Hongera kwa kiomba ushauri kwani huu ni uamuzi sahihi, nami naomba nichangie kadili ya maelezo yako.
Lakini kwenye andiko lako hujatuambia umri wako na wake. Katika maisha yangu ya kutoa ushauri Mara nyingi nazingatia sana umri,kwasababu kuna baadhi ya ishu huwa ni za utoto tu. Mfano hii ya jamaa yako kuzira baada ya kuambiwa hatumii akiri. But ngoja nichangie kidogo.
Inaonekana kuna sintofahamu kati ya ndugu zako na huyo jamaa, kinachosababisha huo mgogoro ni huo urafiki wenu. Wao wanakilinda wewe kama ndugu yao,na kwasababu ulimtambulisha kwao ni rafiki basi nao wantreat kama rafiki yako na ndio maana ni wakali ili kukulinda. Ungewaambia ukweli toka mwanzo labda ungepunguza na kuondoa sintofaham hii.
Mchumba wako alijiegesha kwa uzi wa buibui. Kunakitu kinaendelea kati yenu ambacho kinamkera mmoja wenu, hivyo huyo mchumba wako alikuwa anatafuta kijisababu cha kuharibu uhusiano wenu. Baadhi ya sababu ninazo fikiri kuwa ni chanzo cha hayo ni
A. Labda ulimwambia no kufanya mapenzi mpaka ndoa,
B. Hujiwezi uwanjani na amekuchoka
C. Umepoteza mvuto kwake,
D. Kampata mwingine na alitaka apate kanafasi ka kuvunjia uhusiano
E. Huenda alichokitaka kesha pata na hana hamu na wewe
F. Huenda nyie wote ni watoto ndio maana mnazira kwa ishu za kijinga tu. Rejea sababu maelezo yako, eti kuambiwa atumie akiri anazira hahahahahaha
G. Labda alipigwa biti na kaka zako juu yako na kutishiwa kutekwa na kuteswa kama akiendelea kuwa nawe
Possibilities hizo ni zangu tu kwani ni siri yenu wewe na yeye. Lakini nimejikita huko kwasababu ishu iliyopelekea tatizo hili ni dogo sana kwenye ulimwengu wa mapenzi. Yaani mtu uambiwe hutumii akiri ndio ususe!! Watu wanapigwa,wanatukanwa,wanafanyiwa figisu za kila aina bado wana kaza tu.
Yakufanya kwasasa
1: Kaa nae na umwambie atoe suluhisho mapema ili kama uhusiano umefika mwisho ukajua kabisaa
2:Rasmisha mahusiano yenu hata kwa baadhi ya ndugu km mashangazi au bibi kwa pande zote. Akikataa vunja mahusiano
3: Waeleze kaka zako uhusiano wenu nje ya urafiki,ila kama wewe ni mwanafunzi pole yako.
4: Wakutanishe kaka zako na huyo jamaa ili kusuruhisha ugomvi wenu
5: Vaa moyo wa ujasiri na uwe na moyo wa kufanya maamuzi magumu ikibidi,maana huyo jamaa si salama kwa maisha yenu ya ndoa kwa baadae.
6: Jaribu kuwa karibu na mwenzi wako na kumfariji, huenda akakupa sababu ya yeye kubadirika.
Akikataa jua hiyo sababu ya kuvunja mahusiano yenu.
Binafsi nimeishia hapo