Maxmax72
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 530
- 981
Wakuu kwema?
Kwanza naomba niseme kuwa Mimi ni Mzalendo wa nchi yangu lakini pia ni kijana ambaye ni mchakarikaji wa kila kazi halali.
Ingawa ni mhitimu wa shahada ya kwanza ajabu ni kuwa huu ni mwaka wa tatu sina kazi rasmi zaidi ya kupangaiza tu kwenye vibarua kama vya ujenzi, uvuvi, kilimo na kila kazi iliyo halali, lakini bado sioni mwanga wa kuyaweza maisha na kuishi katika ndoto zangu.
Imefika pahala nikakumbuka hata Mungu alivyotuumba wanadamu hatupangia sehemu moja tu ya kuishi kwamba kwavile mimi nimezaliwa Kigoma ni lazima niishi na kufia Kigoma na sasa nimekuwa nikitafuta kila namna ya kutoka nchi hii nikajaribu na kwingine na nchi zilizo katika ndoto zangu ni Ulaya, Canada na Marekani.
Nimekuwa nikisoma na kuufatilia Nimeona siyo rahisi kuhamia nchi hizi kwa urahisi kwani wana masharti magumu sana hasa kwa watu masikini, lakini nimekaa na kuwaza siwezi kupata Viza kama mkimbizi wa kisiasa hasa kwa wakati kama huu ambapo dunia inajua Tanzania kuna kila aina ya ukandamizaji wa wanasiasa wa upinzani?
Je, nifanyeje na nijiandaeje ili niende kwenye Moja ya balozi hizi kama mkimbizi wa kisiasa?
Naombeni msaada wa mawazo maana naamini hakuna kisichowezekana na isitoshe mimi sitokuwa wa kwanza kufanya hivi.
Karibumi kwenye mjadala na mwenye kejeli ongeeni sana lakini kiukweli wasomi nchi hii hatuna maana tena kwani maisha mazuri tunayasikia tu kwa mwenye mamlaka.