nikajitambulishe kwao

nikajitambulishe kwao

libwaka

Member
Joined
Apr 26, 2013
Posts
53
Reaction score
11
Habari zenu wana jf nami leo naomba mnishauri -kunamsicha nimempenda, sasa tuna wiki 3 tu tangu tufahamiane hivyo ameniambia km nampenda kweli niende nikajitambulishe kwao, mi najiuliza hivi muda unatosha kweli kujitambulisha kwao? ushauri wako mhimu saaaana.
 
Wiki 3 tu ukajitambulishe??? eboh
Kwani hiyo imekuwa ni ajira kwamba lazima uripoti kwa mkuu wa kituo kipya cha kazi...!!!
Nadhani huyo dada kashatendwa sana sasa hajiamini na namna pekee ya kujihami ni kutumia silaha ya kutambulishwa ili iwe kama kitanzi, otherwise ni mshamba wa mahusiano.
 
Mi nadhani unatakiwa utulie kwanza, kama naye anakupenda bila agenda ya siri atakuelewa, wik3 ni mapema mno, ukiona mtu anafanya haraka haraka, kuna kitu anatime ili bomu hata likilipuka iwe too late to revoke, (akili za kuambiwa, changanya na zako, Maneno yangu si sheria)
 
inawezekana amekupenda for real au la ni wale wanaisubiria ndoa kwa hamu kubwa hata hawajali mengine,mie naona ni mapema sana kujitambulisha hujamjua huyo dada vizuri kama mnaendana vizuri
 
Duuuduu majanga

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamie's
 
3 weeks, hapo kweli hata jina lake la pili unalikumbuka sawa sawa? Namba ya simu je? Umeshajuana na marafiki zake wangapi?
take it slow
 
weeee ogopa sana,wiki tatu ni ndogo.usijefanya kitu utachojuta baadae.
 
hili nalo toleoo jipya,3weeks wakati wengine inachukua 3years:mmph::mmph:
 
3 weeeks! Mmmmh! Mapema mno utanunua mbuzi kwenye gunia! Vuta subira!
 
Anafikiri unamdanganya kama unampenda. Ndio maana akiona unaenda kujitambulisha kwao, atajua kweli unampenda.
Ilibidi usimwambie kama unampenda, kama hauna mpango wa kumuoa.
 
Hataki aonekane muhuni na ndo mana anapenda ukajitambulishe, ili hata ikitokea amekufa wakati wa utamu au ameonwa na ndugu zake yupo na wewe, wajue wewe ni mchumba wake, sio tena kujificha uvunguni.
 
Mwambie awe mvumilivu mpate muda wa kufahamiana kitabia coz wik3 n mapema sana
 
to early brother take it slow that you can knw her in and out, stay blessed
 
Wiki 3 ni chache sana tulia, vuta subira kama na yy anakupenda kweli mwambie asubiri mhunguzane na mjuane vzr kitabia kwanza, asipokulewa tupa kuleeeee anataka akuuzie mbuz kwny gunia
 
Mmmh!! Hii kali ya mwaka 3weeks halafu ukajitambukishe!!
Huo ni muda mfupi sana kufahamiana kaanaye chini mwelimishe kwa upendo atakuelewa

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Habari zenu wana jf nami leo naomba mnishauri -kunamsicha nimempenda, sasa tuna wiki 3 tu tangu tufahamiane hivyo ameniambia km nampenda kweli niende nikajitambulishe kwao, mi najiuliza hivi muda unatosha kweli kujitambulisha kwao? ushauri wako mhimu saaaana.

Labda ungedadavua vizuri, ujitambulishe kama nani? rafiki? Au mpenzi?
 
Back
Top Bottom