Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Katika ukurasa huu nitakuwa nikileta tafakuri mbalimbali kumhusu Mhe. Sana Jaji Warioba na Waziri Mkuu Mstaafu. Kiini cha kuleta tafakuri juu yake ni nafasi yake kama alama pekee katika nchi yetu kwa sasa ya kiongozi aliyetukuka ambaye bado tunaishi naye. Yeye ndiye anabaki kuwa alama ya uzalendo kwa nchi yetu, heshima ya nchi yetu, utu, uhuru, uongozi bora na mambo mengine yaliyolifanya taifa letu kupata heshima kubwa ulimwenguni enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya baba wa taifa marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kama alama, Warioba anatofautiana na wengine wengine (wanaoishi kwa sasa) waliofuatia katika awamu zingine na wanaolitawala taifa letu kwa sasa. Watawala hao wengine wamelifanya taifa letu kuwa la aibu, lisiloheshimika na ambalo linakumbatia udhalimu wa aina mbalimbali.
Nikimtafakari Warioba simumalizi. Anauzalendo wa hali ya juu,utu, msimamia kweli ya wananchi, mkarimu kiasi kwamba anafanya kazi kama mtumishi wa wananchi. Ukianzia katika utumishi wake kama mwenyekiti wa tume ya rais ya katiba mpya unaona utu wake. Warioba amewaongoza wenzake kuachana na ubinafisi na kuwatumikia wananchi wa Tanzania katika kuwaletea rasimu ya katiba (aka Rasimu ya Jaji Warioba) ambayo imesheheni maslahi ya wananchi. Warioba ameendelea kuwa mtulivu katika kuhakikisha kuwa ndoto ya wananchi kupata katiba yao wanayoitaka inafikiwa. Kwake Warioba, kinachoitwa kudhalilishwa katika kufafanua katiba ya wananchi wanayoitaka ni ushindi, utumishi na alama ya kuwawakilisha vemawananchi. Amejishusha kutoka kuwa kiongozi hadi kuwa mtumishi mvumilivu kwa wananchi, akihamasishwa na ndoto yao wananchi ya kupata katiba wanayoitaka.
Katika tafakuri inayofuata, nitaeleza ninavyomuelewa Warioba, namana alivyoenenda akiwa mwenyekiti wa tume ya katiba na katika kongamano la katiba lililovamiwa na kuvunjwa na mazalio ya utawala uliolifanya taifa letu kuwa kichekesho na aibu kubwa ulimwenguni.
Kama "humumalizi!", then hiyo ya kumtafakari, ni "kumutakakari!.
Nakutakia tafakuri njema!.
Pasco
Katika sehemu hii ya mwendelezo wa tafakuri kuhusu Mhe. Jaji Sinde Warioba, ninaeleza jinsi nilivyomuelewa Jaji Warioba alivyolinganisha katiba ya sasa ya JMT na rasimu ya katiba ya Jaji Warioba, na rasimu hii ya Jaji Warioba na ile katiba pendekezwa, aka katiba ya Chenge, Sitta na CCM.Nikimtafakari Jaji Sinde Warioba Simumalizi (2)
Katika sehemu hii ya mwendelezo wa tafakuri kuhusu Jaji Warioba, ninamwelezea namna alivyowasilisha hoja katika mdahalo wa katiba mpya uliovurugwa na mazalio ya watawala waliolifanya taifa letu kuwa la aibu katika jumuiya ya kimataifa.
Katika mdahalo ule, Warioba alikuwa mtulivu wa moyo na fikra, akiongea kwa sauti ya upole bila kusoma popote. Aliongea kwa mpangilio mzuri kiasi kwamba sikuhitaji kuandika chochote wakati namsikiliza ili kukumbuka alichoongea. Katika kutoa hoja yake alianza kwa kueleza mpangilio wa hatua katika kufikia katiba mpya ya wananchi.
Aliongea kwa mpangilio mzuri mambo makuu manne. Kwanza aliongelea mchakato wa katiba, pili aliongelea kilichomo katika rasimu ya pili ya katiba akilinganisha na katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT). Tatu akaelezea njisi rasmu ya pili (a.k.a ya Jaji warioba) inavyoendana na maoni ya wananchi na namna rasimu ya katiba inayopendekezwa (a.k.a ya Sitta) inavyopishana na maoni ya wananchi. Nne alieleza matumizi mabaya ya jina la baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kutetea hoja ya kulazimisha kuungwa mkono rasimu ya Sitta. Katika kuelezea mchakato, Jaji Warioba alieleza kuwa awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu ya mchakato wa katiba zimekamilika. Na kuwa bado awamu nyingine ya wananchi kuipigia kura ya ndiyo na hapana. Kwamba katika awamu ya kwanza yalikusanywa maoni na ikapatikana rasimu ya kwanza ya katiba. Katika awamu ya pili maoni yalikusanywa na hivyo rasimu ya kwanza ikaboreshwa na ikazaliwa rasimu ya pili. Baada ya rasimu ya pili kuwasilishwa bungeni na kujadiliwa rasimu ya katiba inayopendekezwa ikatolewa.
Jaji Warioba pia alielezea mahitaji ya kisheria yanayosimamia mchakato huu wa katiba ikiwemo hitaji la kuwepo kwa kamati za ndiyo na hapana katika ngazi ya kitaifa na kimkoa. Pia sheria inaitaka NEC ya uchaguzi wakati ukifika itunge swali la kuipigia katiba pendekezwa kura ya ndiyo na hapana. Pia kuna hitaji la kuandikisha wapiga wa kuipigia rasimu ya katiba pendekezwa. Pia kutoa elimu ya katiba pendekezwa kabla ya kupigiwa kura. Kulingana na ufafanuzi wa Jaji Warioba, kazi ya kuipigia kura katiba haiwezi kufanywa kwa wakati mmoja na zoezi ya kuandikisha wapiga kura. Hivyo, kulingana na matakwa ya kisheria, ratiba iliyokuwa imesemwa awali ya kuipigia kura rasimu ya katiba pendekezwa mwezi Machi, 2015 haitawezekana.
Katika sehemu inayofuata nitaelezea nilivyomuelewa Jaji Warioba jinsi alivyolinganisha katiba ya sasa ya JMT na rasimu ya katiba ya Jaji Warioba, na rasimu hii ya Jaji Warioba na ile katiba pendekezwa, aka katiba ya Chenge, Sitta na CCM.
Nimekupata vizuri.Najua utakatishwa Tamaa na juu ya unachotaka kufanya Mkuu Ila nikutie moyo kuwa kama Ambavyo Jaji anawafuasi lukuki nyuma yake basi nawe Pia utapata wafuasi lukuki wa kusoma na kusapoti mada yako.........nikianza na mimi,Naunga mkono hoja yako ni ukweli usio kificho kuwa Jaji W.ndiye alama ya uzalendo halisi na mtetezi wa kweli kwa wanyonge wa Nchi hii........
Warioba nae fisadi tu.Ccm walimsaidia kuzima kashfa yake ya ufisadi ya Mwananchi Gold amejisahau.Kama yeye msafi atoke Ccm kama alivyofanya mpendazoeYatafakari na makuwadi ya mafisadi majitu kama Poul Makonda
Nashukuru kwa maoni haya. Lakini uliyemtaja hana hadhi ya kiongozi aliyetukuka kama Warioba, achilia mbali hilo, hastahili hata kusikilizwa. Watu wa aina hii nikiwaona kwenye TV huwa nahamisha channel au nazima TV. Ni mazalio ya watawala walioliletea taifa letu aibu na kukosa heshima mbele ya jumuiya ya kimataifa.Yatafakari na makuwadi ya mafisadi majitu kama Poul Makonda
Katika sehemu iliyopita nilifafanua mambo mapya katika rasimu ya pili ya katiba (ya Warioba) nililinganisha na katiba ya sasa ya JMT inayotumika kwa sasa, na rasimu ya katiba inayopendekezwa (ya Sitta, Chenge na CCM). Nilielezea kuwa hoja ya wajumbe wa CCM wa bunge maalumu ya katiba kuwa asilimia 80% ya maoni ya wananchi yamezingatiwa haina mashiko. Nilieleza kuwa kadiri ya ufafanuzi wa Jaji Warioba ingekuwa jambo la ajabu kwa tume kuyaacha yale mazuri katika katiba ya sasa, ambayo pia yamependekezwa na wananchi yabaki. Jaji Warioba alisema kuwa asilimia 81% ya mambo yaliyomo katika katiba ya sasa ya JMT yalibakishwa kwenye rasmu ya pili ya katiba ya tume ya Jaji Warioba, kwa sababu ni mazuri kwa nchi yetu.Katika sehemu hii ya mwendelezo wa tafakuri kuhusu Mhe. Jaji Sinde Warioba, ninaeleza jinsi nilivyomuelewa Jaji Warioba alivyolinganisha katiba ya sasa ya JMT na rasimu ya katiba ya Jaji Warioba, na rasimu hii ya Jaji Warioba na ile katiba pendekezwa, aka katiba ya Chenge, Sitta na CCM.
Katika kulinganisha, Warioba alianza kwa kueleza kuwa kuna hoja kutoka kwa baadhi ya waliokuwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba (wakitaka kuihalalisha) kuwa asilimia 80% ya maoni ya wananchi yamezingatiwa katika rasimu ya katiba pendekezwa (ya Sitta, Chenge na CCM). Warioba alieleza kuwa katika kuandaa rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba), wajumbe wa bunge la katiba, kwa kuzingatia maoni ya wananchi waliyaweka yote mazuri yaliyopo katika katiba inayotumika sasa ya JMT.
Warioba alieleza kuwa ingekuwa jambo la ajabu kwa tume kuyaacha yale mazuri katika katiba ya sasa, ambayo pia yamependekezwa na wananchi yabaki. Jaji Warioba alisema kuwa asilimia 81% ya mambo yaliyo katika katiba ya sasa ya JMT yalibakishwa kwenye rasmu ya pili ya katiba ya tume ya Jaji Warioba, kwa sababu ni mazuri kwa nchi yetu.
Jaji Warioba, alielezea mambo sita mapya kabisa ambayo hayapo katika katiba ya sasa ambayo wananchi walitaka yawemo katika katiba mpya na wao waliyaweka katika rasmu ya pili (ya Warioba). Mambo hayo ni wananchi kuwawajibisha viongozi wao, ukomo wa ubunge, mawaziri kutokuwa wabunge, mgombea binafsi, tume huru ya uchaguzi na muungano wa Serikali tatu. Ukilinganisha na rasimu ya katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM, karibu mambo yote mapya ya msingi ambayo wananchi walitaka yamemo katika katiba mpya yameondolewa na bunge maalumu la katiba (a.k.a bunge la katiba ya CCM).
Katika sehemu inayofuata, nitafafanua kadiri ninavyokumbuka na nilivyomuelewa Jaji Warioba, mambo ya msingi mapya yaliyopendekezwa na wananchi na yaliyomo katika rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba) lakini hayamo katika katiba pendekezwa sababu yameondolewa na bunge maalumu la katiba ya Sitta na Chenge (katiba ya CCM).
katika ukurasa huu nitakuwa nikileta tafakuri mbalimbali kumhusu mhe. Sana jaji warioba na waziri mkuu mstaafu. Kiini cha kuleta tafakuri juu yake ni nafasi yake kama alama pekee katika nchi yetu kwa sasa ya kiongozi aliyetukuka ambaye bado tunaishi naye. Yeye ndiye anabaki kuwa alama ya uzalendo kwa nchi yetu, heshima ya nchi yetu, utu, uhuru, uongozi bora na mambo mengine yaliyolifanya taifa letu kupata heshima kubwa ulimwenguni enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya baba wa taifa marehemu mwalimu julius kambarage nyerere. Kama alama, warioba anatofautiana na wengine wengine (wanaoishi kwa sasa) waliofuatia katika awamu zingine na wanaolitawala taifa letu kwa sasa. Watawala hao wengine wamelifanya taifa letu kuwa la aibu, lisiloheshimika na ambalo linakumbatia udhalimu wa aina mbalimbali.
Nikimtafakari warioba simumalizi. Anauzalendo wa hali ya juu,utu, msimamia kweli ya wananchi, mkarimu kiasi kwamba anafanya kazi kama mtumishi wa wananchi. Ukianzia katika utumishi wake kama mwenyekiti wa tume ya rais ya katiba mpya unaona utu wake. Warioba amewaongoza wenzake kuachana na ubinafisi na kuwatumikia wananchi wa tanzania katika kuwaletea rasimu ya katiba (aka rasimu ya jaji warioba) ambayo imesheheni maslahi ya wananchi. Warioba ameendelea kuwa mtulivu katika kuhakikisha kuwa ndoto ya wananchi kupata katiba yao wanayoitaka inafikiwa. Kwake warioba, kinachoitwa kudhalilishwa katika kufafanua katiba ya wananchi wanayoitaka ni ushindi, utumishi na alama ya kuwawakilisha vemawananchi. Amejishusha kutoka kuwa kiongozi hadi kuwa mtumishi mvumilivu kwa wananchi, akihamasishwa na ndoto yao wananchi ya kupata katiba wanayoitaka.
Katika tafakuri inayofuata, nitaeleza ninavyomuelewa warioba, namana alivyoenenda akiwa mwenyekiti wa tume ya katiba na katika kongamano la katiba lililovamiwa na kuvunjwa na mazalio ya utawala uliolifanya taifa letu kuwa kichekesho na aibu kubwa ulimwenguni.
Nikimtafakari Jaji Sinde Warioba Simumalizi (5)Nikimtatafakari Jaji Sinde Warioba Simumalizi (4)
Katika sehemu iliyopita nilifafanua mambo mapya katika rasimu ya pili ya katiba (ya Warioba) nililinganisha na katiba ya sasa ya JMT inayotumika kwa sasa, na rasimu ya katiba inayopendekezwa (ya Sitta, Chenge na CCM). Nilielezea kuwa hoja ya wajumbe wa CCM wa bunge maalumu ya katiba kuwa asilimia 80% ya maoni ya wananchi yamezingatiwa haina mashiko. Nilieleza kuwa kadiri ya ufafanuzi wa Jaji Warioba ingekuwa jambo la ajabu kwa tume kuyaacha yale mazuri katika katiba ya sasa, ambayo pia yamependekezwa na wananchi yabaki. Jaji Warioba alisema kuwa asilimia 81% ya mambo yaliyomo katika katiba ya sasa ya JMT yalibakishwa kwenye rasmu ya pili ya katiba ya tume ya Jaji Warioba, kwa sababu ni mazuri kwa nchi yetu.
Jaji Warioba, alielezea mambo sita mapya kabisa ambayo hayapo katika katiba ya sasa ambayo wananchi walitaka yawemo katika katiba mpya na wao waliyaweka katika rasmu ya pili (ya Warioba). Mambo hayo ni wananchi kuwawajibisha viongozi wao, ukomo wa ubunge, mawaziri kutokuwa wabunge, mgombea binafsi, tume huru ya uchaguzi na muungano wa Serikali tatu. Ukilinganisha na rasimu ya katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM, karibu mambo yote mapya ya msingi ambayo wananchi walitaka yamemo katika katiba mpya yameondolewa na bunge maalumu la katiba (a.k.a bunge la katiba ya CCM).
Katika sehemu hii ninafafanua kadiri ninavyokumbuka na nilivyomuelewa Jaji Warioba, kuhusu pendekezo la wananchi kuwawajibisha viongozi wao. Ninaanza na pendekezo la wananchi kuwawajibisha wabunge. Katika rasimu ya pili ya katiba (ya Jaji Warioba) wananchi walitaka kuwawajibisha wabunge wasiokaa katika majimbo yao, na walitaka kuwawajibisha wakishindwa kuwawakilisha wananchi waliowachagua. Hitaji hili la wananchi liliwekwa katika rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba). Lakini katika rasimu ya katiba pendekezwa (ya Sitta, Chenge na CCM) wameondoa. Badala yake wamewapa madaraka vyama vya siasa, na bunge la JMT kuwawajibisha wabunge wao. Hii inapingana na dhana ya kwamba madaraka yote kadiri ya katiba ya JMT msingi wake ni wananchi. Kwamba wananchi wamenyimwa fursa ya kuwawajibisha viongozi waliowachagua, na wakati huohuo, taasisi zisizohusika kuwachagua wabunge ndizo zimepewa madaraka ya kuwawakilisha wabunge. Hii haikubaliki na ni moja ya sababu kubwa kuikataa katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM.
Katika sehemu inayofuata, nitaendelea kutoa ufafanuzi wa mambo mapya ya msingi yaliyopendekezwa na wananchi na kuingizwa katika rasimu ya pili ya katiba (ya Jaji Wariona) lakini yakaondolewa na bunge maalumu ya katiba ya CCM.
Hapa siyo sehemu ya kutafuta wachumba. Kama unataka kuolewa kajitangaze kwenye jukwaa husika, wateja watakuchangamkia na kukuoa ghafla.kama unampenda basi peleka posa akuoe
Nikimtafakari Warioba Simumalizi (6)Nikimtafakari Jaji Sinde Warioba Simumalizi (5)
Katika sehemu iliyopita niliendelea kutoa ufafanuzi kadiri nilivyomsikiliza na kutafakari yale aliyoeleza Mh. Jaji Warioba. Nilieleza kuwa katika rasimu ya pili ya katiba (ya Jaji Warioba) wananchi walitaka kuwawajibisha wabunge wasiokaa katika majimbo yao, na walitaka kuwawajibisha wakishindwa kuwawakilisha wananchi waliowachagua. Hitaji hili la wananchi liliwekwa katika rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba). Lakini katika rasimu ya katiba pendekezwa (ya Sitta, Chenge na CCM) wameondoa. Badala yake wamewapa madaraka vyama vya siasa, na bunge la JMT kuwawajibisha wabunge wao. Niliel;eza kuwa jambo hili haikubaliki na ni moja ya sababu kubwa kuikataa katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM. Katika sehemu hii ninatoa ufafanuzi kuhusu maoni ya wananchi kuhusu ukomo wa ubunge na mawaziri kutokuwa wabunge. Katika rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba) maoni ya wananchi kuhusu ukomo wa ubunge na mawaziri kutokuwa wabunge yalingizwa katika rasimu ya pili ya katiba (ya Jaji Wariona) lakini yakaondolewa rasimu ya katiba pendekezwa (ya Sitta, Chenge na CCM).
Kadiri ya maoni ya wananchi, walitaka ukomo wa kuwa ubunge uwe vipindi vitatu. Lakini bunge maalumu la Sitta, Chenge na CCM wameondoa kabisa ukomo wa ubunge. Pia wameondoa maoni ya wananchi ya kutaka mawaziri wasiwe wabunge. Kuondolewa kwa maoni ya wananchi kuhusu mawaziri kutokuwa wabunge kuna maana kuwa serikali itaendelea kuwa sehemu ya bunge. Hii ina maana kuwa bunge litashindwa kuisimamia serikali ipasavyo kwa vile wabunge mawaziri wanakuwa na conflict of interest. Na kwa hiyo inadumaza uwajibikaji wa serikali kwa bunge na kwa wananchi pia kwa sababu kinadharia wabunge ni wawakilishi wa wananchi.
Kuondolewa kwa maoni ya wananchi kuhusu mawaziri kutokuwa wabunge, inatoa ujumbe kuwa serikali haitaki kuwajibika kwa wananchi kama ilivyo kwa wabunge kukataa kuwajibika kwa wananchi (kumbuka maoni yao ya kutaka kuwawajibisha wabunge wasiokaa majimboni mwao yameoendolewa katika rasimu ya katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM). Mambo haya mapya ya wananchi kuondolewa katika katiba pendekezwa ni sababu nyingine ya kuikataa katiba hiyo ya Sitta, Chenge na CCM.
Katika sehemu inayofuata nitaendelea kutoa ufafanuzi wa mambo mapya yaliyopendekezwa na wananchi na kuwekwa katika rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba) lakini yakaondolewa katika rasimu ya katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM.
Natumaini hata baba yako unamwita hivyoWarioba nae fisadi tu.Ccm walimsaidia kuzima kashfa yake ya ufisadi ya Mwananchi Gold amejisahau.Kama yeye msafi atoke Ccm kama alivyofanya mpendazoe
Ndugu yangu kuna watu hawana hata chembe ya huruma kwa nchi yetu. Ukweli unabaki palepale kuwa Warioba ni alama pekee katika nchi yetu kwa sasa ya kiongozi aliyetukuka ambaye bado tunaishi naye. Hawa wengine wamekengeuka. Hawana kabisa uzalendo kwa nchi yetu. Hawataki kuwajibika kwa wananchi kupitia katiba nzuri ya wananchi ili waendelee kuiba mali na rasli mali za nchi yetu kwa manufaa yao binafsi.Natumaini hata baba yako unamwita hivyo