Mukulu wa Bakulu
JF-Expert Member
- Aug 12, 2014
- 4,050
- 12,968
Wanawake wengine kua single parent hua wanataka wenyewe huyu binti toka nimefahamiana nae hata miezi 2 haijaisha, nimetoka nae mara moja tu ghafla juzi ananiambia ana mimba ya wiki 2, nikashindwa kukataa au kukubali ila nawaza kuikataa.
Nikamshauri akaitoe (yeah, akatoe mimba), akaniambia atanipa jibu, baadae akamwambia mama yake kua nimempa mimba na nimemshauri akaitoe, mama yake akasema isiitoe italea mwenyewe mtoto.
Kuwaambia wazazi wake kua mimi nimetaka mimba itolewe was a fatal mistake, hata kama hakua tayari kuitoa hakupaswa kuwaambia wazazi wake, najiuliza hivi ikitokea mtoto akazaliwa nikaenda kumuona wazazi wake watanionaje, watanichukuliaje, mtoto atakua akiambiwa kua baba yako(kama kweli ni mimi) alitaka mimba yako itolewe, yani kuanzia sasa mahusiano yangu na huyo mtoto mtarajiwa yako ruined.
Uamuzi wangu, naikataa hii mimba once and for good.