Duduvwili
JF-Expert Member
- Jan 31, 2015
- 3,905
- 3,821
We jamaa umeongea point japo utapingwa sanaUsikimbie mkuu, watu wanaoishi maisha ya aina yako tuko wengi.
Muda unaotumia kutafuta uhamie wapi bila kuwa na uhakika wa kupata au kukosa heri uendelee kupambana ndani ya nchi yetu
Hawa mabwana kuna wakati ukifikiria sana unaona hata huu mfumo wa elimu ya kukariri bila vitendo waliotuletea na kutushurtisha kuufata ulikua mpango wa kutuchelewesha kujitafuta sisi na rasilimali zetu.
Na matokeo yake tunayaona maisha magumu baada ya kumalizia miaka karibu 20 shuleni bila kuwa na chochote mfukoni, na kibaya zaidi bado tunawaona wao ndio kimbilio letu na suluhu katika ugumu wa maisha bila kuona vile wenyewe wanavyokimbilia rasilimali zetu zenye thamani zaidi ya hayo makaratasi yao kwa sababu tunashindwa kuzitumia
Wacha twende na John Pombe Magufuli yeye anatuwazia mema sana kuliko tunavyodhani
Cc magu2016 kuna ndugu anataka kuhama nchi huku...