Nikipata majibu ya maswali haya narudi CHADEMA

Duh unaweza ukaona mtoa post hajawahi tumia hata nusu ya muda alotumia kuandika hii post kuwaza kwa nini shilingi yetu imeshuka thamani. Pole nchi yangu Tanzania
Nikuulize kitu. Wewe shilingi ikishuka thamani inakuathiri nini hasa. Uliambiwa bei ya mchele, unga, muhogo, itapanda?
 
Dah! Dkt kilembwe umenibainishia umbulula wa magwanda kumbe wote hapo wameshinnwa kujibu hata moja. Sasa mini nakwambia majibu ya hayo yote ni chadema baibai oct. 2015
 
Kusema wasaliti,huoni ni kujidharirisha? jaribu kufikiri kabla ya kujibu hoja.inaonesha vijana ni wahuni wavuta bangi ?
 
mimi hilo la posho ndo linanishangazaga sana kwakweli....et matumizi mabaya ya fedha za umma wakati wote wanakula kwanini wasiziache?
 
Mwanachama huvutiwa na kujiunga na chama kutokana na itikadi na mwenendo wake.
 
mie nakushauri kwa moyo mmoja USIRUDI CHADEMA. maswali yako ni magumu yametushinda.
 
Kweli mkuu. Hayo maswali kingekuwa Chadema chama makini na kipo tayari kuchukua dola kisingeshindwa maswali mepesi kama haya. Lakini kwa sababu bado wanayumba yumba, its until they settle down and recognize themselves.
ni kweli hasa ukizingatia kuwa inaendeshwa kimatakwa ya watu binafsi wachache
 
Nataka kurudi Chadema mara baada ya .....

Nitayaamini maneno yanayotolewa na wanachadema siku siku haya maswali yakipatiwa majawabu

Natamani sana kuwa Kamanda lakini haya yananitatanisha,naombeni majibu ili nifanye maamuzi magumu.

1.Walituambia kuwa chama cha wananchi CUF ni tawi la ccm,wakaenda mbali kwa kuwaita kuwa ni chama cha Mashoga ghafla wakasahau matusi yao na wakaanza mashirikiano Mapya,Je ile tuhuma iliishia wapi?

2.Chadema walituaminisha kuwa Chama cha NCCR mageuzi kimejaa Usalama wa Taifa,wakaenda mbali wakamkejeli Mbatia, tena ndani ya Bunge kuwa,yupo Upinzani huku akiitumikia ccm,ghafla tu Mbatia ni Mshirika namba Mbili wa Ukawa bila watanzania kuelezwa kama zile tuhuma zilikuwa za kweli au za kutunga kwa nia ya kuwalaghai watu.

3.Chadema kwenye Ilani yake 2010 walituambia kuwa tukiwachagua hawatachukua posho kama hatua mojawapo ya kuonyesha kwa vitendo kuchukizwa na matumizi mabaya ya serikali.Je Kwanini wamekiuka Ilani yao?

4.Chadema Mwaka 2011 walikataa kushirikiana na vyama vya Upinzani ili kuunda kambi ya Upinzani yenye sauti na nguvu,wakatuambia kuwa Vyama vyote ni mawakala wa ccm isipokuwa Chadema,hivyo kushirikiana nao ni kurudisha nyuma harakati za ukombozi,ghafla tu baraza kivuli la mawaziri likavunjwa na wale vibaraka wa ccm wakaingizwa kwenye kambi ya upinzani bila sisi wafuasi kuambiwa ni lini ukibaraka wao umeisha mpaka wakaaminiwa.

5.Tuliambiwa kuwa David Kafulila ni mtu hatari kwa ustawi wa Upinzani hasa Chadema,tukaambiwa ni Sisimizi ambae hana umuhimu wowote ndani ya Chadema ,ghafla tu Sisimizi kageuka tembo,Mtu hatari kageuka Shujaa na sasa ananadiwa na viongozi wa Chadema kuwa ukawa imepata tuzo,Je ni lini kafulila alianza kuaminiwa ?

6.Tuliambiwa tena kuwa ,Serikali kutumia mashangingi huku Zahanati hazina dawa ni kiwango cha juu cha Ubinafsi,Mbowe akalikataa Shangingi la Kiongozi wa Upinzani....ghafla nimemuona Bukoba akiwa na Shangingi lenye maandishi KUB. Je ndio lilelile alilolikataa hadharani au ni lingine?

7.Mbowe alituahidi kwenda mahakamani,na kudai kuwa wanasheria wake wanaandaa mashtaka dhidi ya Zitto Kabwe baada ya Zitto kumtuhumu kuwa alipokea fedha toka kwa makada wa ccm na kuwa alicheza dili ns Kinana kuhusu deni analodaiwa na NSSF.Je taratibu za ufunguaji kesi ziliishia wapi ?

8. Chadema Mwaka 2011 ilitangazia Umma kutomtambua Rais Kikwete kwakuwa alishindwa na Slaa,ghafla wanatangaza kuomba mashauriano na Rais waliemkataa,wakafika Ikulu kujadiliana juu ya maswala mbalimbali ya Kitaifa,wakanywa Juice na kupiga picha,Je ni lini Chadema ilianza kumtambua Rais na kwanini sisi wananchi hatukuelezwa kuwa kuanzia sasa Kikwete ni Rais?
Sina nia ya kuibua Marumbano yasiyotujenga bali nataka mtu mwenye uelewa mkubwa kuliko mimi anaondoe Uvulivuli ili nami nijitambue.


Naomba nijibiwe hayo ili nami niwe Kamanda nitakaeitetea Chadema popote.

Hayo Majawabu yakipatikana,ndio utakuwa mwisho wa Chama cha ACT-Wazalendo maana umma utaiamini Chadema na hivyo kuiunga mkono.

Kama Maswali yakikosa Majibu basi Chadema itakosa uhalali wa kutuhumu ACT-Wazalendo na viongozi wake na hivyo wananchi wataendelea kujiunga na ACT-Wazalendo kwa kuamini kuwa maneno yoyote yanayotolewa na Chadema ni Ulaghai.

Karibuni kwa majibu Makamanda ili nasi tupate chakuwaambia wananchi ili waipuuze ACT-Wazalendo.



Karibu CCM chama kinachojali maslahi ya wananchi huku hakuna zengwe na fitna kama za chadema na ukawa kwa ujumla. Karibu sana waambie na wafuasi wenzako CCM ndo mpango wa Mungu toka zamani.
 
Kwa hiyo hii ndio stayle yako ya kumtetea zito ili awe UKAWA?hakuna majibu maana hata ukijibiwa hutaelewa na hata ukielewa hutajitambua,kaa huko huko gizani
 
Back
Top Bottom