Hapa kuna mawili kaka.
1. Unaweza ukatoa "kibubu" kwa maafande wote hao wawili, yakaisha, au
2. Andika barua kwa Mkuu wa Trafiki wa Kituo Husika, kisha weka nakala kwa watu hawa wafuatao:
a) Kama uko Dar es Salaam, nakala 1 weka kwa Mkuu wa Trafiki wa Wilaya na nakala ya 2 iweke kwa Mkuu wa Trafiki wa Mkoa
b) Weka nakala 1 kwa IGP na nakala nyingine 1 weka kwa Ofisi ya Mkoa/Wilaya ya PCCB.
Kisha kaa usubiri na kusikilizia moto wake.
Hawa jamaa huwa wanajifanya wajanja, haswa katika ngazi za chini. Wanatugeuza sisi raia kuwa mradi wao. Lakini ukiandika barua kulalamika ngazi za juu, utaona jinsi watakavyoogopa. Hawapendi kabisa mambo yafike huko juu, kwani wanakuwa wanawaumbua na kuwaaibisha viongozi wao wa juu.
Kwa mujibu wa "kanuni zisizo rasmi" ndani ya Jeshi la Polisi, ni "kosa la jinai" au "utovu wa nidhamu" kwa askari wa ngazi ya chini "kushindwa kumalizana" na "mteja wake" (wewe hapo) na kusababisha mambo yaende ngazi za juu.
Niliwahi kuandika barua iliyomfukuzisha kazi askari mmoja wa cheo cha Inspekta. Kwa hiyo tumia kalamu yako. Kama huwezi kuandika vizuri, tafuta mtu akusaidie kurekebisha vizuri lugha, ieleweke kwa wepesi na ufasaha.
Kila la heri.