Nifanyaje niachane na ubashiri?

Nifanyaje niachane na ubashiri?

Waungwana, poleni na majukumu yenu, enzi hizo nilikuwa mlevi wa pombe lakini kimaajabu tu nikaweza kuacha, nikahamia kwenye sigara, huko nako nikapambana nikaweza kuacha kabisa!

Sasa si ndio nikaanza kubet! Waungwana nmekuwa mlevi mbwa wa kubet! Yaani nabet kila siku, makampuni karibu yote nimejisajili! Mbaya zaidi napigwa kila siku hasa nikiweka dau kubwa, nkiweka dogo angalau napata ya kubrashia viatu!

Waungwana nifanyeje niachane na huyu sheitwani? Maana kama jana Liverpool na Man U wamenichakaza haswaaa!!! Msaada majamaa!!
Ile 30,000/= ya yule mama wa vicoba ndiyo uliitumia kubet?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Siachi kubeti, hata hivi sasa nimebeti matokeo ya mechi fulani yawe 2-3, na hadi sasa matokeo yako hivyo zimebaki dakika 10, nisaidieni kushika nyeti yabaki hivyo hivyo jamani!
 
Siachi kubeti, hata hivi sasa nimebeti matokeo ya mechi fulani yawe 2-3, na hadi sasa matokeo yako hivyo zimebaki dakika 10, nisaidieni kushika nyeti yabaki hivyo hivyo jamani!
Wapenda sifa wameongeza goli, mechi imeisha 2-4 mkeka umechanika na nimekosa 15,000/= kwa 700/= niliyoweka
 
Wewe acha ila Mimi kubeti ndio siachi kamwe
Screenshot_20201006-204152.jpg
 
Waungwana, poleni na majukumu yenu, enzi hizo nilikuwa mlevi wa pombe lakini kimaajabu tu nikaweza kuacha, nikahamia kwenye sigara, huko nako nikapambana nikaweza kuacha kabisa!

Sasa si ndio nikaanza kubet! Waungwana nmekuwa mlevi mbwa wa kubet! Yaani nabet kila siku, makampuni karibu yote nimejisajili! Mbaya zaidi napigwa kila siku hasa nikiweka dau kubwa, nkiweka dogo angalau napata ya kubrashia viatu!

Waungwana nifanyeje niachane na huyu sheitwani? Maana kama jana Liverpool na Man U wamenichakaza haswaaa!!! Msaada majamaa!!
Tatizo hujui kubashiri tafuta watalaam kama cc ucopy mikeka utafurahia betting ngoja nikutumie baadhi ya mikeka ya wk moja iliyopita
 

Attachments

  • Screenshot_20201006-171732.png
    Screenshot_20201006-171732.png
    49.5 KB · Views: 15
  • Screenshot_20201004-174020.png
    Screenshot_20201004-174020.png
    53.9 KB · Views: 14
  • Screenshot_20201006-171901.png
    Screenshot_20201006-171901.png
    64.3 KB · Views: 16
  • Screenshot_20201006-171732.png
    Screenshot_20201006-171732.png
    49.5 KB · Views: 14
  • Screenshot_20201005-185304.png
    Screenshot_20201005-185304.png
    51 KB · Views: 13
  • Screenshot_20201004-174237.png
    Screenshot_20201004-174237.png
    35.1 KB · Views: 13
  • Screenshot_20201004-174056.png
    Screenshot_20201004-174056.png
    51.5 KB · Views: 13
  • Screenshot_20201004-174020.png
    Screenshot_20201004-174020.png
    53.9 KB · Views: 15
  • Screenshot_20201004-173920.png
    Screenshot_20201004-173920.png
    56 KB · Views: 11
  • Screenshot_20201004-174237.png
    Screenshot_20201004-174237.png
    35.1 KB · Views: 12
  • Screenshot_20201004-173840.png
    Screenshot_20201004-173840.png
    45.6 KB · Views: 13
  • Screenshot_20201004-102714.png
    Screenshot_20201004-102714.png
    53.2 KB · Views: 13
  • Screenshot_20201004-173216.png
    Screenshot_20201004-173216.png
    58 KB · Views: 10
Mpaka sasa niko njia panda!!ila jana na leo nmejikeep busy kidogo sijabet kabisaaa!!nmejaribu kuacha smartphone nyumbani nikatoka na kitochi!
 
Na mwenyewe anabahatisha tu on long run ni loss Mimi nimefanya na paid service wanajiita betensured wana kitu wanaaita sure 2 na sure 3 yaani wanakupa odd 2 na odd 3 za uhakika lakini nimeishiwa kunyolewa mpaka basi kuna Siku nimetia laki laki kwenye hiyo odd 2 na 3 na zote mbili nikapunwa. Sio kwamba haupati lakini rate ya kupunwa in kubwa tofauti na wanavyotangaza.
Hao wanaojiita wa uhakika ni wachawi tu. Mara nyingi odds wanatoa za uongo halafu baada ya matokeo wanafanya kuedit kuwa walipost sawa. Nimekumbana nao sana kwenye safari za ujinga wa kutaka kuwa bilionea. Ukiangalia site nyingi za hao wahuni, huwa hawaruhusu comments.
 
Nakuapia hujaacha wew...hakuna aliewai acha
Japo inahitaji kujitoa kwelikweli. Ile ni kama pomne au sigara na pengine kama cocain. Kuna muda ukisikia tangazo unasikia roho inakwambia jaribu.

Kilichonisaidia kuvumilia, niliamua kuhamisha mawazo yangu kutoka kwao, na line zangu za mpesaa niliblock PIN za miamala hivo pesa haiwezi kutoka na hauwezi kubet kwa namba ya mtu maana pesa ikiingia anaweza kukugeuka. Hii mbinu imenisaidia sana.

Note: Nilihakikisha kwanamna yoyote ile siwezi kureset password (kitambulisho nilichotumia sikumbuki namba zake na sinacho kwasasa) msiniulize nimewezaje kuishi hivo, nataka kuwa mbali na betting. Inahitaji kujitoa kwelikweli na kuhakikisha unatumia mbinu zote za kimedani ili kuishinda tamaa.
 
Back
Top Bottom