Nijuzeni mana huwa sielewi

Nijuzeni mana huwa sielewi

Hivi mwanamke kumtongoza mwanaume ni tabia ya kawaida au ni umalaya?
da92610c42940e70ef9f230201b9097e.gif
ef45d7cd1ebc7954bf72ccd1972fe292.jpg
89ac1653da18bdbff20b9199e7dcb5f7.jpg
vyote
 
Ni kitu cha kawaida japo ni nadra sana... lakini pia mwanamke ana moyo na anapenda.. pale hisia zake zinapoangukia kwako... basi akikwambia usishangae.
 
Na ni vigumu sana mwanaume kumkataa mwanamke inapotokea hali kama hiyo, sema mara nyingi mwanamke huishia kutumika tu
 
Haijakatazwa mwanamke kumtongoza mwanaume jamii inachukulia Kama vile binti aliekosa nidhamu lakin sivyo ukimwona mwanaume anatabia njema ukahisi he can make a good husband basi unamwambia kwa adabu tu.

Kuna vingi wanawake tumekatazwa Kama vile tabia ya kununanuna,kutokuwa na shukrani, kukaa Faragha na mtu ambae sio maharimu wako n.k

Yeah true
 
Kila mtu ana haki ya kueleza hisia zake kwa mwenzake hasa mtu anayempenda sema tu mtazamo wa jamii zetu ndo shida. Mwanamke kumtongoza mwanaume haimaanishi ni malaya, huwenda ndo mwanaume pekee aliyempenda. Kumbuka kila mtu ana mtu anayempenda na anaweza kuwa rahisi kwa mtu fulani kwakua tu ndilo lilikuwa hitaji lake au akawa mgumu kwa mtu mwingine kwakua hakumpenda na ndipo jitihada za kumshawishi huyu mtu zinapofanya kazi mpaka akubaliane nawe kisha kukupenda.

Hata malaya anaweza kujifanya mgumu vilevile ili umuone wa maana, wala hataweza kukutongoza lakini utaingia mwenyewe, hivyo basi ikitokea umetongozwa na mwanamke mheshimu na mkubalie kama utampenda au mkatae kwa staha na sababu nzuri maana si lazima uwe nae.

Tukibakia na mtazamo kuwa kila mwanamke anayetongoza mwanaume ni malaya basi maisha ya unafiki na kuigiza hayataisha kwenye jamii zetu.
 
Me sidhani kama ni umalaya ila iliyo mara nyingi wanawake hutumia indirect way kutongoza kwa vitendo na akiona bado huelew hapo sasa ndio uamua kukuambia ya moyoni si umalaya mwanamke kumtongoza mwanaume
 
Haijakatazwa mwanamke kumtongoza mwanaume jamii inachukulia Kama vile binti aliekosa nidhamu lakin sivyo ukimwona mwanaume anatabia njema ukahisi he can make a good husband basi unamwambia kwa adabu tu.

Kuna vingi wanawake tumekatazwa Kama vile tabia ya kununanuna,kutokuwa na shukrani, kukaa Faragha na mtu ambae sio maharimu wako n.k
Kukaa falagha na mtu ambae siyo maharimu wako! Imekaaje hii?
 
Hairuhusiwi kukaa mwanaume na mwanamke wanaoweza kuoana Faragha mipaka ni muhimu na kuchunga hekima btn you two maana mkikaa wawili Faragha haramu inaweza kutokea
 
Sina shaka na uliyoyaeleza yapo sahihi. Tatizizo langu ni matumizi ya neno maharimu, ulivyolitumia kwenye sentensi kanusha.
 
Kila mtu ana haki ya kueleza hisia zake kwa mwenzake hasa mtu anayempenda sema tu mtazamo wa jamii zetu ndo shida. Mwanamke kumtongoza mwanaume haimaanishi ni malaya, huwenda ndo mwanaume pekee aliyempenda. Kumbuka kila mtu ana mtu anayempenda na anaweza kuwa rahisi kwa mtu fulani kwakua tu ndilo lilikuwa hitaji lake au akawa mgumu kwa mtu mwingine kwakua hakumpenda na ndipo jitihada za kumshawishi huyu mtu zinapofanya kazi mpaka akubaliane nawe kisha kukupenda.

Hata malaya anaweza kujifanya mgumu vilevile ili umuone wa maana, wala hataweza kukutongoza lakini utaingia mwenyewe, hivyo basi ikitokea umetongozwa na mwanamke mheshimu na mkubalie kama utampenda au mkatae kwa staha na sababu nzuri maana si lazima uwe nae.

Tukibakia na mtazamo kuwa kila mwanamke anayetongoza mwanaume ni malaya basi maisha ya unafiki na kuigiza hayataisha kwenye jamii zetu.
Na mimi hapa huwa napata ugumu kujua kwamba wanawake hupata vipi chaguo lao? Labda tuseme wanakubali baada ya kushawishiwa na waume walio nao sio chaguo lao.

Sawa, utakuta wengine wanasema humwandalia mazingira ya kumtongoza. Mi hilo silioni tofauti na aliyekutamkia na pengine huyu aliyefunguka huenda akawa na nia ya dhati. Kwahiyo usifikiri kujiweka kimtego ili umnase mwanaume ndo utaonekana wa maana tofauti na yule mwanamke aliyefunguka.
 
Ni kitu cha kwaida saana mwanamke kumtongoza mwanaume kwani hata yy anamoyo
 
Haijakatazwa mwanamke kumtongoza mwanaume jamii inachukulia Kama vile binti aliekosa nidhamu lakin sivyo ukimwona mwanaume anatabia njema ukahisi he can make a good husband basi unamwambia kwa adabu tu.

Kuna vingi wanawake tumekatazwa Kama vile tabia ya kununanuna,kutokuwa na shukrani, kukaa Faragha na mtu ambae sio maharimu wako n.k
umenena vyema sana dadangu....
 
Back
Top Bottom