Nigeria wagoma kufanya mazoezi

Nigeria wagoma kufanya mazoezi

kamerun waligoma haikua na sababu maana hakuna walichokua wamefanya lakini kwa naijeria ni haki kabisa na pia wanastahili motisha na wajengwe kisaikolojia maana hatua waliyo ni ngumu sana si ajabu ukaona wenyeji wanabaki watazamaji
Nigeria wanastahiki kwa sababu wameingia raundi ya 16 bora? Hapana. Kila timu inastahiki kupewa haki yao, na kwa wakati. Ujanja wa kusubiri hadi timu itolewe ni kutumia fadhaa ya kutolewa huko na lawama zinazoambatana nako, kuwanyima wachezaji haki yao. Cameroon walikuwa sahihi, kadhalika Ghana. Nawashangaa tunaowaita wachezaji wanaodai chao wasaliti, bila ya kujua kuwa tunahalalisha ulafi wa viongozi wa timu hizo. Ulafi unaoishia kuona tamaa za viongozi ni bora kuliko heshima ya Bara hili. Tuna haki ya kuamini kwamba lau Muntari na Boateng wasingefukuzwa kwa msimamo wa kudai chao na cha wenzao, Ghana wangeifunga Ureno ile legelege na hatimaye kusonga mbele kwa faida ya USA kufungwa na Ujerumani. Lau Boateng angekuwa mroho wa pesa, angesubiri kuchezea timu ya Taifa ya Ujerumani kama ndugu yake, ambako kila mtu hupewa kinono chake na kwa wakati. Lakini mbona kila 'wanapokosa nidhamu' kwa kugoma, fedha zao hupatikana? Kama hiyo ndio dawa ya kupewa haki yao, kila mtu atagoma, isipokuwa mnadhimu wewe, labda!
 
Viongozi wengi wa federation ni wapigaji ndo maana wachezaji inawauma kuona wanapigwa danadana ktk posho na bonus..
 
sijajua uko upande upi!
unamaanisha kwamba kwanini viongozi hawatoi hela hadi watu wagome au
unawalaumu wanaogoma kwa kusema sio kila kitu ni cha kugoma?

mkuu nawashangaa viongozi hawatoi fedha mpaka wachezaji wagome
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom