Nifanyeje?

Habari zenu wapendwa?

Nimepata ajira mpya katika kampuni flani kitengo cha masoko (marketing) kama mjuavyo marketing inahitaji mtu uzunguke sana ukutane na watu sana... nimeanza kupata appointment na watu mbali mbakli wengine hunialika lunch ili tukanegotiate biashara... shida inakuja kwa mpenzi wangu hanielewi kabisa kisikia kuwa nakwenda lunch na mtu flani hasa mwanaume kwa ajili ya kunegotiate biashara anahisi kama hwua kuna mengine zaidi. Mimi kwa upande wangu hwua hakuna cha zaidi isipokuwa ni biashara tu. na iliwahi kutokea kuwa mbaba mmoja alinihaidi kunipa tender flani ila kigezo atoke na mimi. nilikataa na biashara iliishia hapo.

huwa napata wakati mgumu sana katika kufanya marketing ukizingatia mimi ni msichana. naomba ushauri nii-face vipi hii situation pia nimuelewesheje mpenzi wangu anielewe kuwa mimi nipo kikazi na sio vinginevyo? je wadada wenzangu halii hii imeshawakuta? mlii-solve vp?

Asanteni na karibuni kwa michango na ushauri pia.

habari zinajichanganya hapa, hivi tatizo ni mpenzi wako au marketing?. lakini si kweli kutoka toka dinner , ndo kunakufanya uwe active marketer. ni vema hata wewe mwenyewe ujiangalie, kwani kama wewe ndo unauza ninatarajia wewe ndo utoe mualiko wa dinner, etc. au aliye mteja wako pia aweza kukukualika , lakini si suala la kukubali kila mualiko.

ukiachana na mchumba , zingatia pia maadili ya kazi yako. kwa mfano waweza kwenya mialiko ambayo baadae ndani ya kampuni yako wakakuona ulikwenda kushiriki kuhujumu kampuni yako. ki ujumla uwe mwangalifu, si tu kwakuwa mchumba anakaba penati la hasha, hata kwa kazi yako pia. nimeuza kwa miaka mingi nikiwa nafasi ya chini , hata juu. sikuwa na mialiko isiyo na malengo. na asilimia 80 ya mialiko yangu ilitengenezewa file note ( wa potential to business), na 20% ndo ilikuwa kujirusha. sijui kwako ikoje
 
Back
Top Bottom