nifanyeje ajue nampenda

happy amos

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
251
Reaction score
434
was 2010 nilipomaliza chuo nikaenda field nikakutana na kijana mmoja uongo mbaya nilitokea kumpenda sana tena sana sana sana, kama kawaida ningum kwa mwanamke kutamka na kingine sikua type yake kwani nilijaribu kumuuliza kimaongezi anapenda mwanamke wa aina gani sifa alizozitaja sikua nayo hata moja, hichi ndicho kilichonitia hofu zaidi nikaogopa kumuonyesha hisia zangu, basi nilibaki na maumivu yangu bila kumwambia mtu nilishindwa nifanyeje kwani kila nikimuona nilikua mnyonge sana nikaamua niende kwa mganga akanilia tu hela zangu sikufanikiwa, nikaamua kitu kimoja ili kujiridhisha nikatafutta lain mpya nikabadirisha na jina na sauti nikawa na mawasiliano na yeye ya kimapenzi bila yy kujua kama alikua anawasiliana na mimi mpaka nikateka hisia zake ikafikia hatua anataka tuonane nikawa namzungusha mpaka sasa miaka inaenda mi 3 sasa, kwa upande wangu mimi mhusika nikaamua nikaweka mazoe naye ya karibu ya kuheshimiana akawa ananiita mamdogo kiutani mpaka sasa tumekua family friend ndugu zake wananijua kama mamdogo wa kirafiki ndugu zangu wanamjua kwani kwangu huwa anafika na ananiheshim sana,nikawa nampa zawadi na pesa nyingi kwa kisingio kuwa nimepewa na yule feki sasa, nashindwa nifanyeje nampenda sana namaanisha nashindwa nifanyeje kwani tayari tupo kama ndugu sasa, leokaniandikia msg kapata girlfriend mwingine baada ya aliekua nae kushindwa kuonana nae kwa miaka mi3 sasa amambae ni mm fake, nifanyeje ndugu zangu nampenda sana nashindwa kulala mpaka sasa ni saa 7 usiku sina usingizi namfikirianashindwa kumwambia kwa sababu kuu 2
1. sina sifa za kua nae
2. tayari tuna mahusiano kama ndugu na aniheshim sana mpaka ndugu zangu wanamjua na kumheshim nifanyeje
 
ukimweleza hisia zako na jinsi ulidhamiria kuwa nae atakuelewa
jikaze mtoto wa kike hizi ni zama za uwazi na ukweli
dhana ya kusema mwanaume ndio akuanze ishapitwa na wakati.
 
oi subiri kupambazuke ili tuongee vizuri nijue haswa shida yako ni ipi? kupenda na kutamani
 
jaman! We mwambie tu uone reaction yake, guys huwa hatuna complications sana yani.
 
Mwache mwanaume akupende,mwanamke ukipenda sana utajikuta unaumia.hakuna raha mwanaume akikupenda kukutafuta kukulilia Ina umuhimu wake.Tulia God timetable is the best honey .Good things comes for those who waits.yaani hapa nikipika chai mume wangu anahisi naungua,
 
nahisi nimechelewa kumwambia sababu ya ukaribu tulio nao like ndugu kwa mtu asieelewa atajua ni ndugu yangu kwani naishi arusha yeye anaishi Dar lakini huwa anaaga kwao anakuja kunisalimia na kufikia kwangu/ kwetu na wanamchukulia kama ndugu akiwa anashida anaweza amwambia hata mama yangu kwani anamwita bibi na yeye anamchukulia kama mjukuu! what if! nikimwambia akakataa akachukia unafikiri itakuaje ndugu hawawezi shtuka da!!! sijui nisemeje mimi nampenda kuliko chochote mimi istoshe mimi sio type yake jaman
 
Sasa kama wajijua siye type yake kwann unasisitiza kutaka kuwa naye? Pia umesema ana girlfriend so unataka kuwatenganisha au plan yako ni nini? Sidhan kama unampenda as u say....
 
Mie naona mwambie tu kila kitu bila kuficha chochote pamoja na hilo la kumuuliza kwamba anapenda mwanamke wa aina gani na alipokujibu ukajiona huna sifa hata moja na pia hayo mawasiliano yenu ya miaka mitatu na hata kumzungusha alipokuomba mkutane rasmi. Ila utangulize samahani ya kutoka moyoni kwako maana hilo la kucheza na moyo wake kwa miaka mitatu linaweza kumuumiza sana na hata kuuvunja undugu wenu. Siku zote msema kweli ni mpenzi wa Mungu, kama umeamua kufunguka hapa jamvini sidhani kama utashindwa kufunguka kwake. Kila la heri.
 

Labda kuna kitu sijaelewa hapa, what makes you think that wewe siyo type yake?
 
 
Ulichelewa kuomba jamvi kabla ya wenzio,ujanja kupata na si kuwahi, pole weye!!!
 
Dogo acha upuuuzi wako wa kujaribu Kumwambia blah blah blah zako kuwa unampenda na what!!!!!!!!! Trust me its a Party Pupper!!!!!!!! Yaani utam turn off kabisaaa na wewe na atakupa flat NO!!!!!!!! Hali si mbaya sana kama kakuandikia sms ana new GF!!!!!!!! Hiyo inaonesha kuwa NAKUREMIND THE OFFER STILL STANDS INCASE YOU WANNA JUMP IN!!!!!!!!!!

Cha kufanya na wewe sms, im so lonely nimebreak up na my BF!!!! Iwould enjoy ya company jaani katika hiki kipindi kigumu!!!! Usikilizie! If ukipata appointment LOOSE CONTROL BABY!!!!!!!!!! GET WILD!!!!!!! Hapo utazisingizia stress za kuachwa na pombe!!!! (Ndo maana siachi pombe mwenzio, naisingizia mambo kibao!!!!!!!!) Usitamke Nakupenda blah blah blah!!!! You are too old for NGOJERAS!!!!! We onesha matendo tuuuu!!!
 
Alichokushauri lara 1 ni kizuri.Unaweza kuongezea na hili..Tafta line ingine asiyoijua fanya kama ulimuhadithiaga mtu fulan kuhusu unavyompenda huyo kijana na sasa huyo mtu kaamua kukupasulia ukweli wewe yan kama amefanya umbea fulan kumjulisha hvo.Mfano...CHALII,KIJANA ..BORA NKUPE SIRI HII HUYU DEMU AMBAYE UNAMUITA MAMA MDOGO KWA KWELI HAJIWEZ JUU YAKO ILA NDO HVO WASICHANA HAWAWEZ KUSEMA PLUS MNAHESHMIANA SANA.ALISHAWAH KUNIELEZA HAYA NA LEO KANIELEZA TENA KUWA AMEJIHSI DUNIA KUMUELEMEA ULIPOMWAMBIA UMEPATA NEW GF .USINIULIZE MIMI NAN ILA AMINI NIKUAMBIAYO.FANYA UAMUZ SAHIHI KWA ANAYEKUPENDA KWA DHATI. BYE.Ukimaliza kutuma ile mesej toa line alaf kaa hata siku 2 uiweke tena kujua amejibuje na hata kama hajajibu ujumbe keshaupata.Usije ukajaribu kumwambia upuuzi ulofanya kwa miaka mi3.Utamkosa.Fanya hvo urud ku2pa majibu
 
Mbona simpo! Mwonyeshe kibubu atakavyochangamka

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 

na pia akija mtengeneze mazngira amwage sumu zake
 

Wewe hujatuliaaaa kabisaaa upo Kama nyani ngadu... au ni mmeo
 

Jibu kamili ni hapo kwenye RED, tafadhali sana usimharibie wewe endelea na uhusiano wa ki udugu ulioutengeneza. Biashara asubuhi jioni mahesabu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…