Nijiue ama? Kutokana na hii picha na hali yangu

Iweje wakristo wabadili Quran marekani na kuipunguza sura zake ili ziendane na kanuni zake ndio useme mimi mwenye kusema nimehifadhi juzuu kadhaa kimakosa. Je yule aliyekojolea Qurran Dar es salaam.

Donald Trump kusema atawatoa waislam Amerika na ya watu kuua albino kwa ushirikina sio mambo makubwa.?

Yamenikuta Yamenikuta Yamenikuta Kijana mwenzio.

Kwa mpandiano wa CD namna hii..........wewe karibia unakuwa plate number mpya.........hebu wahi hospital fasta kabla hujafikia kipengele cha dozi kubwa..............
 
Nimekuonea huruma sana mana inaonyesha wazi kuwa una msongo mkubwa wa mawazo ambayo sio nzuri kwako wala kwa yoyoye.

Hakuna sauti ya Mungu wala nini we nenda hospitali katibiwe mana ukizidi kuchelewa tatizo litakuwa kubwa zaidi.

Halafu nimegundua pia hesabu zinakusumbua sana

Mwisho kabisa concetrate na afya yako Donald Trump wala hao ulowataja hawata kusaidia lolote katika maisha yako. Dini pia weka pembeni kwasasa we unahitaji hospitali tu. Usisahau kumweleza doctor kuhusu hizo sehemu ulizoharibiwa ili wakutibu na usirudie tena kufanya hayo mambo yaliyokuharibu mwili kwa kisingizio cha sauti. (Mwanaume alisema ameharibika mwili mie huwa nna tafsiri moja tu ndomana nasisitiza hosp.)
Tafuta mtu wa saikolojia ili akusaidie kuondoa mawazo ya hiyo sauti ya Mungu fake.
Kila la heri
 
Yani Ni Kwamba Alikwa Mwislamu(Tamsya) Akaamua Kugombea Uongozi Wa Dini, Alivyoshindwa Akaona Bora Awe Mlokole Sasa Akatupa Ktabu Cha Dini Chooni, Ndipo Alipoanza Kuwehuka Huyu, Kwakweli Tunatakiwa Kumsaidia Sana Kwani Anataka Kujiua Ili Aepukane Na Huo Uwehu (sauti Aisikiayo).

nahisi kama huyu mtu ana lengo tofauti na hili aliloliandika.......ila km endapo hayo aliyoandika ni kweli basi ni rahisi sana kutatua changamoto hiyo anayopitia na hii ni kupitia kwa yesu kristo bwana na mwokozi wetu.....Asome MATHAYO:7;7-9
 
Naanza kwa kusema shalom. Tumsifu yesu kristo.

Mimi ni kijana wa umri wa miaka 30. Naishi mkoani Kilimanjaro.

Mwaka huu ni wa saba Tangu nilipoanza kusikia sauti ikiniongelesha. Ilianza tarehe 26 April 2008 ambayo ndio siku yangu ya kuzaliwa. Ilianza kama kunidhihaki huku ikinichekesha kwa vituko huku ikijiita mungu. Mara ya kwanza iliniambia "nenda mbele rudi nyuma tembea simama". Ilianza kunichimbua ubongo kwenye utosi wangu bila uoga. Ninachokuambia ni kweli. Sababu ya msingi inaweza ikawa hii.

" Nikiwa shule siku moja tulikuwa tunaafuta viongozi. Sasa katika hiyo shule mimi na mwenzangu tulikuwa tumetokea shule ya kiislamu. Katika uongozi wa TAMSA mkoa kulikuwa na nafasi wazi. Sasa nikawa nimefika shuleni Kibaha Secondary.

Tukaanza masomo. Wakati tunakabidhiwa uongozi tukaulizwa je mmehifadhi juzuu ngapi. Na kila mmoja akataja. Na mimi nikataja.

Kumbe alikuwa ananitega. Siku nyingine nikawa nimelala usiku nikamuona mtu aliyejifunga vazi la kuhiji. Basi nikagundua kuwa ni MUNGU. Nikamuona amenitupa nyuma ya wenzangu wakati ndotoni tuko assembly grounds.

Nikatupwa nyuma kwa kidole nikaangukia kwa mtu wa tisa kutoka mwisho. Yaani kumbe alikuwa anamaanisha kuwa hiyo ndio position yangu kimatokeo ya mtihani. Paper lilivyokuja tukafanya nikapata two ya kumi na moja.

Basi wakati huo nahisi kichwa ni kizito na chenye uwezo mdogo wa kufikiri ingawa uwezo wa kuelewa masomo upo. Nikarudi nyumbani kufundisha tempo. Nikafikia mwisho wa kufundisha ila sikuendelea na masomo chuo kwa kuwa nilikuwa nimeshaharibwa seheemu kubwa ya mwili.

Nikaanza kujipumzisha kila siku. Na kukata tamaa. Basi nikakaa nyumbani siku hiyo ndio nikaanza kusikia sauti ikiniogelesha. Mimi sijawahi kujua sauti hii ni kwanini ilikuwa ikinielekeza kufanya dhambi na kupenda nifikirie mabaya."

Siku ya siku ikafika. Nikaamka asubuhi nikaenda kumtembelea mtoto wa mjomba wangu akiwa dukani kwa baba yake. Baada ya kuondoka na kurudi nyumbani nikiwa njiani. Sauti ikaniambia umesikika ulipowaza. Kuna kitu niliwaza. Nikakasirika na kuwahi nyumbani na kutupa kitabu cha dini chooni. Nilichukia sana kuambiwa nasikika nikiwaza.

Hadi leo sauti ipo na inasema haitoki. Nikiikemea kwa jina la yesu na Quran haitoki. Mimi naamini huyu ni mungu wa kweli.

Ingawa nina dhambi nikionesha kutubu haitoki. Ni mwaka wa nane sasa.

Iweje wakristo wabadili Quran marekani na kuipunguza sura zake ili ziendane na kanuni zake ndio useme mimi mwenye kusema nimehifadhi juzuu kadhaa kimakosa. Je yule aliyekojolea Qurran Dar es salaam.

Donald Trump kusema atawatoa waislam Amerika na ya watu kuua albino kwa ushirikina sio mambo makubwa.?

Yamenikuta Yamenikuta Yamenikuta Kijana mwenzio.
Unakemea kwa jina la YESU na Quran.?chagua moja na uamini katika hilo moja .mimi nakushauri kwa vile umeitupa hiyo chooni basi mtafute Mungu kwa upya katika Kristo YESU.jisalimishe kwa YESU nawe utapokea ukombozi wa kweli.usiishi katika uvuguvugu,chagua kuwa moto au baridi.!
 
huwezi kupona kwa dini kwa sababu unajaribu kua mkristo na muislam kwa wakati mmoja. kwa kifupi huna imani. chagua moja mwamini kristo kua ni mwana wa mungu alikufa kwa ajili ya dhambi zako, kisha alifufuka kutoka kwa wafu na yuko hai mbinguni kwa baba yake. pia fuata mafundisho yake nawe utaokolewa. yafanye haya ukitoka hospitali kwanza.
 
Mental case coumpanded by delusions
Tangulia Muhimbili kitengo cha afya ya akili
 
haya maluweluwe yako yanafanana na yule yohana wa patmo....
yeye maluweluwe yake akayaita ufunuo wa yohana,,,,,bu...bu......but actually ni tatizo linaloletwa na kulala huku ukiwa hujala kwa mda ,mrefu...
 
Sikufich mkuu hata mm cjaelewa kitu

Me neither. Inawezekana ni kutokana na hali yake. Kuna kijana jamaa yangu alipata matatizo kama hayo njiani akiwa anatoka katika graduation akiwa ktk basi. Tulishauriwa apelekwe kuombewa, mara kwa waganga, but believe me, aliponea Muhimbili kitengo cha magonjwa ya akili na sababu si bangi wala mapepo, bali kuna mambo alikuwa anatarajia kuyafanikisha haraka akaonekana kukwama ikamsumbua sana na Dk akasema pia over- excitement ya kugraduate iliongezea tatizo. Please wahi Muhimbili kijana utapona.
 
Schizophrenia or Bipolar disorder ndio ugonjwa wako. Usipuuzie hata kidogo safari ianze kuelekea hospitali.Kawaida mungu huwa anatusikiliza lakin ukianza kumsikia yeye ujue huo ni ugonjwa wa akili
 
Hakika nakwambia unahitaji maombi. ..una mapepo. ..

Fuata ushauri huu alafu uje utupe mrejesho. ..tatizo lako ni dogo nenda ufanyiwe maombi
 
Hiyo ni NDOTO YA MARUWERUWE...!!!

Sasa, umekuwa kama walokole wakiota, wanajua Yesu amewatembelea...

Ubongo UNATUNZA MEMORY...sasa unachowaza sana sanaaa ndio MARA NYINGI UNAOTA... au unasikia kikiita ktk UBONGO WAKO... infact hakuna sauti wala nini...ni MAWAZO TU YANAKUSUMBUA...

FANYA haya... anza kusililiza music au nyimbo au fuatilia michezo unayopenda na kuongea na kuwaza positives... epuka kukaa mwenyewe kwani hali hiyo inatokana sometimes na kukataa tamaa ya maisha, au ukiwa mwenyewe jaribu kufuatilia habari za michezo uipendayo...!!!

hali hiyo itapotea kabisa...!!!
 
nakubaliana na wewe kabisa, ndugu yetu huyu anaugonjwa wa akili na ninachomshukuru Mungu bado anao uwezo wakujua analo tatizo, na kutafuta msaada.

naomba msimkejeli na kama kuna mtu anayemfaham basi achukue jukumu lakumpeleka pale mawenzi hospital kuna kitengo cha magonjwa ya akili atatibiwa atapona na hatimaye atarudi darasani na kuwa mtu muhimu katika jamii.

ndugu yangu kama utapata wasaa wakusoma ujumbe huu tafadhali sana sana jiandae na uelekee pale mawenzi hospital ukiwa umeambatana na ndugu wa karibu.

ninakutakia matibabu mema na Mungu akupe ujasiri wakuiendea njia iliyo sahihi.


Nimeipenda rai yako mkuu frontline1.

Mkuu Xperience, unaweza kutueleza uko wapi kwa sasa ili mwana JF alie karibu nawe (na atakaekua na muda) akutane na wewe na mzungumze mikakati.

Unahitaji kumuona mtaalam wa magonjwa ya kichwa lakini ukiwa na mwenzio au wenzio wa kukusindikiza inasaidia zaidi.
Pole sana, utapata ahueni lakini unahitaji msaada kwa sasa.

Kwa watakaojitolea kukutana na ndugu yetu tutawasaidia counseling tips kupitia pms.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom