Nifanyaje ili nimuache lakini asiumie?

Nifanyaje ili nimuache lakini asiumie?

Anthony Threedeyea

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2013
Posts
471
Reaction score
47
Habari zenu wakuu,

Napenda kujitokeza mbele yenu kuomba ushauri kwa ili suala nalollpitia kwa sasa japokuwa inaweza kuonekana jambo la kawaida kwa wadau wengine hapa ndani.

Kwa ufupi nimetokea kupendana na binti mmoja msukuma mwenyeji wa wilaya ya Sengerema kiukweli ni binti mpole, mkarimu na mwenye kujali na amenionyesha mapenzi ya kweli sikatai hasa hasa kipindi nilikua vibaya kiuchumi.

Alinipa msaada mkubwa sana, kama mwanaume nimekua nikimwaidi mambo mbalimbali nikijua leo ni tofauti na kesho katika kutoa ahadi zangu yaliyofanikiwa ni machache sana na amekua hapendezwi na hii hali imefikia kipindi ule ukarimu wake umeanza kupotea kutokana na kuniita majina mbalimbali kama vile msanii, mwanasiasa, maneno mengi.

Kiukweli hali hii ya kutoa ahadi zisizo na vitendo zimenifanya nipoteze hamu ya mapenzi kwake pia najihisi kama mkosefu
maisha yamebadilika kwa upande wangu naitajikujiendeleza kimasomo na mdogo wangu pia aneanza a-level mwezi unaokuja pia familia ya nyumbani inanitegemea.

Hivyo basi nimepiga tathimini kuja kupata mafanikio yanayoeleweka itanichukua miaka kama mitano na kwa ulimwengu wa sasa sidhani kama atakua upande wangu dhamira yangu hapa ni kuomba ushauri wa kumfanya tutengane kwa amani bila yeye kuumia na itakua vizuri kama yeye ndo itakua chanzo ili afaidi ulimwengu kwa sasa mimi sina maisha.

Asanteni
 
Mwambie humtaki akukome!!!
then tupia hapa kapicha na namba yake ya simu..!
 
Vunja ukimya...

Sema nae

Na hivi kwa nini utoe ahadi ambazo huwezi kutekeleza???
 
Hv,wakati wa matatizo kama hayo si ndo wakati mzuri wa kujua yupi mke mwema na yupi hovyo?si ndo wakati wa kujua kama ni mvumilivu au la!Mwambie ukweli ili ajue kwa kuwa heri ukweli mchungu kuliko uongo mtamu!
 
We uanza kwa kumsifia kama ulivyomsifia humu, mwambie ukweli na uanze kumwita majina kama hayo anayokwita wewe, uwe na msimamo, hata akikubembeleza vipi we mwambie hauna jinsi huo ndio ukweli na inabidi mkubaliane nao,,muahidi mtaendelea kuwa marafiki.. punguza mawasiliano naye ibaki salamu tu.
 
Unaposema kuwa kwa sasa huna maisha....unamaanisha kuwa kwa sasa huna UHAI na umeandika haya ukiwa kaburini au ahera...???
 
Ikiwa hawa ndio wanaume waliobakia karne hii....kweli kina dada ni haki yao kutokuona umuhimu wa kuolewa......
 
Umeharibu mwenyewe kwa kutoa ahadi usizoweza kutekeleza. Mi nakushauri kitu kimoja, kaa nae chini na uongee nae kwamba ulikua na nia na unatamani kutekeleza ahadi zako ila tatizo ni hali ya kiuchumi. Akikuelewa huyo ni mke mwema na asipokuelewa ndo ushaharibu tena. Na akikuelewa, uache kutoa ahadi usizoweza aisee... wengine hawapendi kabisa kupewa ahadi za uongo maana ni sawa na kucheza na akili za mtu na kumfanya poyoyoooo....
 
Hv,wakati wa matatizo kama hayo si ndo wakati mzuri wa kujua yupi mke mwema na yupi hovyo?si ndo wakati wa kujua kama ni mvumilivu au la!Mwambie ukweli ili ajue kwa kuwa heri ukweli mchungu kuliko uongo mtamu!

bora waachane maana mwnaume akienda masomoni atakuja na kichwa kipya na utaona dada wa watu anakuja kuomba ushauri kupotezewa mda soooo!!???
 
Naona nyie hamuwezi lile agano la shida na raha. Mweleze ukweli yeye achague mwenyewe kama kweli unampenda.
 
Mtafutie Bwana mwingine umkabidhi kisha ushike njia yako...
 
Kuachwa kuachwa tu , maumivu yapo pale pale.
Cha muhimu acha kutoa ahadi feki feki, omba msamaha kwa kushindwa kutimiza ahadi zako za zamani na mwisho mwelezee malengo yako na majukumu uliyonayo. Kwa hakika muda ukifika atasepa zake mwenyewe akuache utimize ndoto zako.
 
Back
Top Bottom