saudia kuwauzia silaha za dola bilioni mia tatu. Saudia ananunua masilaha yote hayo ili tu ajilinde dhidi ya Iran. Kumbuka Marekani ilishamuonya hata Israel kuhusu kuvamia Iran na walishamuambia kabisa ukirusha kombora lolote kwenda Iran tutalitungua.
Pia kumbuka biashara kubwa sana ya silaha ipo hapo middle east na Asia. Hilo la kwanza.
Pili,
Kiusalama
Kumbuka Marekani kafanikiwa kutandaza rada zake sehemu nyingi hasa huko Ulaya kwa kisingizio cha makombora ya Iran. Juzijuzi hapa Putun alikua analalamika kuhusu Marekani kuweka rada na mitambo yake ya kutungulia makombora Romania,Poland kwa kisingizio cha vitisho vya Iran.Hiyo yote ni kutaka kuzizunguka Urusi na China ili kuzuia makombora yao kama ikitokea vita kati yao, yaaani makombora ya wenzake yasifike kwake ila yake yafike kwao.
Kama nikivyokuelezea kwa Iran na NK ni hivyohivyo sema kwa NK ipo tofauti kidogo maana NK karibu anakaribia kupata uwezo wa kupiga baadhi ya miji ya Marekani. Japokua Marekani anafaidika pia na mgogoro huu lakini pia anaumiza kichwa maaana na yeye hayuko salama.
Kwa ishu ya NK nayo naweza kuiweka makundi kama hayo juu.
Kiusalama
Kumbuka maeneo ya mashariki, magharibi, kaskazini kote Marekani ameshafanikiwa kuweka rada zake (kuchunguza nini kinaendelea ndani ya Urusi na China) na mitambo yake ya makombora, bado kusini. Na tumeona kupitia NK ameshafanikiwa kuanza kuweka hiyi mitambo mfano THAAD,kumbuka rada za THAAD zinaweza kuona hadi ndani ya China hivyo kua rahisi kwa Marekani kuichunguza. Bado tunasikia Japan nae anataka kununua mitambo zaidi toka Marekani ya kujilinda.
Biashara ya silaha
Kumbuka moja ya wanunuzi wakubwa wa silaha za Marekani ni South Korea ili kujilinda na NK. Na hivi juzi tumemsikia Trump akiwahimiza SK na Japan wanunue zaidi silaha za Marekani kujilinda dhidi ya NK
Na cha mwisho GDP na PPP ni vitu viwili tofauti.
Nalendwa izzo nankumene GoLang