Nifanye nini ndugu zangu

Nifanye nini ndugu zangu

swahili state

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2014
Posts
261
Reaction score
146
Wadau naomba mnisaidie.Mwezi wa sita mwaka huu nilimaliza kidato cha sita kisha nikapangiwa kwenda jkt kwa mujibu wa sheria.Nikiwa huko nilikutana na binti kutoka Iringa ambaye nilimpenda sana ila sikumwambia kwa kuwa kule JKT unaweza ukapewa adhabu mbele ya watu wengi hivyo sikuhitaji mpenzi ili niwe huru kwaiyo mimi na binti yule tuliishia kuwa marafiki wa kawaida.

Maisha yaliendelea pale kambini binti yule alikuwa ananisaidia kwenye shida ndogo ndogo na mimi pia nilimsaidia.Ilipofika siku ya kuondoka nilimtafuta sikumuona nikaamua niondoke zangu ila nikiwa nje ya geti ghafla binti yule nilimuona akitoka ndani akafika eneo nililopo na akaniambia kwaheri akapanda piki piki faster na kuondoka sikupata hata muda wa kumuomba namba.

Baada ya hapo nilirudi nyumbani Dar ila nikiwa Dar nilipewa namba ya rafiki yake wa karibu na mtu fulani.

Nilimuomba rafiki wa binti huyo anitumie namba ya binti huyo na akanitumia.Kipindi hiko post za chuo zilikuwa zimetoka na mimi nilikuwa nimechaguliwa chuo kikubwa Tanzania nzima kilichopo mkoani dodoma.

Nilipomuuliza binti chuo alichochaguliwa na yeye alichaguliwa hapo ila coz tofauti na yangu ila rafiki yake alichaguliwa hapo kozi moja na mimi.

Siku ya siku nilienda kuripoti chuoni kabla yake yeye na rafiki yake.Baada ya muda mfupi na yeye aliripoti ila alifikia mjini kwa ndugu zake kwa kuwa hakukamilisha usajili ila badae akafika chuoni.

Kuna siku nilimuomba tuonane akaniambia niende kwenye hostel zao na ni mbali kutoka nilipo ingawa chuo ni kimoja ila college tofauti umbali wake ni kama Buguruni na Mnazi Mmoja mana chuo hiki ni kikubwa Dodoma na Tanzania nzima.

Nilipofika kule alikuwa hapokei simu niliporudi nikamtumia sms ya kumlaumu na nikamwambia siongei nae tena akaniomba msamaha na nikamsamehe.

Kesho yake nikaenda tena nikiwa nimependeza nilipofika nikaenda hadi hostel kwao hadi chumba chake alikuwa peke yake.

Alinikaribisha kiti na yeye akakaa kitandani.Alinisifia nimependeza pia akasema ana matatizo mana amekuta vitu vya ajabu kwenye diary ya boyfriend mimi nikamtongoza akawa anakataa na akaniambia mimi ni handsome hataki presha mana mabinti wengi watanipenda mwisho akasema atanijibu.

Nilimtafuta usiku akasema haiwezekani na kesho yake akaniambia anaye boyfriend.Nikamuuliza ina maana mimi hunipendi akasema ananipenda sana ila hawezi kumiliki watu wawili nikimsumbua sana anaacha kuchati.

Ndugu zangu nifanye nini huyu binti nampenda sana silali kwa raha kwajili yake.
 
Una-mbwe mbwe jombaa.....Mara UDOM chuo kikubwa sana Dodoma na TZ nzima mara kakuambia we ni Handsome....Anyway back to the topic komaa nae kama mwaka mzima hivi hapo ndo utaweza kata tamaa, Raha ya mapenzi ni kusumbuana si yule unakutana nae kwenye daladala unatongoza na unashuka nae saa hiyo hiyo Guest....Hapo ndo pakuchua ma-xperience.
 
tafuta mwingine kwani vigezo unavyo maana wewe ni handsome
 
Kumbe UDOM ni chuo kikubwa Tanzania nzima aiseeee, sasa wewe amekuambia ana boifrend unaendelea kung'ang'ania au unataka kuwa wapembeni hivyo hivyo?
Natamani kuachana nae ila moyo unashindwa mana nampenda kwa dhatiani
 
Kumbe UDOM ni chuo kikubwa Tanzania nzima aiseeee, sasa wewe amekuambia ana boifrend unaendelea kung'ang'ania au unataka kuwa wapembeni hivyo hivyo?

Natamani kuacha kumsumbua ila moyo unakataa mana nampenda kwa dhati
 
Wadau naomba mnisaidie.Mwezi wa sita mwaka huu nilimaliza kidato cha sita kisha nikapangiwa kwenda jkt kwa mujibu wa sheria.Nikiwa huko nilikutana na binti kutoka Iringa ambaye nilimpenda sana ila sikumwambia kwa kua kule jkt unaweza ukapewa adhabu mbele ya watu wengi hivyo sikuitaji mpenzi ili niwe huru kwaiyo mimi na binti yule tuliishia kuwa marafiki wa kawaida.Maisha yaliendelea pale kambini binti yule alikuwa ananisaidia kwenye shida ndogo ndogo na mimi pia nilimsaidia.Ilipofika siku ya kuondoka nilimtafuta sikumuona nikaamua niondoke zangu ila nikiwa nje ya geti gafla binti yule nilimuona akitoka ndani akafika eneo nililopo na akaniambia kwaheri akapanda piki piki faster na kuondoka sikupata hata muda wa kumuomba namba.Baada y hapo nilirudi nyumban dar ila nikiwa dar nilipewa namba ya rafiki yake wa karibu na mtu flani.Nilimuomba rafiki wa binti huyo anitumie namba ya binti huyo na akanitumia.Kipindi hiko post za chuo zilikuwa zimetoka na mimi nilikuwa nimechaguliwa chuo kikubwa Tanzania nzima kilichopo mkoani dodoma.Nilipo muuliza binti chuo alichochaguliwa na yeye alichaguliwa hapo ila coz tofauti na yang ila rafiki yake alichaguliwa hapo koz moja na mimi.Siku ya siku nilienda kuripot chuoni kabla yake yeye na rafiki yake.Baada ya mda mfupi na yeye alilipoti ila alifikia mjini kwa ndugu zake kwa kua hakukamilisha usajili ila badae akafika chuoni.Kuna siku nilimuomba tuonane akaniambia niende kwenye hostel zao na ni mbali kutoka nilipo ingawa chuo ni kimoja ila college tofaut umbali wake ni kama buguruni na mnazi mmoja mana chuo hiki ni kikubwa dodoma na Tz nzima.Nilipofika kule alikuwa apokei simu niliporudi nikamtumia sms ya kumlaumu na nikamwambia siongei nae tena akaniomba msamaha na nikamsamehe.Kesho yake nikaenda tena nikiwa nimependeza nilipofika nikaenda hadi hostel kwao hadi chumba chake alikuwa peke yake.Alinikaribisha kiti na yeye akakaa kitandan.Alinisifia nimependeza pia akasema anamatatizo mana amekuta vitu vya ajabu kwenye diary ya boyfriend mimi nikamtongoza akawa anakataa na akaniambia mimi ni handsome hataki presha mana mabinti wengi watanipenda mwisho akasema atanijibu.Nilimtafuta usiku akasema haiwezekani na kesho yake akaniambia anaye boyfriend.Nikamuuliza inamana mimi hunipendi akasema ananipenda sana ila hawezi kumiliki watu wawili nikimsumbua sana anaacha kuchat ndugu zangu nifanye nini huyu binti nampenda sana silali kwa raha kwajili yake.

Acha upuuzi wewe. Kazania masomo yako. Huyo binti ataolewa na watu wengine kabisa, ambao tayari wana kazi zao za maana. Nakushauri uachane naye mara moja. Unapoteza muda wako. Ukiendelea kumfuatilia Utajuta mbele ya safari.

 
Una-mbwe mbwe jombaa.....Mara UDOM chuo kikubwa sana Dodoma na TZ nzima mara kakuambia we ni Handsome....Anyway back to the topic komaa nae kama mwaka mzima hivi hapo ndo utaweza kata tamaa, Raha ya mapenzi ni kusumbuana si yule unakutana nae kwenye daladala unatongoza na unashuka nae saa hiyo hiyo Guest....Hapo ndo pakuchua ma-xperience.

Kwaiyo akiendelea kusema ana mtu nimwambieje
 
Mwambie huyu bwana mdogo maana naona hajitambui na hajui yupo chuo kufanya nini? Analeta akili za A - level wakati yupo chuo.
 
Tatizo upo chuo kikubwa kuliko vyote tanzania alafu ulivalia ukapendeza
 
Aaaaaah! ni shida,muacheni dogo wa watu,ndo impacts za u-teenegers hizo,akikua ataacha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom