NIDA Mnakwama Wapi?

NIDA Mnakwama Wapi?

Nilikuwa nazungumzia kitambulisho Cha kura maana nilipoteza. Nida pia wananizingua hadi leo bila bila
Kitambulisho kura hakina longolongo kupata.Kama umepoteza unaenda ofisi ya mtendaji akupe barua ukaripoti polisi.Ukishapata police loss report unaenda kwa jamaa wa tume ya uchaguzi,ambao wanapita kila mkoa ,kufanya marekebisho ya daftari la wapiga kura.Wanakupa kitambulisho kingine!
 
Nenda ofisi za nida utapewa namba ya kitambulisho
Hiyo namba INA nguvu sawa na kitambulisho chenyewe?Naweza pata passport mpya emigration kwa kutumia hiyo namba pekee?
 
Kitambulisho cha kupigia kura hakina faida kwako kinafaida kwao uwachague wapate uraisi,ubunge na uwaziri ndio maana ukikitaka hausumbuliwi

Na hichi cha NIDA wao hawana faida nacho ila wewe ndio unafaida nacho maana usipokuwa nacho mambo yako mengi yana kwama kwa hiyo hata ukichelewa kukipata wao hawajali

Lakini siku itakapo amuliwa kuwa wenye NIDA I'd ndio watakao piga kula utaona siku hiyo hiyo ukienda utakipata ili mambo yao yasikwame
 
Ndo nipo hapa kwa foleni nimeshafanya hizo process
 
Hiyo namba INA nguvu sawa na kitambulisho chenyewe?Naweza pata passport mpya emigration kwa kutumia hiyo namba pekee?
Mmh sina uhakika, namba itakusaidia kusajili line. Ila ukiwaeleza kuwa unahitaji kwaajili ya passport wanaweza kukupa
 
Nida hawana makosa sana kama sisi tunavyofikiria,mwenye makosa ni yule aliyepitisha sheria kushinikiza kuwa na kitambulisho kupata huduma muhimu kama passport,kusajili kampuni nk.
 
SIO VITA
Nenda ofisi za nida utapewa namba ya kitambulisho
Sio vitambulisho hatacusajili wa simu unakwamwishwa na NIDA. Nilenda mlimani city kwa nia ya kusajili namba za simu nikakuta mawasiliano na NIDA hayapo. Niliulizia voda na tigo tatizo ni hilo. Sijapata tena nafasi ya kusafiri kwenda huko labda waweke mawakala karibu na ninakoishi na mawasiliano na NIDA yawe mazuri. Vinginevyo nitasubiri mpaka watoa huduma za simu wakose pesa kwa kufunga simu na serikali nayo ikose AKILI ZITAFUNGUKA.
 
Mmh sina uhakika, namba itakusaidia kusajili line. Ila ukiwaeleza kuwa unahitaji kwaajili ya passport wanaweza kukupa
Line sina shida nayo km passport.Ninayo line ya MTN ninayotumia kwenye Whatsapp kutumia WiFi. Vitambulisho vyenyewe wakishakusajili wanakudua tena rejea kisa cha Nape na Kinana. Kusajili line iko pending!
 
Nida hawana makosa sana kama sisi tunavyofikiria,mwenye makosa ni yule aliyepitisha sheria kushinikiza kuwa na kitambulisho kupata huduma muhimu kama passport,kusajili kampuni nk.
Aliyepitisha Sheria ya Kitambulisho Vya NIDA ndio huyohuyo aliyepitisha sheria ya kitambulisho Vya mpiga kura.Sasa NIDA wao wanakwama wapi mbona wenzao wako vizuri?
 
Kuna kama kaukweli hiviii
Kitambulisho cha kupigia kura hakina faida kwako kinafaida kwao uwachague wapate uraisi,ubunge na uwaziri ndio maana ukikitaka hausumbuliwi

Na hichi cha NIDA wao hawana faida nacho ila wewe ndio unafaida nacho maana usipokuwa nacho mambo yako mengi yana kwama kwa hiyo hata ukichelewa kukipata wao hawajali

Lakini siku itakapo amuliwa kuwa wenye NIDA I'd ndio watakao piga kula utaona siku hiyo hiyo ukienda utakipata ili mambo yao yasikwame
 
Unahisi malalamiko yako ntayafanyia kazi kuja kunisemea hapa?
 
Hiyo namba INA nguvu sawa na kitambulisho chenyewe?Naweza pata passport mpya emigration kwa kutumia hiyo namba pekee?
Jibu ni Ndiyo hiyo number ukiipata unaweza kufanyia kila kitu pamoja na hiyo ya kuomba hati ya kusafiria. Na siyo lazima uende Nida kupata number yako. Unaweza kupiga *152*00# kisha utachagu 3 na baadae 2. Hakikisha unaingiza majina yako matatu km ulivyoandikisha. Utaweka number ya simu uliyoandikisha kisha tuma hizo taarifa na utatumiwa number yako ndani ya sekunde 10. Huduma hiyo utalipia Tsh.100. Unaweka Salio la kawaida kwenye simu yako. Huduma hii ni kwa mitandao yote ingawa halotel huwa inasumbua. Km utapata number hiyo unaweza pia kupakua nakala ya kitambulisho chako kwenye tovuti ya Nida ambayo ni www.nida.co.tz
 
Nadhani NIDA hawana tatizo. Tatizo ni hela na vifaa. Kama hujapewa fedha na vifaa utafanyaje kazi?. Tusiwalaumu NIDA.
 
Wapiga kura wanahitajika wengi kuwapigia kura CCM kuliko kitambulisho cha taifa tofauti ni hiyo
 
Back
Top Bottom