RALPH TRESVANT, Mleta mada!
Mtalii rasmi aliekuja kutalii tu na kurudi kwao pindi amalizapo utalii wala hahitaji usajili wa line hapa nchini wacha uongo.
Huyu atatumia simu yake direct kwa kuwa anayo line yake rasmi iliyosajiliwa huko atokako.na hapa itafanya international roaming tu.
Lakini pia kwa sasa kuna option ya pili kwa watalii wote kupitia Wi-Fi routers.
Hizi kwa sasa zipo zimezagaa kwa kila hotel na camps za kufikia wageni. Tena wengi wameweka bila password ili kila mgeni aweze kutumia bila usumbufu.
Na kampuni za kusafirisha wageni baadhi zinazo hizo Wi-Fi routers ndani ya magari yao full time.
Pia hata sehemu au milango(entry gates)za hifadhi nchini kuna hizi Wi-Fi for free. So acheni uongo usio na maana.
Kama una lengo la kuyasema mapungufu katika zoezi la NIDA liseme kivingine ila sio kwa mgongo wa utalii au watalii.
Kama una jambo na serikali pia uko free kuitema sumu yako humu maana ndio kwa wajaa sumu. Sio lazima kuchafua sekta zisizo na mahitaji ya siasa uchwara.
Mlisema serikali itakimbiza watalii kisa kufunga
bureau de changes.
Lakini mpaka sasa tunaona serikali ikinufaika na mfumo wa bureau ndani ya benki zetu na watalii wako juu kama kawaida.
Sent using
Jamii Forums mobile app