Niende au nisiende?

Niende au nisiende?

tang'ana

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2015
Posts
12,054
Reaction score
16,509
Nimeitwa kwenye usaili kwenye chuo kikuu kimoja maarufu jijini dar kilichoko karibu na mlimani city ,idadi ya watu tulioitwa kwenye hyo nafasi ni 33 ila sijajua wanataka watu wangapi.

Sasa nauliza niende au nisiende maana niko arusha kwa sasa na usaili ni tarehe 13 mwezi huu ila hofu yangu ni kuwa naweza nikapoteza muda na gharama zangu kumbe wao huko wana watu wao waliowaandaa.

Tupeane mawazo wakuu.
 
Bora kupoteza muda kwa hicho kuliko kulala kwenu......!!!
 
Naamini kwa yeyote atakayejibu atasema "nenda"
 
hata mm nakuwaga na mawazo ya kukata tamaa kama yakwako na mwisho wa siku napoteza.
 
Bora kupoteza muda kwa hicho kuliko kulala kwenu......!!!

sio kwamba nimelala tu nyumbani,kuna sehemu nipo napiga kazi,ila nilitaka kuangalia challenges nyingne hasa huko serikalini.
 
Nenda tuu ukajaribu inaweza kuwa bahati yako mkuu
 
sio kwamba nimelala tu nyumbani,kuna sehemu nipo napiga kazi,ila nilitaka kuangalia challenges nyingne hasa huko serikalini.

Watu 33 sio nyomi hata ni kujiamini na uwezo Kwisha.....kila la kheri!!
 
Kama ni ud jiandae na mshahara mdogo,nashangaa kwanini hiki chuo wanalipa mishahara midogo ukilinganisha na vyuo vingine
 
mkuu usiende ulitubaki wachache kwenye kinyang'anyiro
 
Kama ni ud jiandae na mshahara mdogo,nashangaa kwanini hiki chuo wanalipa mishahara midogo ukilinganisha na vyuo vingine

kwa kazi za kada ipi kiongozi...ukilinganisha na chuo gani kwa mfano
 
kwa kazi za kada ipi kiongozi...ukilinganisha na chuo gani kwa mfano

Kwa mfano mzumbe,muhimbili,open university scale zao zipo juu ila ud ,udom walewale ila wote wanatumia scale moja ya pgss kwa watu wa arts puts kwa walimu nk..
 
Kwa mfano mzumbe,muhimbili,open university scale zao zipo juu ila ud ,udom walewale ila wote wanatumia scale moja ya pgss

sawa kaka lkn hujanitajia kazi zipi kwa mfano....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom