Nikaione hali ya Godbless Lema Arusha

Nikaione hali ya Godbless Lema Arusha

Status
Not open for further replies.

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Niko njiani kwenda Arusha kuhudhuria Semina za kiwakili na Mkutano wa nusu mwaka wa Mawakili utakaofanyika tarehe 26 mwezi huu. Nitakuwa Arusha hadi Jumapili ijayo.

Uwepo wangu Arusha utanipa fursa ya kuona hali ya kisiasa ya Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema dhidi ya Monaban wa CCM kuelekea uchaguzi wa Oktoba 25. Hodini wanaJF wa Arusha.
 
lema ana hali mbaya sana this time.
 
Last edited by a moderator:
Hali ya Monaban au kipenda Mollel ni mbaya sana mikutano yake imepwaya sana pamoja na kusomba watu lakini pengo lipo wazi kabisa.Kwa ujumla CCM wanategemea kata ya kati upande wa udiwani.

Niko njiani kwenda Arusha kuhudhuria Semina za kiwakili na Mkutano wa nusu mwaka wa Mawakili utakaofanyika tarehe 26 mwezi huu. Nitakuwa Arusha hadi Jumapili ijayo.

Uwepo wangu Arusha utanipa fursa ya kuona hali ya kisiasa ya Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema dhidi ya Monaban wa CCM kuelekea uchaguzi wa Oktoba 25. Hodini wanaJF wa Arusha.
 
ccm ndo mboga gani huku A-town...tushaachana na hiyo kitu mazee
 
Akipata lema sawa, akipata monaban sawa tu coz wote ni wake EL
 
Nackia hata Mbeya Mjini mgombea wa ccm yupo hoi bin taaban
 
Karibu sana ila ukisika PAAAA ujue limekukosa, sasa hivi hiyo ndiyo style ya policcm kuwatafutia ccm kura, na watu tushazoea kufuta machozi na kusonga mbele. Tunawaumiza kwenye sanduku la kura.
 
Mh wakili karibu sana Arusha, nasikitika kukujulisha utaona mikutano ya Monaban na familia yake ila UKAWA hatuna wa kushindana nae hapa Arusha, kwa hiyo hatufanyi mikutano ya kampeni. Lema anatafuta wabunge majimbo mengine, Bananga nae anapambania wabunge na madiwani sehemu nyingine.
 
Ukitaka mikutano ya lema itakubidi ukeshe sokoni na stand.

Mandhari ya jiji la Arusha ni bendera za ccm na magari ya matangazo ni ya ccm tu.

lema kapigwa na butwaa na mbaya zaidi ameshindwa hata kutekeleza agizo la mamvi la kwenda Tanesko kufuatilia umeme.

Mwisho wa lema Arusha umefika kwani hana alilotekeleza zaidi ya kuongoza maandamano tu akishirikiana na wafanyabiashara ndogondogo kutoka moshi.

Ambulance aliyoahidi haijaletwa na ameishia kuchukua ambulance moja kutoka kwa nassari ili kuhadaa umma.

Machinga complex hatujaiona

Hospitali ya mpya ya manispaa hatujsiona

General tyre hakijaeleweka.

Mama ntilie wako vile vile.

Kwa ufupi lema hana alilotekeleza Arusha na Monaban ndio mbadala wake.
 
Majimbo 3 ya mkoa wa Arusha yaani Arusha mjini kwa Lema,Karatu kwa Qambalo na Arumeru Mashariki kwa Nassari aka Dogo janja hakuna haja ya kampeni zote ni za CDM
 
Ukitaka mikutano ya lema itakubidi ukeshe sokoni na stand.

Mandhari ya jiji la Arusha ni bendera za ccm na magari ya matangazo ni ya ccm tu.

lema kapigwa na butwaa na mbaya zaidi ameshindwa hata kutekeleza agizo la mamvi la kwenda Tanesko kufuatilia umeme.

Mwisho wa lema Arusha umefika kwani hana alilotekeleza zaidi ya kuongoza maandamano tu akishirikiana na wafanyabiashara ndogondogo kutoka moshi.

Ambulance aliyoahidi haijaletwa na ameishia kuchukua ambulance moja kutoka kwa nassari ili kuhadaa umma.

Machinga complex hatujaiona

Hospitali ya mpya ya manispaa hatujsiona

General tyre hakijaeleweka.

Mama ntilie wako vile vile.

Kwa ufupi lema hana alilotekeleza Arusha na Monaban ndio mbadala wake.

Lema hana mpinzani hapa Arusha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom