Nico Zengekala... Mwanamuziki kipofu aliyetikisa Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nico Zengekala... Mwanamuziki kipofu aliyetikisa Tanzania.

Discussion in 'Entertainment' started by Bujibuji, Aug 26, 2011.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,451
  Likes Received: 22,404
  Trophy Points: 280
  ILIPOSIKIKA sauti yake kila mpenzi wa muziki
  anayefuatilia bendi za hapa nyumbani alihisi
  kuna kitu kipya kimeingia katika tasnia ya
  muziki wa dansi.
  Hiyo ilikuwa mwaka 1982 alipoingia kwa
  mara ya kwanza nchini mwimbaji hatari
  kutoka mkoa wa Pwani nchini Kenya Nico
  Zengekala akiwa ni mwimbaji tumaini wa
  bendi ya Les Quban.
  Bendi hiyo ilianzishwa nchini Kenya lakini
  ilikuwa na wanamuziki kutoka Tanzania
  ambapo awali ilikuwa pamoja na mwimbaji
  maarufu Juma Kilaza aliyetamba sana
  mkoani Morogoro kabla ya kufanyika
  mapinduzi ya uongozi yaliyomnyang'anya
  Kilaza uongozi na pia kumtimua
  kwenye bendi na jahazi hilo kushikwa na
  mpuliza saxophone marehemu Comson
  Mkomwa.
  Walipoingia katika kumbi za burudani za
  jijini Dar bendi hiyo ikiwa pia na mpiga gitaa
  la solo Mohamed Tungwa, wapuliza ala za
  upepo kama Said Makelele, Jumanne
  Mwamzungu, akina Majuto Mbungani na
  Shaibu Monduli bendi hiyo iliweza kuingiza
  ushindani kwa bendi kongwe
  kama Juwata wakati huo, Mlimani Park na
  hata bendi zilizokuwa na asili ya
  wanamuziki kutoka nchini Zaire (sasa
  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) kama
  vile Orchestra Safari Sound, Marquiz du Zaire
  na Matimila.
  Nyimbo zilizozipeleka puta bendi nyingine
  pamoja na mashabiki kwa ujumla ni pamoja
  na Shemango, Kambarage Nyerere, Jack na
  nyingine kadhaa.
  Uimbaji wa Zengekala ulianza kupata sifa
  ndani na nje ya bendi hiyo na watabiri wa
  masuala ya muziki wakati huo walithubutu
  hata kueleza wazi kwamba mwanamuziki
  huyo kamwe asingedumu katika bendi hiyo.
  Hatimaye, mawazo hayo yakawa kweli
  kwani Zengekala mwenyewe alimueleza
  mwimbaji mwenzake wa karibu wakati huo,
  Shaibu Monduli kwamba yeye alitamani sana
  kuiimbia bendi ya Juwata Jazz inayotumia
  mtindo wa Msondo Ngoma.
  Akamsisitizia kwamba dhamira hiyo alikuwa
  nayo tangu alipokuwa nchini kwao Kenya
  ambako alizisikia nyimbo za bendi hiyo na
  pia akatamani siku moja kuimba na akina
  Hassan Bitchuka, Shaaban Dede, Joseph
  Lusungu na waimbaji wengine wakongwe.
  Hivyo alitaka hatua yake ya kufika nchini
  Tanzania iende na dhamira yake ya kujiunga
  na bendi hiyo endapo atakubaliwa.
  Vurumai kubwa ilijitokeza miongoni mwa
  viongozi wa bendi ya Les Quban waliokuwa
  wakitumia mtindo wa Vinavina na wale wa
  Juwata baada ya kujua nyota ile ya jaha
  inaangazia kwenye bendi yao.
  Hatimaye Zengekala akatua Msondo na
  kuweka mapenzi makubwa ya urafiki na
  mwimbaji mwingine chipukizi aliyemkuta
  Msondo marehemu Tino Masinge.
  Alipojiunga tayari bendi
  hiyo ilishawakamata waimbaji mbalimbali
  akiwemo TX Moshi William kutoka bendi ya
  Polisi Jazz.
  Wimbo wake wa kwanza na bendi ya
  Juwata ulikuwa ni Solemba ambao alipenda
  apigiwe solo na gwiji la chombo hicho Dk
  Saidi Mabela na yeye akashirikiana kuimba
  akiwa na Suleyman Mbwembwe na Tx Moshi
  William.
  Enzi hizo tayari Hassan Bitchuka alishaihama
  Msondo na kujiunga na Mlimani Park lakini
  ikatokea siku moja bendi hiyo kufanya shoo
  katika ukumbi mmoja pale DDC Magomeni
  Kondoa.
  Kwa kuwa siku hiyo Bitchuka naye
  alikuwemo ukumbini na Msondo ndiyo
  iliyopata nafasi ya kufungua pazia la
  burudani ile basi umati wa watu uliojaa
  ulidhani Bicthuka ameamua kwenda kuipiga
  tafu Sikinde kumbe ilikuwa ni sauti ya Nico
  Zengekala aliyekuwa akiimba wimbo uitwao
  Sogea karibu.
   
 2. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 532
  Likes Received: 340
  Trophy Points: 80
  mzee wa SOLEMBA..
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,451
  Likes Received: 22,404
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Sauti yake bado inanisisimka masikioni mwangu.
   
 4. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  [Mwanzo] Rudi Table
  Solemba - JUWATA JAZZ(Nico Zengekala)]
  Ulinipa ahadi tukutane kwenu,
  Nikitumaini nimewahi,
  Nilichopata kwako ni matusi ooh, ooh na
  dharau tele
  Ungenieleza ukweli solemba,
  Kuliko kunidanganya ooh,
  Najuta kuitimiza ahadi ooh ambayo si ya
  kweli.
  (Chorus)
  [Wote]
  Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
  ila dharau uliweka mbele solemba.
  [Zengekala]
  Nilichomwa na jua toka asubuhi,
  mpaka saa nane Solemba sababu ya
  kukungoja wewe
  Kumbe ulikua ndani ukichungulia dirishani
  Nimeshituka Solemba ,
  Nimeshituka Solemba
  [Wote]
  Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
  ila dharau uliweka mbele solemba.
  [Zengekala]
  Sikutaki tenaaa, sina haja nawe,nimeshapata
  mwingine atakaye nipenda kwa roho moja,
  Tafuta bwana mwingine utakae mbabaisha
  kama mimi
  Huna huruma Solemba.......Aloi I love you
  baby
  [Wote]
  Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
  ila dharau uliweka mbele solemba.
  Rudi mwanzo
  [TUMA - Nico Zengekala]
  Nilisimama kwenye kona, ya uhuru na
  msimbazi,
  Natizama wanaopita , wanaorudi mamaaaa,
  Huenda nikaiona sura yake tuma.
  Nasimama nikiwaza, ahadi yetu tuliopanga,
  Tukutane Darisalama, Tuma mama,
  Nia na madhumuni wazazi watuone.
  Nilishikwa na mnutsuko shoga yake
  aliniponiejia na kunieleza
  Tuma ee tuma ee keshaolewa
  Nilishikwa na mshituko mapigo ya moyo
  enda mbio
  Sikutegemea Tuma, kama angevunja ahadi
  yetu ama kweli penye uzia hupenyeza rupia
  CHORUS:
  Usinione nimekonda ewe Tuma, hakuna
  lingine mama
  Ila ni wewe Tuma.
  (Usiku wote nalala nikikuwaza nakuita jina
  lako oh oh Tuma)
  Repeat: Usinione nimekonda ewe Tuma.
  Rudi mwanzo
   
 5. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,037
  Likes Received: 750
  Trophy Points: 280
  Alikuwa tishio,sauti nzuri sana.
   
 6. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  mkuu hapo umenigusa ni historia nzuri, huyu jamaa alikuwa mkali sana. Nasikia kuna siku alituzwa akaficha pesa yake kwenye chumba alichokuwa akilala mwenzie akaiba yeye akaitafuta na kuipata alikoificha room mate wake na kuificha tena cha ajabu mwenye macho (uono)alifika na kuitafuta bila mafanikio Nico akawa anamcheka tu jinsi alivyokuwa akihaha though alikuwa hamuoni...Nasikia pia alikufa kwa kuwekewa sumu sijui ukweli wa madai haya...mwenye info zaidi plz...
   
 7. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45


  Hizo habari ni kweli; kuna li mwanamuziki moja la siku nyiingi (kongwe) ndio lililomuua huyu kijana. Kisa alikuwa anamfunika.............ngoja ataona jinsi kifo chake kitakavyokuwa cha mateso kwa dhambi ya kumuua kijana mbichi mwenye sauti ya kipekee.

  Wimbo wa Jack wa Mapendo, Mama Hisani............ the guy was kipajid
   
 8. ngalikikinakiki

  ngalikikinakiki Member

  #8
  Aug 30, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hakuuwawa kwa sumu alikufa kutokana natatizo la kifafa alilokuwa nalo na hivyo kujikaba kwa ulimi wake mwenyewe
   
Loading...