Nifanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nifanyeje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Luvvy, Apr 23, 2012.

 1. L

  Luvvy Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naombeni ushauri maana kwakweli nashindwa kujishauri kama nisuke au ninyoe.

  Miezi michache iliyopita(haifiki mitano) nilikutana na kaka mmoja sehemu yake ya kazi nikiwa napata huduma pale. Kutokana na kazi yake aligundua kwamba kuna kitu ningehitahi soon toka kwenye ofisi anazofanyia yeye, hivyo akaniambia nichukue namba yake ya simu ili siku nikiwa nahitaji hicho kitu nimtafute ili kurahisisha mambo kwa upande wangu. Sikuona ubaya maana najua nchi yetu hii inaendeshwa na connection kwahiyo nikaichukua. Siku kama tatu nne baadae nikamtafuta kumuuliza angewezaje kunisaidia kwa muda mfupi na nini atahitaji kutoka kwangu , mawasiliano yakaanzia hapo. Ni mcheshi kama mimi kwahiyo kulikua na utani mwingi, ila bada ya kunisaidia(alinifanikishia kazi yangu kwa muda mfupi sana tena bila kuchukua senti yangu) tukajikuta tunakuwa marafiki. Kujuliana hali, kutoka, kucheka na kufurahi mpaka kutembeleana.

  Katika urafiki wetu aliwahi kuniambia kwamba alikua na mchumba hapo nyuma ila waliachana kutokana na familia yake kutokumpenda au kutokumkubali huyo binti. Hakunieleza zaidi kuhusu hilo kwa siku hiyo na mimi nikaliacha, ila aliishia kusema kuwa hakuwa na mtu kwa kipindi hicho nalo nikaliacha hivyo hivyo kwakua sikua nimemfikiria zaidi ya rafiki na mtu wakuflirt nae, haswa baadae ya kuanza kunirushia NAKUPENDA tunapoongea huku nikijua fika ni usanii tu.

  Sasa mwezi uliopita kwenye «mikutano» yetu hii tukafanya mapenzi, bila majadiliano ya aina yoyote ile, yani ilitokea tu. Nilikua sina mtu na nilijua nae hana hivyo sikua na presha wala sikuwa na mawazo ya kuwa ndo tumeshaanza mahusiano japo yeye anauita ule.uhusiano. Siku ya pili nilikua nna safari ya mkoani kwahiyo nikasafiri na nikawepo mbali kwa zaidi ya wiki moja. Mawasiliano yakaendelea kama kawaida mpaka nikarudi. Niliporudi nikaanza kuhisi tofauti, nikaishia kuhisi nna mimba na nikamtafuta nikamwambia uso kwa uso. Alianza kwa kuuliza ikiwa haikua ya mtu mwingine sikuona tabu nikamjibu hapana. Mwisho akaishia kusema ya kua hakukua na ubaya.

  Binafsi nilimhakikishia kwamba sijamwambia ili nimfunge kwa lolote(mahusiano au fedha) ila akadai kua anataka kuwa involved. Akafikia hata kuanza na habari za utakuja kukaa hapa, hili na lile, pia akagusia kabisa kwamba nikitoa atanichukia vibaya sana. Maisha yakaendelea.

  Siku nilipopata uhakika nikamjulisha nadhani ilikua kwa msg. Siku mbili baadae akajitubia kua yeye ana mpenzi. Nikashangaa, kumuuliza kulikoni hakutoa taarifa mwanzo akasema eti sikumuuliza. Ikabidi nimpe live kwamba bila ya kuulizwa mapema kabisa alisema hana na huo utetezi wake ni wa kijinga maana hata mpenziwe akimuuliza hawezi kujitetea hivyo,utetezi wake ukaishia hapo.

  Basi mi nikamjulisha kwamba hana haja ya kuwa na shaka, aendelee na maisha yake na mimi ntaanza yangu mapya bila ya kumhusisha yeye tena kwa lazima. Akaja na hoja ya kumwacha aliyenae ili awe na mimi. Akaniuliza kama ntaconsider kuwa nae(kuishi nae actually) kama ataachana na aliye nae. Nikamjibu kwamba hilo linahitaji muda mimi kufikiria, akasema sawa.

  Mawasiliano yakaendelea kama kawaida, baadae nikaamua kumuuliza kuhusu mpenzi wake huyo aliyeko mbali. Niliyopata ni kwamba ANAMPENDA, HAWAJAWEKEANA MALENGO ila bado wazo la kumwacha kwaajili yangu bado lipo.

  Sasa najiuliza, ni akili kweli kumwacha aachane na mtu anaempenda ili awe na mimi? Sindio mwanzo wa kunyanyaswa na kuchitiwa kila siku? Au hata kusimangwa kwamba sikupendwa mimi, alipendwa mwenzangu?Binafsi hisia zangu ni mchanganyiko, natamani kuwa nae (probability ni kwamba kama angeniambia tuwe kwenye mahusiano kabla ya hili sakata ningesema NDIO) ila nna wasiwasi sana. Sina imani nae, na kama sitokuwa na mahusiano nae nataka kila mtu ajali maisha yake ili kuavoid drama, kwenye hili naona sitokua namtendea haki. NIFANYEJE?
   
 2. g

  gforum Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wewe jiandae kutuanza mtoto mwenyewe, kama vipi kuolewa pia ni vyema ila kwa kuziheshimu isia zako nakushauri ufunge kwa imani ya dini yako ukiri ulimkosea mungu na uombe hekima ya mungu. That is all mungu atakupa hekima.
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Una option?

  Unajua karaha ya kuwa single mom?

  Unacheza wewe.
   
 4. DERICK2000

  DERICK2000 JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtu rafiki tu,unaenda kulala nae.Jifunze kusema No,kwa marafiki,especial wa kiume.ukiona anasitasita na maamuzi yake.ujue kuna jambo hapo..hope u have learned something.hakuna urafiki wa ke na me.wakaachana bila ya kutakana.wapo,but only 2% kati ya 100%.Lea tu mtoto dada.
   
 5. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Najua ni wakati mgumu ila naomba usiitoe mimba kabisa.....
  Mengine yatajipanga yenyewe
   
 6. Mbuty

  Mbuty JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 336
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Oh pole,imekwisha tokea,una kiumbe tayari,cjafahamu future yako ikoje i mean kama unafanya nni for survival. Kuna kuishi pa1 na kuna ndoa,sasa wwe ndio unamjua vizuri kama anakupenda au la! Kama anakuja kwako coz anakupenda and he's not feeling pity that's ok if not well pana shida kidogo. Follow ua heart mpendwa.
   
 7. kapistrano

  kapistrano JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,204
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Bado unayo nafasi ya kutulia na kumsoma jamaa kisaikologia then utaoberve na usionesha sn kuwa bila yeye wewe si kitu ukishagundua msimamo wake chukua hatua kwani cku zote mtu anaechukua mamuzi magumu huwa anafanikiwa.
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  kama umeamua kuzaa, zaa ulee mwanao. Akija huyo mwanaume sawa, asipokuja ni sawa.

  Halafu dada hujipendi wala hujithamini, maradhi yote haya, unacheza peku peku ili iweje?
   
 9. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  mnh kama una kazi ya kukuingizia kipato na hivyo kumudu kumtunza mwanao...sioni sananu kwa nini unang'ang'a niana na huyo looser,hana msimamo na kisha muongo....akikuoa akimpata mwingine wa kumzuzua atawachanganyeni na siku hizi magonjwa nje nje.......................................................................kisha na wewe kama umeamua kulala na mwanaume tumia protection kha,mimba unaweza kulea kama hivyo je kama kakuachia ukimwi??? mtu ambaye unajua ana mahusiano na mtu utajiachianaje kirahisi hivyo???:rolleyez::doh:
   
 10. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Huu umalaya sijui mtauacha lini nyie mabint wa kileo,asa mtu ni rafki tu,unaenda kumvulia chupi?enewei,ndo faida hyo,lea huo mzgo wako mwenyewe.
   
 11. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Utata sports club ushavinjari hapo!
  Unafahamu nikisema neno, TAHREER SQUARE?
  kama jibu ni ndiyo basi chukua hatua couple yako na huyo mwanaume ni mtihani ambao haujatungwa!
   
 12. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Sema shida ni kula kavu....mh
   
 13. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Aseme No wakati anataka; what do u take women for? Wanshangaza!
   
 14. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Huyo mwanaume si malaya? Naye si alivua nguo, au kuvua nguo ni haki ya kina kaka tu?

  Atalea na uwezo anao; what's ur problem? Wewe kila siku unakuja na miuzi ya wanawake tofauti tofauti, malaya mkubwa wewe!
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  like like
   
 16. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Good point; bidada fuata huu ushauri!
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Asante Kaunga. . .
  Kuna watu wana maudhi. . .huyo jamaa kila siku ana jipya trna yasoeleweka ila bado anaona ana haki ya kumwaga matusi na kuhukumu kana kwamba yake hua ni mazuri au ya maana zaidi.

  MWENYE mada. . .
  Maisha hayaishi baada ya kupata mimba. . kuna maisha baada ya hapo!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. k

  kisukari JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  kwanza hongera kwa kuwa mja mzito.lakini,mwanzo kabisa ulisema ulimchukulia mtu wa ku flirt nae tu,na hukuwa nae serious.na juu ya hivyo,usingemvulia nguo,na juu ya hapo condom jamani muhimu.unless muwe mmepanga tukienda peku peku,kuna matokeo haya na haya.anyway yameshatokea,kwa upande mwengine wa shilingi,huyo jamaa ni tapeli,atakuchanganya akili yako.kama uwezo unao,jipange mwenyewe focus na uja uzito wako.maana leo anakwambia huyo mwengine anampenda.ukae ukijua mtakua mna share,au laa kama upo tayari ku share
   
 19. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Lizzy
  Yaani amenichefua sana; kweli dada kachemsha na kwa maoni yangu si kiasi kikubwa kama mkaka, (kwani mkaka alikuwa na relation nyingine) lkn lijitu linaloongoza kwa uzinzi (according to his threads) linakuwa la kwanza kumuita dada ambaye naye ana right ya kupenda na hata kumake a mistake Malaya!

  Halafu pia hii mentality ya kuwa wanawake tunapaswa kubrmbelezwa ndio tuingie kwenye mahusiano inaniudhi sana, iko so fake. Nikikupenda hata kama nitashindwa kukuambia; nitakuonesha. Na likiharibika, l have myself to blame!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. petrinamwana

  petrinamwana JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 878
  Likes Received: 258
  Trophy Points: 80
  Mambo yasikute wewe tusome tu mitandaoni yakiwa kwako utatamani uvue pichu uvae kichwani
   
Loading...