NIDA vs Immigration vs Makampuni ya Simu: Watalii nao kikaangoni

Dec 17, 2019
17
5
Watalii wallopo ndani ya nchi ambao walichukua line za simu nao hali mbaya.

Mfumo wa Immigration hausomeki kule NIDA na makampuni ya simu nao wanasema hawaoni kitu. Sisi ambao tuko kwenye sekta ya utalii tunashindwa kuelewa tatizo liko wapi.

Watalii walipo ndani ya nchi wakienda kusajili line wanaambiwa alama za vidole vyao hazionekani kwa sababu Immigratiion hawajapeleka taarifa zao NIDA hivyo kampuni za simu hazitambui.

Hapa mtaliii anaacha kwenda kutazama wanyama tuko busy kuumiza vichwa na NIDA.

Hivi hiii software ina matatizo gani? Kampuni gani ilipewa tenda? Nani ananufaika na huuu mtafaruku?
 
Tukisema CCM inatulaza kwa huzuni kwa kuendekeza uchawi na kuendesha nchi kutokana na maagizo ya waganga badala ya wataalam muwe mnatuelewa.

ISAYA 50:11 Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
 
RALPH TRESVANT, Mleta mada!

Mtalii rasmi aliekuja kutalii tu na kurudi kwao pindi amalizapo utalii wala hahitaji usajili wa line hapa nchini wacha uongo.

Huyu atatumia simu yake direct kwa kuwa anayo line yake rasmi iliyosajiliwa huko atokako.na hapa itafanya international roaming tu.

Lakini pia kwa sasa kuna option ya pili kwa watalii wote kupitia Wi-Fi routers.

Hizi kwa sasa zipo zimezagaa kwa kila hotel na camps za kufikia wageni. Tena wengi wameweka bila password ili kila mgeni aweze kutumia bila usumbufu.

Na kampuni za kusafirisha wageni baadhi zinazo hizo Wi-Fi routers ndani ya magari yao full time.

Pia hata sehemu au milango(entry gates)za hifadhi nchini kuna hizi Wi-Fi for free. So acheni uongo usio na maana.

Kama una lengo la kuyasema mapungufu katika zoezi la NIDA liseme kivingine ila sio kwa mgongo wa utalii au watalii.

Kama una jambo na serikali pia uko free kuitema sumu yako humu maana ndio kwa wajaa sumu. Sio lazima kuchafua sekta zisizo na mahitaji ya siasa uchwara.

Mlisema serikali itakimbiza watalii kisa kufunga bureau de changes.

Lakini mpaka sasa tunaona serikali ikinufaika na mfumo wa bureau ndani ya benki zetu na watalii wako juu kama kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama una mfanyakazi wa kigeni yaani (Expatriate) katika kampuni husika na yeye siyo raia. Je, atafuata utaratibu gani ili aweze kusajili namba zake za simu?
 
Hili zoezi linapelekwa haraka haraka kwa sababu ya uchaguzi wa october 2020 na nina wasiwasi kama database za NIDA hazina loopholes kwa aina ya watu walioko humo. Naona hili limechangiwa na kuongozwa na mshamba wa teknolojia
 
Watalii wallopo ndani ya nchi ambao walichukua line za simu nao hali mbaya.

Mfumo wa Immigration hausomeki kule NIDA na makampuni ya simu nao wanasema hawaoni kitu. Sisi ambao tuko kwenye sekta ya utalii tunashindwa kuelewa tatizo liko wapi.

Watalii walipo ndani ya nchi wakienda kusajili line wanaambiwa alama za vidole vyao hazionekani kwa sababu Immigratiion hawajapeleka taarifa zao NIDA hivyo kampuni za simu hazitambui.

Hapa mtaliii anaacha kwenda kutazama wanyama tuko busy kuumiza vichwa na NIDA.

Hivi hiii software ina matatizo gani? Kampuni gani ilipewa tenda? Nani ananufaika na huuu mtafaruku?
Hivi kabla ya simu za mkononi, watalii walitembezwa vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom