Nifanye nini ndugu zangu

Nifanye nini ndugu zangu

wewe hebu soma achana na habari za kuunganisha vikojoleo
 
Wadau naomba mnisaidie.Mwezi wa sita mwaka huu nilimaliza kidato cha sita kisha nikapangiwa kwenda jkt kwa mujibu wa sheria.Nikiwa huko nilikutana na binti kutoka Iringa ambaye nilimpenda sana ila sikumwambia kwa kuwa kule JKT unaweza ukapewa adhabu mbele ya watu wengi hivyo sikuhitaji mpenzi ili niwe huru kwaiyo mimi na binti yule tuliishia kuwa marafiki wa kawaida.

Maisha yaliendelea pale kambini binti yule alikuwa ananisaidia kwenye shida ndogo ndogo na mimi pia nilimsaidia.Ilipofika siku ya kuondoka nilimtafuta sikumuona nikaamua niondoke zangu ila nikiwa nje ya geti ghafla binti yule nilimuona akitoka ndani akafika eneo nililopo na akaniambia kwaheri akapanda piki piki faster na kuondoka sikupata hata muda wa kumuomba namba.

Baada ya hapo nilirudi nyumbani Dar ila nikiwa Dar nilipewa namba ya rafiki yake wa karibu na mtu fulani.

Nilimuomba rafiki wa binti huyo anitumie namba ya binti huyo na akanitumia.Kipindi hiko post za chuo zilikuwa zimetoka na mimi nilikuwa nimechaguliwa chuo kikubwa Tanzania nzima kilichopo mkoani dodoma.

Nilipomuuliza binti chuo alichochaguliwa na yeye alichaguliwa hapo ila coz tofauti na yangu ila rafiki yake alichaguliwa hapo kozi moja na mimi.

Siku ya siku nilienda kuripoti chuoni kabla yake yeye na rafiki yake.Baada ya muda mfupi na yeye aliripoti ila alifikia mjini kwa ndugu zake kwa kuwa hakukamilisha usajili ila badae akafika chuoni.

Kuna siku nilimuomba tuonane akaniambia niende kwenye hostel zao na ni mbali kutoka nilipo ingawa chuo ni kimoja ila college tofauti umbali wake ni kama Buguruni na Mnazi Mmoja mana chuo hiki ni kikubwa Dodoma na Tanzania nzima.

Nilipofika kule alikuwa hapokei simu niliporudi nikamtumia sms ya kumlaumu na nikamwambia siongei nae tena akaniomba msamaha na nikamsamehe.

Kesho yake nikaenda tena nikiwa nimependeza nilipofika nikaenda hadi hostel kwao hadi chumba chake alikuwa peke yake.

Alinikaribisha kiti na yeye akakaa kitandani.Alinisifia nimependeza pia akasema ana matatizo mana amekuta vitu vya ajabu kwenye diary ya boyfriend mimi nikamtongoza akawa anakataa na akaniambia mimi ni handsome hataki presha mana mabinti wengi watanipenda mwisho akasema atanijibu.

Nilimtafuta usiku akasema haiwezekani na kesho yake akaniambia anaye boyfriend.Nikamuuliza ina maana mimi hunipendi akasema ananipenda sana ila hawezi kumiliki watu wawili nikimsumbua sana anaacha kuchati.

Ndugu zangu nifanye nini huyu binti nampenda sana silali kwa raha kwajili yake.

yaani nimesoma nikajikuta tu nacheka
kwanza uandishi mbovu then kisa hakieleweki vizuri.
Anyway umenifanya nianze ku imagine mazingira ya udom.
Humanities na Ng'ox labda ndo umbali unaosema wa buguruni na m/ mmoja.
 
Ukishamaliza chuo na GPA 2.1 ndo utajua raha ya kusoma chuo huku ukiwa na demu. All the best
 
afu UDOM hujasoma peke ako mkuu umekisifia weee kama nini sijui bai ze wasalimie ng'ong'ona afu demu humanities hahahaaaaaa si bure ndio ulipo ryt now
 
afu UDOM hujasoma peke ako mkuu umekisifia weee kama nini sijui bai ze wasalimie ng'ong'ona afu demu humanities hahahaaaaaa si bure ndio ulipo ryt now
Poa ntawasalimia hadi kijijini kwa wajasi
 
yaani nimesoma nikajikuta tu nacheka
kwanza uandishi mbovu then kisa hakieleweki vizuri.
Anyway umenifanya nianze ku imagine mazingira ya udom.
Humanities na Ng'ox labda ndo umbali unaosema wa buguruni na m/ mmoja.

Mkuu ulitaka niandike vipi kwa lugha ya kwetu mtu kama wewe tunakuita mdashi,
 
Usiwe king'ang'anizi wewe kama amekutolea nje mpotezee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom