Nikiingia Ikulu hata mwanangu atafungwa-Hamad | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nikiingia Ikulu hata mwanangu atafungwa-Hamad

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Sep 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mgombea urais wa Zanzibar kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad  Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema iwapo ataingia Ikulu ya Zanzibar mwezi ujao hakuna mtu atakayekuwa juu ya sheria na iwapo mwanawe au Waziri wake akibainika ametenda kosa atakwenda jela.
  Aidha, Maalim amesema akichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar katika uchaguzi ujao ataunda taasisi ya kupambana na rushwa na amewaonya watendaji serikalini wanaotoa zabuni kwa upendeleo au kujinufaisha mwisho wao Novemba 5 atakapoapishwa.
  Mgombea huyo alisema hayo jana katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho uliofanyika viwanja vya Tibirizi, kisiwani Pemba.
  Alisema katika serikali ya umoja wa kitaifa atakayoiongoza akichaguliwa viongozi, wananchi wote pamoja na yeye mwenyewe watakuwa chini ya sheria.
  “Hata mwanangu Suleiman Seif atafungwa kama atabainika mbele ya sheria kuwa amefanya kosa, na hata awe Waziri akivunja sheria atafungwa,” alisema Maalim Seif.
  Alisema ahadi hiyo itatekelezeka kwa vile wakati wa uongozi wake vyombo vyote vya sheria, zikiwemo mahakama zitafanya shughuli zake kwa uhuru mkubwa na hakutakuwa na nafasi ya kusema huyo ni mtoto wa Rais. Kuhusu rushwa mgombea huyo alisema vitendo hivyo vipo kwa wingi Zanzibar na vimeenea katika zabuni za serikali na ununuzi wa mali, kutokana na zabuni kutofanywa kwa uwazi.
  Aliwaeleza wafuasi na wanachama wa CUF kuwa atahakikisha shughuli zote serikalini zinafanywa kwa uwazi kwa mujibu wa misingi ya utawala bora.
  Aidha, alisema iwapo atachaguliwa kuingia Ikulu Zanzibar atapinga aina zote za ubaguzi, ikiwemo vitendo vya baadhi ya wananchi wenye sifa kunyimwa vitambulisho vya Uzanzibari ukaazi, vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa (Masheha).
  Alisema ubaguzi wa aina yoyote utakuwa haramu na Wazanzibari wote watakuwa sawa na serikali ya umoja wa kitaifa itagusa matabaka na itakuwa na uwakilishi wa vyama vyote vya siasa vyenye wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
  Alieleza kwamba atahakikisha wananchi wote watapata hati za kusafiria bila ya usumbufu wowote kinyume na hali inayojitokeza hivi sasa, ambapo wale wanaotafuta hati hizo wamekuwa wakikumbana na usumbufu mkubwa.
  Aliendelea kuwaahidi wananchi wote wa Zanzibar watarajie mabadiliko makubwa ya upatikanaji wa huduma za jamii, ikiwemo usafiri wa uhakika kati ya visiwa vya Unguja na Pemba utakaowawezesha wananchi kufanya shughuli za kibiashara kwa urahisi kati ya visiwa hivyo.
  Aliwaahidi wafanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa atawapandishia mshahara na kuwalipa sh 150,000 kwa mwezi kwa wafanyakazi wa kima cha chini, na wale wa kima cha juu wataongezewa kwa uwiano huo.
  Mapema mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho, na kiongozi wa upinzani bungeni anayemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohammed amewataka wananchi wa Pemba kutomuangusha Maalim Seif kwa vile alipitia misukosuko mikubwa akiwa na CUF kwa nia ya kuwaletea maisha bora Wazanzibari.
  Kiongozi huyo alisema miongoni mwa misukosuko aliyoipitia Maalim Seif pamoja na CUF ni chama hicho kusingiziwa kinahusika na ugaidi, ambapo Marekani na Canada baadaye zilithibitisha kwamba madai hayo yalikuwa uongo mtupu.
  Alisema Maalim Seif ndiye kiongozi anayeweza kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo Zanzibar kwa vile muda wake wote ameutumia kutetea haki za Zanzibari na hata alipotimuliwa CCM aliwahidi wananchi katika uwanja huo huo wa Tibirinzi kwamba atakuwa pamoja nao akiwa ndani au nje ya serikali.
  Naye, Makamo Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali aliwataka wanachama na wafuasi wa CUF kisiwani Pemba wasibabaishwe na vyama vyengine vinavyojipenyeza na kuwahadaa wananchi.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Wana semaga tu.
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  MwanaFA1,
  Ni kweli kama ukisoma manifesto ya CUF hakuna ubabaishaji tupo serious na utawala bora na haki za binaadamu, hilo CUF imelifanikisha hata kabla ya kuingia ikulu...kumbuka ni CUF waliopendkeza na kulazimisha kuanzishwa kwa ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) ili kuondokana na ukiritimba wa jeshi la polisi kubambikia watu kesi.

  Imeelezwa katika manifesto yetu kuwa ofisi ya haki za binaadamu (Ombusman) itaanzishwa na itakuwa huru ndiyo maana Maalim anasema yeyote atakayevunja haki ya mwenzake hata kama mwanawe hatasalimika.

  Mkuu naona unakuwa kama CCM wakiambiwa nchi hii inaweza kumsomesha mtoto wa kitanzania bure kutoka std 1 mpaka chuo kikuu, unakuwa huamini na unaona haiwezekani...huku ukishindwa kuangalia mangapi yasiyokuwa na maana yanafanyika kwa fedha na gharama kubwa kupitiliza yanawezekana?
  Maalim hasemagi tu anasema kile kinachowezekana
   
 4. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  haki sawa kwa wote
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Shein for Bright future in Zanzibar
   
 6. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,654
  Trophy Points: 280
  Ahh, wapi! Hembu waacheni wazanzibari wachague Raisi wao kwani hata huyo SHEIN si chaguolao bali wanalazimishwa kutoka Tanganyika.
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na ndiyo maana kwenye mkutano wao wa ufunguzi wa kampeni juzi Kibandamaiti, wamekusanya wanachama wao wa mikoa mitatu ya Unguja kuja kwa magari hadi mjini kuhudhuria...wanasema wameweka rekodi wenyewe...wakati Maalim simple tu...mjini magharibi ilitosha kujaza uwanja...by the way CUF inajivunia mtaji wa wapiga kura wengi na si wanachama...tuna wanachama mpaka watoto wadogo ambao si wapiga kura...kama utaangalia mikutano ya CCM utakuta chokoraa nyingi halafa wanajilabu kuwa ndiyo dalili ya ushindi, wamechelea.
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu ninacho pinga ni kauli ya kusema hata ikiwa ni mwanae. Viongozi wengi sana wana semaga hili la hata mwanangu au hata mke/mume wangu lakini kiukweli when it touches home it is a different story. Wengi hutumia kauli hii kuonyesha msisitizo lakini nadhani anaweza kufanya hivyo bila kudai kwamba hata mwanae hato mkingia kifua. Ni wachache sana ambao kweli wanaweza waka achia hilo na mara nyingi una kuta uhusiano wa huyo mtu na mwanae ni estranged. Anyway labda mimi naongea kama mimi kwa sababu na amini kabisa ningekua na mtoto hakika nisinge muachia hivi hivi kama ninaweza kumtetea.
   
 9. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  remote control or Tanganyika
   
 10. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ndugu yangu, sasa hivi si wakati wa siasa za jino kwa jino

  kwa hio chaguo muafaka kwa wazanzibari ni shein, na kwa sababu Seif atakuwa ni makamo atamshauri na yale ambayo kweli yana faida tutayaiingiza kwenye plan ya serikali

  unajua maalim Seif na walio nyuma yao wana jazba sana ktk kuiendesha nchi na nnaogopa day one tu akiwa rais mambo hayataenda kwa anavyotaka

  maana yeye anaamini kuendesha mambo kwa nguvu, anaamini nnadhani pamoja na wengine hapa hatua ya kwanza ni kuuvunja muungano au kufanya mambo mpaka watanganyika waone heri wawe na serikali yao.

  Maalim Seif anauangalia muungano kwenye mapungufu tu, na hayuko tayari kuja na suluhisho lililobora

  siombei hata siku moja Maalim aongoze Zanzibar, najua Maalim ni Kiongozi mzuri ila asiwe Rais
   
Loading...