Nikimtafakari Jaji Sinde Wariba simmalizi

Nikimtafakari Jaji Sinde Wariba simmalizi

Nakuunga mkono mleta uzi...hao wanaotoa comments za kukupinga bila shaka wana lao jambo. Binadamu hatukosi mapungufu na hata Nyerere alikuwa nayo. Lakini Warioba kwa upande wangu namuona kama image ya Mwl. Nyerere!
Nilishasema kwa watu wa namna hiyo ni kuwa- ignore. Siwatofautishi na watu kama Nape na Makonda. Aina ya watu hawa wapuuzi nikiwaona kwenye TV nahamisha Channel au nazima TV.
 
Hawa wote Presida,Six,Chenge,Werema,Lukuvi na Wabunge waliopewa mshiko walikuwa wanajua wanachokifanya.Sijui kama Cheyo leo yupo mzima,atakuwa ndani yake anajutia usaliti wa nchi yake kama hakupokea yawezekana na yeye alipewa MZIGO.


Ninachotaka kusema ni kuwa Prezida amekosea,tunamuomba asiendelee kukosea kwa kuipigia CHAPUO Katiba ya MAFISADI,hilo tu.
Katiba ya wanachi, kama ilivyoandaliwa na Warioba inaziba mianya watawala wezi na mafisadi. Wao wameikataa, wakiongozwa na mwenyekiti wao wa taifa wa chama chao cha mafisadi.
 
Nikimtafakari Jaji Sinde Warioba Simumalizi (7)

Katika sehemu iliyopita (6) nilieleza namna ambavyo Sitta Chenge na CCM wameondoa maoni ya wananchi waliotaka mabadiliko na kuwepo serikali tatu na mgombea binafsi. Katika sehemu hii, ninaeleza kadiri ya ufafanuzi wa Warioba namna jina la Baba wa Taifa linavyotumika vibaya kuhalalisha katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM.

Warioba alieleza kuwa Baba wa Taifa, ambaye katika uhai wake wote alisema kuwa haoni hata nukta ya kupunguza au kuongeza katika azimio la Arusha, hawezi kuondoa maadili ya uongozi katika katiba. Pia hawezi kuondoa pendekezo la wananchi kukataza viongozi kuweka pesa nje ya nchi. Nyerere asingekata tunu za taifa kama vile usawa wa binadamu ambavyo Sitta, Chenge na CCM wameziondoa. Kumbuka usawa wa binadamu ni kiini cha Azimio la Arusha la Nyerere. Warioba alieleza kuwa katika uongozi wake Nyerere, kuna watu walimwendea na kumshawishi aweke pesa zake nje ya nchi, kwa maelezo kuwa pesa zake zitakuwa salama. Nyerere, si tu kuwa alikataa bali alitangaza bungeni mawazo hayo mabaya. Kwa hiyo ni upotoshaji wa Sitta, Chenge na wafuasi wa CCM wanaoipigia upatu rasimu ya katiba iliyoondoa maoni ya wananchi, kuwa Nyerere angeungana nao katika kuondoa maadili ya uongozi, tunu za taifa ikiwemo usawa na uwajibikaji, kuruhusu viongozi kuweka pesa nje ya nchi na kukataa uwajibikaji kama walivyofanya katika katiba hiyo pendelezwa ya CCM. Warioba alieleza pia kuwa katiba pendekezwa ya CCM ni mbovu, alisema kuwa wao wameondoa tunu za taifa walizopendekeza wananchi na kuweka mambo yao kama Muungano ambayo siyo tunu bali ni inheritance yaani urithi.

Kwa ujumla, katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM haikubaliki kwa wananchi, wazanzibar na watanganyika, tunaikataa. Haikubaliki kwa wananachi kwa sababu wameondoa mapendekezo yao mapya. Haikubaliki kwa wazanzibar kwa sababu, Tanganyika imeendelea kushona kanzu ya muungano na hivyo kuitawala Zanzibar kwa kuwa itaitegemea Tanganyika katika kupata fedha za kuendesha serikali. Haikubaliki kwa Tanzania bara kwa sababu wazanzibari wanaonekana kupewa kila wanachotaka na kushiriki shughuli za bunge na uongozi na zingine za maisha Tanzania bara, huku watanzania bara wakiwa hawana haki na mamlaka kushiriki katika mambo ya Zanzibar.

Kitu kingine, ni kuwa asilimia zaidi ya 80% ya mambo mapya yaliyopendekezwa na wananchi na kuwekwa katika rasimu ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba) yameondolewa katika katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM. Kumbuka kutofautisha, kuwa ingawa asilimia 81% ya mambo yaliyomo katika rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba) yamo katika rasimu ya katiba pendekezwa, karibu mambo yote mapya (zaidi ya asilimia 80%) yaliyomo katika rasimu ya pili ya katiba (ya Jaji Warioba) na ambayo hayapo katika katiba inayotumika sasa yameondolewa na Sitta, Chenge na CCM katika rasimu yao ya katiba. Kinachotia kichefuchefu, ni baadhi ya wasomi, ambao wako CCM, wengine hujiita eti watumishi wa Mungu, wanaonekana kwenye vyombo vya habari wakitetea rasimu ya katiba ambayo imeondoa karibu mambo yote mapya yaliyopendekezwa na wananchi kuwemo katika katiba yao. Hao, wanastahili kulaaniwa na Mungu.
 
Katiba ya wanachi, kama ilivyoandaliwa na Warioba inaziba mianya watawala wezi na mafisadi. Wao wameikataa, wakiongozwa na mwenyekiti wao wa taifa wa chama chao cha mafisadi.

Ni kwa sababu wamepata fungu na wanatafuta njia ya kuzideposit nje ya nchi kwa kutumia kipengele cha katiba.

Yaani ningemshauri kidogo tu,hiyo KATIBA asiipigie CHAPUO tena.
 
Katika ukurasa huu nitakuwa nikileta tafakuri mbalimbali kumhusu Mhe. Sana Jaji Warioba na Waziri Mkuu Mstaafu. Kiini cha kuleta tafakuri juu yake ni nafasi yake kama alama pekee katika nchi yetu kwa sasa ya kiongozi aliyetukuka ambaye bado tunaishi naye.

Yeye ndiye anabaki kuwa alama ya uzalendo kwa nchi yetu, heshima ya nchi yetu, utu, uhuru, uongozi bora na mambo mengine yaliyolifanya taifa letu kupata heshima kubwa ulimwenguni enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya baba wa taifa marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kama alama, Warioba anatofautiana na wengine wengine (wanaoishi kwa sasa) waliofuatia katika awamu zingine na wanaolitawala taifa letu kwa sasa. Watawala hao wengine wamelifanya taifa letu kuwa la aibu, lisiloheshimika na ambalo linakumbatia udhalimu wa aina mbalimbali.

Nikimtafakari Warioba simumalizi. Anauzalendo wa hali ya juu,utu, msimamia kweli ya wananchi, mkarimu kiasi kwamba anafanya kazi kama mtumishi wa wananchi. Ukianzia katika utumishi wake kama mwenyekiti wa tume ya rais ya katiba mpya unaona utu wake. Warioba amewaongoza wenzake kuachana na ubinafisi na kuwatumikia wananchi wa Tanzania katika kuwaletea rasimu ya katiba (aka Rasimu ya Jaji Warioba) ambayo imesheheni maslahi ya wananchi.

Warioba ameendelea kuwa mtulivu katika kuhakikisha kuwa ndoto ya wananchi kupata katiba yao wanayoitaka inafikiwa. Kwake Warioba, kinachoitwa kudhalilishwa katika kufafanua katiba ya wananchi wanayoitaka ni ushindi, utumishi na alama ya kuwawakilisha vemawananchi. Amejishusha kutoka kuwa kiongozi hadi kuwa mtumishi mvumilivu kwa wananchi, akihamasishwa na ndoto yao wananchi ya kupata katiba wanayoitaka.

Katika tafakuri inayofuata, nitaeleza ninavyomuelewa Warioba, namana alivyoenenda akiwa mwenyekiti wa tume ya katiba na katika kongamano la katiba lililovamiwa na kuvunjwa na mazalio ya utawala uliolifanya taifa letu kuwa kichekesho na aibu kubwa ulimwenguni.

Eleza cv yake kwanza yeye hatoki butiama kwao ni nyamuswa ukaribu wake na mwalimu nyerere uko wapi ? Je wasira hakuwa karbu na nyerere?
 
Eleza cv yake kwanza yeye hatoki butiama kwao ni nyamuswa ukaribu wake na mwalimu nyerere uko wapi ? Je wasira hakuwa karbu na nyerere?
Hapa sizungumuzii ukaribu wa kifamilia wala ki-jiografia. Nazungumzia ukaribu katika uongozi wa nchi. Haujui kuwa Warioba alipata kuwa Waziri mkuu enzi za utawala wa Mwalimu? Nimesema wazi kuhusu CV ya Warioba kama alama ya mtu aliyetukuka ambaye bado tunaishi nae, aliyekuwa kiongozi katika utawala wakati wa Baba wa taifa. Wasira ni mwana mtandao wa CCM maslahi. Ndiyo maana anapigia chapuo katiba pendekezwa ya CCM ambayo imetupilia mbali mahitaji mapya ya wananchi katika katiba mpya. Wasira hataki uwajibikaji, anataka viongozi wafiche pesa nje, hawezi kamwe kutajwa kulinganishwa na Warioba, achilia mbali kufikiriwa kama kiongozi mwenye maadili.
 
Hapa sizungumuzii ukaribu wa kifamilia wala ki-jiografia. Nazungumzia ukaribu katika uongozi wa nchi. Haujui kuwa Warioba alipata kuwa Waziri mkuu enzi za utawala wa Mwalimu? Nimesema wazi kuhusu CV ya Warioba kama alama ya mtu aliyetukuka ambaye bado tunaishi nae, aliyekuwa kiongozi katika utawala wakati wa Baba wa taifa. Wasira ni mwana mtandao wa CCM maslahi. Ndiyo maana anapigia chapuo katiba pendekezwa ya CCM ambayo imetupilia mbali mahitaji mapya ya wananchi katika katiba mpya. Wasira hataki uwajibikaji, anataka viongozi wafiche pesa nje, hawezi kamwe kutajwa kulinganishwa na Warioba, achilia mbali kufikiriwa kama kiongozi mwenye maadili.

kama sikukosea warioba hajawa waziri mkuu wakati wa nyerere.alikuwa wakati wa mwinyi na kujiuzulu kabla ya kufukuzwa kazi baada ya nyerere kuituhumu serikali kuwa imejaa rushwa.ndio maana nikata cv
 
Jaji Warioba kama binadamu anaweza kuwa na mabaya aliyofanya.Ila kwa sasa namuhesabu kama mzalendo mwenye uchungu na nchi mwenye kuelewa ni nini watanzania wanataka na sio ni nini chama kinataka
 
kadri ya kumbukumbu zangu warioba alikuwa mbunge wa bunda vipindi viwili baada ya ushindi wa mashaka dhiidi ya wasira
 
Back
Top Bottom