Nikimtafakari Jaji Sinde Wariba simmalizi

Stabilaiza

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2012
Posts
1,843
Reaction score
1,143
Katika ukurasa huu nitakuwa nikileta tafakuri mbalimbali kumhusu Mhe. Sana Jaji Warioba na Waziri Mkuu Mstaafu. Kiini cha kuleta tafakuri juu yake ni nafasi yake kama alama pekee katika nchi yetu kwa sasa ya kiongozi aliyetukuka ambaye bado tunaishi naye.

Yeye ndiye anabaki kuwa alama ya uzalendo kwa nchi yetu, heshima ya nchi yetu, utu, uhuru, uongozi bora na mambo mengine yaliyolifanya taifa letu kupata heshima kubwa ulimwenguni enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya baba wa taifa marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kama alama, Warioba anatofautiana na wengine wengine (wanaoishi kwa sasa) waliofuatia katika awamu zingine na wanaolitawala taifa letu kwa sasa. Watawala hao wengine wamelifanya taifa letu kuwa la aibu, lisiloheshimika na ambalo linakumbatia udhalimu wa aina mbalimbali.

Nikimtafakari Warioba simumalizi. Anauzalendo wa hali ya juu,utu, msimamia kweli ya wananchi, mkarimu kiasi kwamba anafanya kazi kama mtumishi wa wananchi. Ukianzia katika utumishi wake kama mwenyekiti wa tume ya rais ya katiba mpya unaona utu wake. Warioba amewaongoza wenzake kuachana na ubinafisi na kuwatumikia wananchi wa Tanzania katika kuwaletea rasimu ya katiba (aka Rasimu ya Jaji Warioba) ambayo imesheheni maslahi ya wananchi.

Warioba ameendelea kuwa mtulivu katika kuhakikisha kuwa ndoto ya wananchi kupata katiba yao wanayoitaka inafikiwa. Kwake Warioba, kinachoitwa kudhalilishwa katika kufafanua katiba ya wananchi wanayoitaka ni ushindi, utumishi na alama ya kuwawakilisha vemawananchi. Amejishusha kutoka kuwa kiongozi hadi kuwa mtumishi mvumilivu kwa wananchi, akihamasishwa na ndoto yao wananchi ya kupata katiba wanayoitaka.

Katika tafakuri inayofuata, nitaeleza ninavyomuelewa Warioba, namana alivyoenenda akiwa mwenyekiti wa tume ya katiba na katika kongamano la katiba lililovamiwa na kuvunjwa na mazalio ya utawala uliolifanya taifa letu kuwa kichekesho na aibu kubwa ulimwenguni.
 
Yatafakari na makuwadi ya mafisadi majitu kama Poul Makonda
 
Najua utakatishwa Tamaa na juu ya unachotaka kufanya Mkuu Ila nikutie moyo kuwa kama Ambavyo Jaji anawafuasi lukuki nyuma yake basi nawe Pia utapata wafuasi lukuki wa kusoma na kusapoti mada yako.........nikianza na mimi,Naunga mkono hoja yako ni ukweli usio kificho kuwa Jaji W.ndiye alama ya uzalendo halisi na mtetezi wa kweli kwa wanyonge wa Nchi hii........
 
Katika ukurasa huu nitakuwa nikileta tafakuri mbalimbali kumhusu Mhe. Sana Jaji Warioba na Waziri Mkuu Mstaafu. Kiini cha kuleta tafakuri juu yake ni nafasi yake kama alama pekee katika nchi yetu kwa sasa ya kiongozi aliyetukuka ambaye bado tunaishi naye. Yeye ndiye anabaki kuwa alama ya uzalendo kwa nchi yetu, heshima ya nchi yetu, utu, uhuru, uongozi bora na mambo mengine yaliyolifanya taifa letu kupata heshima kubwa ulimwenguni enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya baba wa taifa marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kama alama, Warioba anatofautiana na wengine wengine (wanaoishi kwa sasa) waliofuatia katika awamu zingine na wanaolitawala taifa letu kwa sasa. Watawala hao wengine wamelifanya taifa letu kuwa la aibu, lisiloheshimika na ambalo linakumbatia udhalimu wa aina mbalimbali.

Nikimtafakari Warioba simumalizi. Anauzalendo wa hali ya juu,utu, msimamia kweli ya wananchi, mkarimu kiasi kwamba anafanya kazi kama mtumishi wa wananchi. Ukianzia katika utumishi wake kama mwenyekiti wa tume ya rais ya katiba mpya unaona utu wake. Warioba amewaongoza wenzake kuachana na ubinafisi na kuwatumikia wananchi wa Tanzania katika kuwaletea rasimu ya katiba (aka Rasimu ya Jaji Warioba) ambayo imesheheni maslahi ya wananchi. Warioba ameendelea kuwa mtulivu katika kuhakikisha kuwa ndoto ya wananchi kupata katiba yao wanayoitaka inafikiwa. Kwake Warioba, kinachoitwa kudhalilishwa katika kufafanua katiba ya wananchi wanayoitaka ni ushindi, utumishi na alama ya kuwawakilisha vemawananchi. Amejishusha kutoka kuwa kiongozi hadi kuwa mtumishi mvumilivu kwa wananchi, akihamasishwa na ndoto yao wananchi ya kupata katiba wanayoitaka.

Katika tafakuri inayofuata, nitaeleza ninavyomuelewa Warioba, namana alivyoenenda akiwa mwenyekiti wa tume ya katiba na katika kongamano la katiba lililovamiwa na kuvunjwa na mazalio ya utawala uliolifanya taifa letu kuwa kichekesho na aibu kubwa ulimwenguni.

Nikimtafakari Jaji Sinde Warioba Simumalizi (2)
Katika sehemu hii ya mwendelezo wa tafakuri kuhusu Jaji Warioba, ninamwelezea namna alivyowasilisha hoja katika mdahalo wa katiba mpya uliovurugwa na mazalio ya watawala waliolifanya taifa letu kuwa la aibu katika jumuiya ya kimataifa.

Katika mdahalo ule, Warioba alikuwa mtulivu wa moyo na fikra, akiongea kwa sauti ya upole bila kusoma popote. Aliongea kwa mpangilio mzuri kiasi kwamba sikuhitaji kuandika chochote wakati namsikiliza ili kukumbuka alichoongea. Katika kutoa hoja yake alianza kwa kueleza mpangilio wa hatua katika kufikia katiba mpya ya wananchi.

Aliongea kwa mpangilio mzuri mambo makuu manne. Kwanza aliongelea mchakato wa katiba, pili aliongelea kilichomo katika rasimu ya pili ya katiba akilinganisha na katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT). Tatu akaelezea njisi rasmu ya pili (a.k.a ya Jaji warioba) inavyoendana na maoni ya wananchi na namna rasimu ya katiba inayopendekezwa (a.k.a ya Sitta) inavyopishana na maoni ya wananchi. Nne alieleza matumizi mabaya ya jina la baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kutetea hoja ya kulazimisha kuungwa mkono rasimu ya Sitta. Katika kuelezea mchakato, Jaji Warioba alieleza kuwa awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu ya mchakato wa katiba zimekamilika. Na kuwa bado awamu nyingine ya wananchi kuipigia kura ya ndiyo na hapana. Kwamba katika awamu ya kwanza yalikusanywa maoni na ikapatikana rasimu ya kwanza ya katiba. Katika awamu ya pili maoni yalikusanywa na hivyo rasimu ya kwanza ikaboreshwa na ikazaliwa rasimu ya pili. Baada ya rasimu ya pili kuwasilishwa bungeni na kujadiliwa rasimu ya katiba inayopendekezwa ikatolewa.

Jaji Warioba pia alielezea mahitaji ya kisheria yanayosimamia mchakato huu wa katiba ikiwemo hitaji la kuwepo kwa kamati za ndiyo na hapana katika ngazi ya kitaifa na kimkoa. Pia sheria inaitaka NEC ya uchaguzi wakati ukifika itunge swali la kuipigia katiba pendekezwa kura ya ndiyo na hapana. Pia kuna hitaji la kuandikisha wapiga wa kuipigia rasimu ya katiba pendekezwa. Pia kutoa elimu ya katiba pendekezwa kabla ya kupigiwa kura. Kulingana na ufafanuzi wa Jaji Warioba, kazi ya kuipigia kura katiba haiwezi kufanywa kwa wakati mmoja na zoezi ya kuandikisha wapiga kura. Hivyo, kulingana na matakwa ya kisheria, ratiba iliyokuwa imesemwa awali ya kuipigia kura rasimu ya katiba pendekezwa mwezi Machi, 2015 haitawezekana.

Katika sehemu inayofuata nitaelezea nilivyomuelewa Jaji Warioba jinsi alivyolinganisha katiba ya sasa ya JMT na rasimu ya katiba ya Jaji Warioba, na rasimu hii ya Jaji Warioba na ile katiba pendekezwa, aka katiba ya Chenge, Sitta na CCM.
 
Katika sehemu hii ya mwendelezo wa tafakuri kuhusu Mhe. Jaji Sinde Warioba, ninaeleza jinsi nilivyomuelewa Jaji Warioba alivyolinganisha katiba ya sasa ya JMT na rasimu ya katiba ya Jaji Warioba, na rasimu hii ya Jaji Warioba na ile katiba pendekezwa, aka katiba ya Chenge, Sitta na CCM.
Katika kulinganisha, Warioba alianza kwa kueleza kuwa kuna hoja kutoka kwa baadhi ya waliokuwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba (wakitaka kuihalalisha) kuwa asilimia 80% ya maoni ya wananchi yamezingatiwa katika rasimu ya katiba pendekezwa (ya Sitta, Chenge na CCM). Warioba alieleza kuwa katika kuandaa rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba), wajumbe wa bunge la katiba, kwa kuzingatia maoni ya wananchi waliyaweka yote mazuri yaliyopo katika katiba inayotumika sasa ya JMT.

Warioba alieleza kuwa ingekuwa jambo la ajabu kwa tume kuyaacha yale mazuri katika katiba ya sasa, ambayo pia yamependekezwa na wananchi yabaki. Jaji Warioba alisema kuwa asilimia 81% ya mambo yaliyo katika katiba ya sasa ya JMT yalibakishwa kwenye rasmu ya pili ya katiba ya tume ya Jaji Warioba, kwa sababu ni mazuri kwa nchi yetu.

Jaji Warioba, alielezea mambo sita mapya kabisa ambayo hayapo katika katiba ya sasa ambayo wananchi walitaka yawemo katika katiba mpya na wao waliyaweka katika rasmu ya pili (ya Warioba). Mambo hayo ni wananchi kuwawajibisha viongozi wao, ukomo wa ubunge, mawaziri kutokuwa wabunge, mgombea binafsi, tume huru ya uchaguzi na muungano wa Serikali tatu. Ukilinganisha na rasimu ya katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM, karibu mambo yote mapya ya msingi ambayo wananchi walitaka yamemo katika katiba mpya yameondolewa na bunge maalumu la katiba (a.k.a bunge la katiba ya CCM).

Katika sehemu inayofuata, nitafafanua kadiri ninavyokumbuka na nilivyomuelewa Jaji Warioba, mambo ya msingi mapya yaliyopendekezwa na wananchi na yaliyomo katika rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba) lakini hayamo katika katiba pendekezwa sababu yameondolewa na bunge maalumu la katiba ya Sitta na Chenge (katiba ya CCM).
 
Najua utakatishwa Tamaa na juu ya unachotaka kufanya Mkuu Ila nikutie moyo kuwa kama Ambavyo Jaji anawafuasi lukuki nyuma yake basi nawe Pia utapata wafuasi lukuki wa kusoma na kusapoti mada yako.........nikianza na mimi,Naunga mkono hoja yako ni ukweli usio kificho kuwa Jaji W.ndiye alama ya uzalendo halisi na mtetezi wa kweli kwa wanyonge wa Nchi hii........
Nimekupata vizuri.
 
Yatafakari na makuwadi ya mafisadi majitu kama Poul Makonda
Warioba nae fisadi tu.Ccm walimsaidia kuzima kashfa yake ya ufisadi ya Mwananchi Gold amejisahau.Kama yeye msafi atoke Ccm kama alivyofanya mpendazoe
 
Nashukuru kwa maoni haya. Lakini uliyemtaja hana hadhi ya kiongozi aliyetukuka kama Warioba, achilia mbali hilo, hastahili hata kusikilizwa. Watu wa aina hii nikiwaona kwenye TV huwa nahamisha channel au nazima TV. Ni mazalio ya watawala walioliletea taifa letu aibu na kukosa heshima mbele ya jumuiya ya kimataifa.
 
Katika sehemu hii ya mwendelezo wa tafakuri kuhusu Mhe. Jaji Sinde Warioba, ninaeleza jinsi nilivyomuelewa Jaji Warioba alivyolinganisha katiba ya sasa ya JMT na rasimu ya katiba ya Jaji Warioba, na rasimu hii ya Jaji Warioba na ile katiba pendekezwa, aka katiba ya Chenge, Sitta na CCM.
Katika kulinganisha, Warioba alianza kwa kueleza kuwa kuna hoja kutoka kwa baadhi ya waliokuwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba (wakitaka kuihalalisha) kuwa asilimia 80% ya maoni ya wananchi yamezingatiwa katika rasimu ya katiba pendekezwa (ya Sitta, Chenge na CCM). Warioba alieleza kuwa katika kuandaa rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba), wajumbe wa bunge la katiba, kwa kuzingatia maoni ya wananchi waliyaweka yote mazuri yaliyopo katika katiba inayotumika sasa ya JMT.

Warioba alieleza kuwa ingekuwa jambo la ajabu kwa tume kuyaacha yale mazuri katika katiba ya sasa, ambayo pia yamependekezwa na wananchi yabaki. Jaji Warioba alisema kuwa asilimia 81% ya mambo yaliyo katika katiba ya sasa ya JMT yalibakishwa kwenye rasmu ya pili ya katiba ya tume ya Jaji Warioba, kwa sababu ni mazuri kwa nchi yetu.

Jaji Warioba, alielezea mambo sita mapya kabisa ambayo hayapo katika katiba ya sasa ambayo wananchi walitaka yawemo katika katiba mpya na wao waliyaweka katika rasmu ya pili (ya Warioba). Mambo hayo ni wananchi kuwawajibisha viongozi wao, ukomo wa ubunge, mawaziri kutokuwa wabunge, mgombea binafsi, tume huru ya uchaguzi na muungano wa Serikali tatu. Ukilinganisha na rasimu ya katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM, karibu mambo yote mapya ya msingi ambayo wananchi walitaka yamemo katika katiba mpya yameondolewa na bunge maalumu la katiba (a.k.a bunge la katiba ya CCM).

Katika sehemu inayofuata, nitafafanua kadiri ninavyokumbuka na nilivyomuelewa Jaji Warioba, mambo ya msingi mapya yaliyopendekezwa na wananchi na yaliyomo katika rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba) lakini hayamo katika katiba pendekezwa sababu yameondolewa na bunge maalumu la katiba ya Sitta na Chenge (katiba ya CCM).
Katika sehemu iliyopita nilifafanua mambo mapya katika rasimu ya pili ya katiba (ya Warioba) nililinganisha na katiba ya sasa ya JMT inayotumika kwa sasa, na rasimu ya katiba inayopendekezwa (ya Sitta, Chenge na CCM). Nilielezea kuwa hoja ya wajumbe wa CCM wa bunge maalumu ya katiba kuwa asilimia 80% ya maoni ya wananchi yamezingatiwa haina mashiko. Nilieleza kuwa kadiri ya ufafanuzi wa Jaji Warioba ingekuwa jambo la ajabu kwa tume kuyaacha yale mazuri katika katiba ya sasa, ambayo pia yamependekezwa na wananchi yabaki. Jaji Warioba alisema kuwa asilimia 81% ya mambo yaliyomo katika katiba ya sasa ya JMT yalibakishwa kwenye rasmu ya pili ya katiba ya tume ya Jaji Warioba, kwa sababu ni mazuri kwa nchi yetu.

Jaji Warioba, alielezea mambo sita mapya kabisa ambayo hayapo katika katiba ya sasa ambayo wananchi walitaka yawemo katika katiba mpya na wao waliyaweka katika rasmu ya pili (ya Warioba). Mambo hayo ni wananchi kuwawajibisha viongozi wao, ukomo wa ubunge, mawaziri kutokuwa wabunge, mgombea binafsi, tume huru ya uchaguzi na muungano wa Serikali tatu. Ukilinganisha na rasimu ya katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM, karibu mambo yote mapya ya msingi ambayo wananchi walitaka yamemo katika katiba mpya yameondolewa na bunge maalumu la katiba (a.k.a bunge la katiba ya CCM).

Katika sehemu hii ninafafanua kadiri ninavyokumbuka na nilivyomuelewa Jaji Warioba, kuhusu pendekezo la wananchi kuwawajibisha viongozi wao. Ninaanza na pendekezo la wananchi kuwawajibisha wabunge. Katika rasimu ya pili ya katiba (ya Jaji Warioba) wananchi walitaka kuwawajibisha wabunge wasiokaa katika majimbo yao, na walitaka kuwawajibisha wakishindwa kuwawakilisha wananchi waliowachagua. Hitaji hili la wananchi liliwekwa katika rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba). Lakini katika rasimu ya katiba pendekezwa (ya Sitta, Chenge na CCM) wameondoa. Badala yake wamewapa madaraka vyama vya siasa, na bunge la JMT kuwawajibisha wabunge wao. Hii inapingana na dhana ya kwamba madaraka yote kadiri ya katiba ya JMT msingi wake ni wananchi. Kwamba wananchi wamenyimwa fursa ya kuwawajibisha viongozi waliowachagua, na wakati huohuo, taasisi zisizohusika kuwachagua wabunge ndizo zimepewa madaraka ya kuwawakilisha wabunge. Hii haikubaliki na ni moja ya sababu kubwa kuikataa katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM.

Katika sehemu inayofuata, nitaendelea kutoa ufafanuzi wa mambo mapya ya msingi yaliyopendekezwa na wananchi na kuingizwa katika rasimu ya pili ya katiba (ya Jaji Wariona) lakini yakaondolewa na bunge maalumu ya katiba ya CCM.
 
katika ukurasa huu nitakuwa nikileta tafakuri mbalimbali kumhusu mhe. Sana jaji warioba na waziri mkuu mstaafu. Kiini cha kuleta tafakuri juu yake ni nafasi yake kama alama pekee katika nchi yetu kwa sasa ya kiongozi aliyetukuka ambaye bado tunaishi naye. Yeye ndiye anabaki kuwa alama ya uzalendo kwa nchi yetu, heshima ya nchi yetu, utu, uhuru, uongozi bora na mambo mengine yaliyolifanya taifa letu kupata heshima kubwa ulimwenguni enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya baba wa taifa marehemu mwalimu julius kambarage nyerere. Kama alama, warioba anatofautiana na wengine wengine (wanaoishi kwa sasa) waliofuatia katika awamu zingine na wanaolitawala taifa letu kwa sasa. Watawala hao wengine wamelifanya taifa letu kuwa la aibu, lisiloheshimika na ambalo linakumbatia udhalimu wa aina mbalimbali.

Nikimtafakari warioba simumalizi. Anauzalendo wa hali ya juu,utu, msimamia kweli ya wananchi, mkarimu kiasi kwamba anafanya kazi kama mtumishi wa wananchi. Ukianzia katika utumishi wake kama mwenyekiti wa tume ya rais ya katiba mpya unaona utu wake. Warioba amewaongoza wenzake kuachana na ubinafisi na kuwatumikia wananchi wa tanzania katika kuwaletea rasimu ya katiba (aka rasimu ya jaji warioba) ambayo imesheheni maslahi ya wananchi. Warioba ameendelea kuwa mtulivu katika kuhakikisha kuwa ndoto ya wananchi kupata katiba yao wanayoitaka inafikiwa. Kwake warioba, kinachoitwa kudhalilishwa katika kufafanua katiba ya wananchi wanayoitaka ni ushindi, utumishi na alama ya kuwawakilisha vemawananchi. Amejishusha kutoka kuwa kiongozi hadi kuwa mtumishi mvumilivu kwa wananchi, akihamasishwa na ndoto yao wananchi ya kupata katiba wanayoitaka.

Katika tafakuri inayofuata, nitaeleza ninavyomuelewa warioba, namana alivyoenenda akiwa mwenyekiti wa tume ya katiba na katika kongamano la katiba lililovamiwa na kuvunjwa na mazalio ya utawala uliolifanya taifa letu kuwa kichekesho na aibu kubwa ulimwenguni.

kama unampenda basi peleka posa akuoe
 
Nikimtatafakari Jaji Sinde Warioba Simumalizi (4)
Katika sehemu iliyopita nilifafanua mambo mapya katika rasimu ya pili ya katiba (ya Warioba) nililinganisha na katiba ya sasa ya JMT inayotumika kwa sasa, na rasimu ya katiba inayopendekezwa (ya Sitta, Chenge na CCM). Nilielezea kuwa hoja ya wajumbe wa CCM wa bunge maalumu ya katiba kuwa asilimia 80% ya maoni ya wananchi yamezingatiwa haina mashiko. Nilieleza kuwa kadiri ya ufafanuzi wa Jaji Warioba ingekuwa jambo la ajabu kwa tume kuyaacha yale mazuri katika katiba ya sasa, ambayo pia yamependekezwa na wananchi yabaki. Jaji Warioba alisema kuwa asilimia 81% ya mambo yaliyomo katika katiba ya sasa ya JMT yalibakishwa kwenye rasmu ya pili ya katiba ya tume ya Jaji Warioba, kwa sababu ni mazuri kwa nchi yetu.

Jaji Warioba, alielezea mambo sita mapya kabisa ambayo hayapo katika katiba ya sasa ambayo wananchi walitaka yawemo katika katiba mpya na wao waliyaweka katika rasmu ya pili (ya Warioba). Mambo hayo ni wananchi kuwawajibisha viongozi wao, ukomo wa ubunge, mawaziri kutokuwa wabunge, mgombea binafsi, tume huru ya uchaguzi na muungano wa Serikali tatu. Ukilinganisha na rasimu ya katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM, karibu mambo yote mapya ya msingi ambayo wananchi walitaka yamemo katika katiba mpya yameondolewa na bunge maalumu la katiba (a.k.a bunge la katiba ya CCM).

Katika sehemu hii ninafafanua kadiri ninavyokumbuka na nilivyomuelewa Jaji Warioba, kuhusu pendekezo la wananchi kuwawajibisha viongozi wao. Ninaanza na pendekezo la wananchi kuwawajibisha wabunge. Katika rasimu ya pili ya katiba (ya Jaji Warioba) wananchi walitaka kuwawajibisha wabunge wasiokaa katika majimbo yao, na walitaka kuwawajibisha wakishindwa kuwawakilisha wananchi waliowachagua. Hitaji hili la wananchi liliwekwa katika rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba). Lakini katika rasimu ya katiba pendekezwa (ya Sitta, Chenge na CCM) wameondoa. Badala yake wamewapa madaraka vyama vya siasa, na bunge la JMT kuwawajibisha wabunge wao. Hii inapingana na dhana ya kwamba madaraka yote kadiri ya katiba ya JMT msingi wake ni wananchi. Kwamba wananchi wamenyimwa fursa ya kuwawajibisha viongozi waliowachagua, na wakati huohuo, taasisi zisizohusika kuwachagua wabunge ndizo zimepewa madaraka ya kuwawakilisha wabunge. Hii haikubaliki na ni moja ya sababu kubwa kuikataa katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM.

Katika sehemu inayofuata, nitaendelea kutoa ufafanuzi wa mambo mapya ya msingi yaliyopendekezwa na wananchi na kuingizwa katika rasimu ya pili ya katiba (ya Jaji Wariona) lakini yakaondolewa na bunge maalumu ya katiba ya CCM.
Nikimtafakari Jaji Sinde Warioba Simumalizi (5)
Katika sehemu iliyopita niliendelea kutoa ufafanuzi kadiri nilivyomsikiliza na kutafakari yale aliyoeleza Mh. Jaji Warioba. Nilieleza kuwa katika rasimu ya pili ya katiba (ya Jaji Warioba) wananchi walitaka kuwawajibisha wabunge wasiokaa katika majimbo yao, na walitaka kuwawajibisha wakishindwa kuwawakilisha wananchi waliowachagua. Hitaji hili la wananchi liliwekwa katika rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba). Lakini katika rasimu ya katiba pendekezwa (ya Sitta, Chenge na CCM) wameondoa. Badala yake wamewapa madaraka vyama vya siasa, na bunge la JMT kuwawajibisha wabunge wao. Niliel;eza kuwa jambo hili haikubaliki na ni moja ya sababu kubwa kuikataa katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM. Katika sehemu hii ninatoa ufafanuzi kuhusu maoni ya wananchi kuhusu ukomo wa ubunge na mawaziri kutokuwa wabunge. Katika rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba) maoni ya wananchi kuhusu ukomo wa ubunge na mawaziri kutokuwa wabunge yalingizwa katika rasimu ya pili ya katiba (ya Jaji Wariona) lakini yakaondolewa rasimu ya katiba pendekezwa (ya Sitta, Chenge na CCM).

Kadiri ya maoni ya wananchi, walitaka ukomo wa kuwa ubunge uwe vipindi vitatu. Lakini bunge maalumu la Sitta, Chenge na CCM wameondoa kabisa ukomo wa ubunge. Pia wameondoa maoni ya wananchi ya kutaka mawaziri wasiwe wabunge. Kuondolewa kwa maoni ya wananchi kuhusu mawaziri kutokuwa wabunge kuna maana kuwa serikali itaendelea kuwa sehemu ya bunge. Hii ina maana kuwa bunge litashindwa kuisimamia serikali ipasavyo kwa vile wabunge mawaziri wanakuwa na conflict of interest. Na kwa hiyo inadumaza uwajibikaji wa serikali kwa bunge na kwa wananchi pia kwa sababu kinadharia wabunge ni wawakilishi wa wananchi.

Kuondolewa kwa maoni ya wananchi kuhusu mawaziri kutokuwa wabunge, inatoa ujumbe kuwa serikali haitaki kuwajibika kwa wananchi kama ilivyo kwa wabunge kukataa kuwajibika kwa wananchi (kumbuka maoni yao ya kutaka kuwawajibisha wabunge wasiokaa majimboni mwao yameoendolewa katika rasimu ya katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM). Mambo haya mapya ya wananchi kuondolewa katika katiba pendekezwa ni sababu nyingine ya kuikataa katiba hiyo ya Sitta, Chenge na CCM.

Katika sehemu inayofuata nitaendelea kutoa ufafanuzi wa mambo mapya yaliyopendekezwa na wananchi na kuwekwa katika rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba) lakini yakaondolewa katika rasimu ya katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM.
 
Nikimtafakari Warioba Simumalizi (6)
Katika sehemu iliyopita nilielezea kuwa kadiri ya ufafanuzi wa Jaji Warioba, katika rasimu ya katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM, wameondoa hitaji la wananchi la kuwa na vipindi vitatu vya ukomo wa ubunge. Nilieleza pia kuwa katika rasimu ya katiba pendekezwa ya CCM wameondoa maoni ya wananchi ya kutaka mawaziri wasiwe wabunge. Nilieleza kuwa kuondolewa kwa maoni ya wananchi tafsiri yake ni kuwa wabunge, mawaziri na serikali kwa ujumla hawataki kuwajibika kwa wananchi wanaowaweka madarakani.

Katika sehemu hii ninamtafakari zaidi Warioba kuhusu maoni ya wananchi juu ya mgombea binafsi, juu ya tume huru ya uchaguzi, na kuhusu muungano wa serikali tatu. Katika rasmu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba) maoni ya wananchi kuhusu uwepo wa mgombea binafsi katika ngazi mbalimbali yalizingatiwa na kuingizwa kwenye rasimu ya pili. Katika rasimu hiyo ya pili, mgombea huru anaruhusiwa na halazimiki kuwa mwanachama wa chama cha siasa wala halazimiki kupitishwa na chama cha siasa. Katika rasimu ya katiba pendekezwa ya CCM, mgombea binafsi amewekewa mashariki magumu, ikiwemo hitaji la kupitishwa na chama cha siasa, mashariki ambayo yanaondoa na kuzuia maoni ya wananchi kuhusu uwepo wa mgombea binafsi. Kadiri nilivyoelewa ufafanuzi wa Warioba na ninavyokumbuka ni kuwa tume huru ya uchaguzi imezingatiwa katika rasimu ya katiba pendekezwa ya CCM kama ilivyopendekezwa na tume ya Warioba kwa kuzingatia maoni ya wananchi.

Jambo lingine jipya lililopendekezwa na wananchi na kuzingatiwa na tume ya katiba ya Warioba lakini likondolewa na bunge la katiba la Sitta na Chenge na CCM ni kuwa na nchi moja yenye serikali tatu. Katika rasimu ya katiba pendekezwa ya CCM wameweka serikali 2. Cha ajabu ni kuwa Zanzibar wamepewa mambo mengi kuwa huru ikiwemo kujiunga na jumuiya za kimataifa, lakini kulingana na rasimu ya CCM, ni serikali ya Muungano ndiyo yenye mamlaka kamili. Hata Jumuiya ya Afrika Mashariki kadiri ya rasimu ya CCM, Zanzibar haiwezi kujiunga nayo. Kibaya zaidi, mambo kama ardhi ambayo siyo ya Muungano yameingizwa katika rasimu ya katiba pendekezwa ya CCM. Hii inamaana kuwa serikali ya Muungano itakuwa na jukumu ya kusimamia na kuongelea masuala ya ardhi ya Zanzibar katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Na ikumbukwe kuwa kwa Zanzibar kupewa uhuru wa kujiamulia mambo mengi, Tanzania bara ndiyo inabaki kuwa ndiyo serikali ya muungano. Hii inamaana kuwa CCM inauvunja muungano. Kwa lugha rahisi ni kuwa Tanzania bara inavaa koti la muungano. Na kwa kweli siyo koti, sasa imekuwa kanzu. Kwa nini ni kanzu? Imekuwa kanzu kwa sababu pamoja na Zanzibar kupewa kwa kudanganywa mmbo mengi ya kujiamulia, vyanzo vya mapato ya serikali ya muungano vimeainishwa katika rasimu ya CCM kuwa ni ushuru na kodi. Kwa hiyo serikali ya muungano itakuwa na jukumu la kukusanya kodi na ushuru Zanzibar na Tanzania bara. Na wakati huohuo Tanzania bara imevaa kanzu ya Muungano. Hivyo, Zanzibar inakuwa tegemezi kimapato kwa Tanzania bara ili kuendesha serikali ya Zanzibar. Hivyo uhuru inaopewa Zanzibar, unanyang'anywa tena na Tanzania bara (iliyovaa koti la muunganoi) kwa kuondolewa mamlaka ya kukusanya kodi na ushuru kwa kuendesha serikali yake. Katika rasimu ya Warioba, mamlaka za serikali tatu zimetenganishwa na koti la muunganio ambalo Tanzania bara inavaa kwa sasa limevuliwa. CCM, wakaondoa, wakaona waivishe Tanzania bara kanzu ya muungano.

Suala hili la kuondolewa kwa uwezo wa Zanzibar kukusanya kodi na ushuru katika kuendesha serikali ya Zanzibar, linaongeza kero za muungano na linauweka muungano katika hatari ya kuvunjika. Sababu ni kwamba kodi na ushuru ndiyo ilikuwa kero ya kwanza kabisa ya muungano mwaka 1964. Na kero hii iliondolewa kwa kuirudishia Zanzibar mamlaka ya kukusanya kodi na ushuru ili kuendesha serikali yake. Mapendekezo ya CCM, yana maana kuwa Tanganyika iliyovaa koti la muungano inakuwa inaitawala Zanzibar, maana haina mamlaka ya kukusanya kodi na ushuru kuendelesha serikali yake. Suala lingine ni kuwa katika serikali ya muungano, tume ya Warioba ilipendekeza mawaziri na manaibu mawaziri wasiozidi 40, CCM wameweka mawaziri wengi zaidi. Tume ya Warioba ilipendekeza wabunge wa muugano wasiozidi 75, CCM wameweka wabunge zaidi ya 300. Tume ya Warioba ilipendekeza makamu wa raisi watatu. Katika rasimu ya katiba ya CCM kuna makamu ya rais watano. Utaona kuwa gharama za kuendesha serikali ya muungano zimeongezeka kwa sababu ya wingi wa mawaziri, wabunge na makamu wa raisi katika rasimu ya katiba pendekezwa ya CCM, ukilinganisha ka rasimu ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba).

Kwa ufupi ni kwamba asilimia zaidi ya 80% ya mambo mapya Sita (6) yaliyopendekezwa na wananchi na ambayo hayakuwepo katika katiba ya sasa, lakini yaliwekwa katika rasimu ya pili ya katiba ya wananchi (ya Jaji Warioba) yameondolewa katika katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM. Pia, mapendekezo ya CCM, yameifanya Tanzania bara ivae kanzu ya muungano badala ya koti, na hivyo Tanzania bara itakuwa inaitawala Zanzibar kwa sababu serikali ya Zanzibar itakuwa tegemezi kifedha kwa vile kodi na ushuru vitasimamiwa na serikali ya muungano (Tanzania bara iliyovaa kanzu ya muungano). Hizi ni sababu nyingine za kuikataa rasimu ya katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na CCM. Katika sehemu inayofuata nitaeleza namna jina la Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere linavyotumika vibaya kuhalalisha katiba pendekezwa ya Sitta, Chenge na Warioba.
 
Warioba nae fisadi tu.Ccm walimsaidia kuzima kashfa yake ya ufisadi ya Mwananchi Gold amejisahau.Kama yeye msafi atoke Ccm kama alivyofanya mpendazoe
Natumaini hata baba yako unamwita hivyo
 
Natumaini hata baba yako unamwita hivyo
Ndugu yangu kuna watu hawana hata chembe ya huruma kwa nchi yetu. Ukweli unabaki palepale kuwa Warioba ni alama pekee katika nchi yetu kwa sasa ya kiongozi aliyetukuka ambaye bado tunaishi naye. Hawa wengine wamekengeuka. Hawana kabisa uzalendo kwa nchi yetu. Hawataki kuwajibika kwa wananchi kupitia katiba nzuri ya wananchi ili waendelee kuiba mali na rasli mali za nchi yetu kwa manufaa yao binafsi.
 
Nakuunga mkono mleta uzi...hao wanaotoa comments za kukupinga bila shaka wana lao jambo. Binadamu hatukosi mapungufu na hata Nyerere alikuwa nayo. Lakini Warioba kwa upande wangu namuona kama image ya Mwl. Nyerere!
 
Hawa wote Presida,Six,Chenge,Werema,Lukuvi na Wabunge waliopewa mshiko walikuwa wanajua wanachokifanya.Sijui kama Cheyo leo yupo mzima,atakuwa ndani yake anajutia usaliti wa nchi yake kama hakupokea yawezekana na yeye alipewa MZIGO.

Ninachotaka kusema ni kuwa Prezida amekosea,tunamuomba asiendelee kukosea kwa kuipigia CHAPUO Katiba ya MAFISADI,hilo tu.
 
Back
Top Bottom