Nifanyaje niachane na ubashiri?

Nifanyaje niachane na ubashiri?

mgonga

Senior Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
174
Reaction score
563
Waungwana, poleni na majukumu yenu, enzi hizo nilikuwa mlevi wa pombe lakini kimaajabu tu nikaweza kuacha, nikahamia kwenye sigara, huko nako nikapambana nikaweza kuacha kabisa!

Sasa si ndio nikaanza kubet! Waungwana nmekuwa mlevi mbwa wa kubet! Yaani nabet kila siku, makampuni karibu yote nimejisajili! Mbaya zaidi napigwa kila siku hasa nikiweka dau kubwa, nkiweka dogo angalau napata ya kubrashia viatu!

Waungwana nifanyeje niachane na huyu sheitwani? Maana kama jana Liverpool na Man U wamenichakaza haswaaa!!! Msaada majamaa!!
 
Pole sana mkuu, ni aina ya Uraibu lakini kama umeweza kupambana na pombe na sigara, hilo haliwezi kukushinda.. Jiepushe na mambo ambayo ni kishawishi kwako kubet.
 
Pole sana mkuu, ni aina ya Uraibu lakini kama umeweza kupambana na pombe na sigara, hilo haliwezi kukushinda.. Jiepushe na mambo ambayo ni kishawishi kwako kubet..
Asante mkuu!
 
Ndugu yangu pole kwa hili janga linalomaliza wengi kimyakimya, hakika hii kubet imemaliza wengi nikiwa mmoja wao, jana mimi niliapa kuwa sitawahi kubet tena maishani mwangu hata kama Barcelona anacheza na Singida united.

Na nimeamua kuacha kufuatilia mambo ya mpira kabisa, nimejitoa kwenye magroup ya betting na ya soka yote, nimefuta apps zote za mpira nikiamini kuwa nisipokuwa na hizo vishawishi nitaweza kuacha kabisa.

Jaribu kufanya kama mimi unaweza kufanikiwa kuacha kabisa, tafuta kitu mbadala itakayokuweka busy saa ambazo hauko kazini ili mawazo yasikupeleke huko tena.

Kama wewe ni mpenzi wa vitabu jaribu kusoma time ukiwa free ili akili yako isirudie tena huko.
 
Labda nikioa ndo ntakuwa busy mkuu[emoji23]!nmejaribu kuuza smartphone yangu ili angalau nikiikosa ntaacha,lakini wapii!nkainunua nyingine chap!tatizo jioni nikirudi najikuta sina cha kufanya na sio mpenzi wa movie,ila mpira ndo uko damuni!sina group lolote la beting!ila kuacha ndo mtiti!
Ndugu yangu pole kwa hili janga linalomaliza wengi kimyakimya, hakika hii kubet imemaliza wengi nikiwa mmoja wao, jana mimi niliapa kuwa sitawahi kubet tena maishani mwangu hata kama Barcelona anacheza na Singida united. na nimeamua kuacha kufuatilia mambo ya mpira kabisa, nimejitoa kwenye magroup ya betting na ya soka yote, nimefuta apps zote za mpira nikiamini kuwa nisipokuwa na hizo vishawishi nitaweza kuacha kabisa. jaribu kufanya kama mimi unaweza kufanikiwa kuacha kabisa, tafuta kitu mbadala itakayokuweka busy saa ambazo hauko kazini ili mawazo yasikupeleke huko tena. kama wewe ni mpenzi wa vitabu jaribu kusoma time ukiwa free ili akili yako isirudie tena huko.
 
Back
Top Bottom