Nielemisheni jambo wanasiasa!

Nielemisheni jambo wanasiasa!

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Posts
2,647
Reaction score
4,753
Hivi vyama vingine ukiachana na CCM, CHADEMA, ACT Wazalendo...yaani hivi vyama huwa vinaonekana vipo kwenye karatasi ya kura tu...na hata sidhani hata kampeni kama vinapigaga...sidhani kama vina ofisi zake...sidhani kama ina mikutano yao miguu...

Lakini naona kama msajili anavitambua kuwa vinafuata sheria zote za chama cha siasa...

Lakini kama naviona ni vyama mfu...lakini vipogo toka 2005 nilivyopata akili za masuala ya uchaguzi...sijui tadea mara sauti ya umma...

Mbona msajili kakomaa na chadema tu matisho kibao ya kukifutia usajili...?

Mimi sio mpenzi wa siasa ila nauliza tu...

Ila mimi ni katika wananchi wanaopenda kuhisi ladha ya ushindi inayotokana na ushindani halisi...ushindi huu una ladha tamu sana...kuliko kusherehekea ushindi ambao umesababishwa na mwenzio kufungwa mikono na miguu asishindane na wewe...

Unatumia pesa nyingi na gharama kubwa kupiga kampeni na kutengeneza sifa kwa ajili yako...hali ya kuwa wapinzani umewafungia...na unaenda kwenye uchaguzi au mechi ambapo tayari wewe ulishashinda kwa namna yoyote ile...alafu yakitangazwa matokeo unashangilia nini sasa...kwamba umeshinda..?

Haya mambo ndio yanayonikera kwa simba na yanga...hata ukishinda huna raha...ndio ushindi gani sasa...?

Unafurahia matokeo ya mtoto ambaye ulimpa majibu ya mtihani wote...? Eti mwanangu amepata 100 ya 100...hongera mwanangu...una akili kweli...?
 
Back
Top Bottom