Nichukue uamuzi gani?

Nichukue uamuzi gani?

Dooh mkuu pole sana, inasikitisha sana.. Sijui hata nikupe uahauri gani lakini punguza jazba kidogo, usije kuchukua maamuza ambayo yatakugharimu baadae

Kama unampenda huyo binti basi mvumilie maana muda unavyoenda atapona hayo majeraha "time heals"

Kuhusu hao wazazi wake, wasamehe tu maisha yaendelee.
 
Asante mkuu kwa ushauri wako
 
umeshajaribu kumpeleka kwenye counseling? anahitaji sana sana kupewa counseling tukio la kubakwa huwa lina affect maisha ya mtu for the rest of her life, na hata kwenye tendo itakuwa shida kwenu hata kama utamvulimia mpaka ndoa lakini mwisho wa siku psychologically huyo mtu hayuko sawa mnaweza kuishia kuwa na ndoa isiyo na amani. Na kwa wewe wasamehe tu hao wazazi na huyo alietenda hicho kitu wala usitake kumjua mana unaweza jikuta umefanya jambo ambalo litagharim maisha yako. Ila she really really needs help
 
Habari za muda wakuu!? Nimekuwa member hapa kwa muda lakini kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wangu. Nimefungua ID mpya ili kuleta mada hii.

Leo nimeona niombe ushauri kwenu maana najua kuna watu waelewa, watu wazima wanaojua maisha yalivyo na waliopitia mengi. Nianze

Mimi ni kijana nina miaka 25 na nina mpenzi (miaka 24) na nipo nae sasa miaka miwili na nusu sasa. Tunapenda na kusaidiana kwenye shida na raha.

Huyu mpenzi wangu aliwahi kukumbwa na tatizo la kubakwa akiwa na miaka 12 (sad) wakati tuna date nae kuna siku alichukua muda kunieleza tukio lilivyokuwa na nini kilifuata baada ya hapo. Unfortunately hakuwahi kupata justice (kitu ambacho kinaniumaga sana). Yani aliefanya kile kitendo ni mdogo wa baba yake wa kambo na hakuchukuliwa hatua yoyote hata kufikishwa tu kituo cha polisi na yupo uraiani mpaka leo.

Kinachoniumiza ni mama wa huyu binti, hakuwahi kujali kuhusu ni namna gani lile tukio litaathiri maisha ya mwanae huyu siku zote za maisha yake. Kuna muda huyu mpenzi wangu nikiwa nae (nimekuwa nae mara nyingi ila sijawahi kushiriki nae mapenzi hata mara moja) muda mwingine huwa analia na kumlaumu mama yake (alimwacha na huyu kijana mlevi na kusafiri kwenda msibani wakati walijua tabia yake ya ulevi na mama mkubwa hakuwa anaishi mbali alikua na uwezo wa kumpeleka kwa dada yake mpaka atakaporejea).

Ubaya zaidi ni kuwa huyu binti akiwa still primary alikua analelewa na baba mzazi ambaye alifariki kwa ajali, ndipo huyu binti akahamia kwa mama yake ambae alikua ameolewa na mwanaume mwingine. Tokea amehamia kwa huyo mama haikupita hata miaka miwili ndio likatokea tukio la kubakwa.

Hebu fikiri tukio la kufiwa na mtegemezi wako namba moja hata halijaanza kufutika kichwani linakuja tukio jingine baya maishani mwako. Alafu wale wenye uwezo wa kukusaidia kupata haki yako hawachukui hatua yoyote. Inauma sana, huwa natokwa na machozi mara nyingi nikifikiria kuhusu huyu mtu aliefanya hivyo.

Simfahamu lakini natumaini kuna siku nitamfahamu na nitamsaidia huyu mpenzi wangu kuipata haki yake, hata kama hatutakuwa pamoja tena. Natumaini naweza kujitoa kwaajili yake. Haijalishi kitatokea nini. Mungu ndio atajua.

Nimeishi kwa muda na huyu binti na huwa kweli napata tamaa za kimwili ila nikifikiria tukio alilipitia huwa sitamani hata kumgusia kuhusu hilo swala, hajawahi kuwa katika mahusiano kabla yangu mimi (naweza kuthibitisha hilo). Kufikiria kugusia hilo mara nyingi naweza kusababisha kuibua Post Traumatic Stress ambazo huyu binti amezipata kutokana na tukio hilo.

Hali hiyo imenifanya niwe na chuki na wazazi wake hawa (mama na baba wakufikia) kiasi kwamba najiuliza kama huyu nataka kumfanya awe mke wangu nitawezaje kuwa face hawa watu? Pia imenifanya nimchukie huyo nisie mjua lakini nilieko kwenye harakati za kumjua.

Nia ya kueleza yote hayo ni kuomba ushauri nifanye nini? Nataka kuoa, au hata kabla ya kuoa nipate angalau mtoto naona umri unakwenda kwa kasi, niliwahi kumweleza akaniambia subiri, kila nikimkumbusha hunipa kalenda mpaka sasa aliniahidi angeisha na mimi kuanzia january 2018 lakini siku sio nyingi ameniomba nimwongezee miezi saba.

Je mtu kama yeye tunaweza kuwa na mahusiano yenye furaha? Maana sitaki hata siku moja nimuumize moyo wake. Je kuna siku kweli ataridhia kuwa mke wangu, au ataendelea kunipiga kalenda mpaka nikate tamaa?

Kiujumla sina nia ya kumwacha lakini naomba ushauri kwenu kuhusu hayo niliyoeleza hapo juu.

Najua kuna watu/mtu unaweza kuisoma hii ambaye umeshatokewa na matukio kama haya poleni sana.

Naombeni ushauri nipo njia panda. Ukiona ni sawa kukejeli hamna shida.
anahitaji ushaur tu wa kisaikolojia atakuwa sawa na utamgegeda vizur tu
 
wewe ni shujaa,,,,unaelekea ukomavu halisi....ushauri wangu,,,,maisha ya nyuma ukiyaweka mbele yako huwezi move broo.....futa delete tupa kule.....peleka posa....vuta kinu ndani......anzeni maisha upyaaaaaaa.....zingatia haya....hakikisha na yeye ameridhia,,,, sio kesho kushokutwa anaanza oooohhh nilikwambia nimebakwa hukunisaidia.....vigeu geu kweli hao.....kila la kheri....
 
Nia yangu sio kumgegeda na ingekuwa hiyo labda ningeshamgegeda mara kibao au tungeshaacha. Nia yangu ni kuishi nae siku zote kwa furaha tuwe na watoto wetu, tufurahie maisha. Asante lwa mchango wako.
 
umeshajaribu kumpeleka kwenye counseling? anahitaji sana sana kupewa counseling tukio la kubakwa huwa lina affect maisha ya mtu for the rest of her life, na hata kwenye tendo itakuwa shida kwenu hata kama utamvulimia mpaka ndoa lakini mwisho wa siku psychologically huyo mtu hayuko sawa mnaweza kuishia kuwa na ndoa isiyo na amani. Na kwa wewe wasamehe tu hao wazazi na huyo alietenda hicho kitu wala usitake kumjua mana unaweza jikuta umefanya jambo ambalo litagharim maisha yako. Ila she really really needs help
Huwa anapata counseling ila ni mara chache.. Nitajitahidi kuzungumza nae niona kama tunaweza kupata counseling regularly
 
wewe ni shujaa,,,,unaelekea ukomavu halisi....ushauri wangu,,,,maisha ya nyuma ukiyaweka mbele yako huwezi move broo.....futa delete tupa kule.....peleka posa....vuta kinu ndani......anzeni maisha upyaaaaaaa.....zingatia haya....hakikisha na yeye ameridhia,,,, sio kesho kushokutwa anaanza oooohhh nilikwambia nimebakwa hukunisaidia.....vigeu geu kweli hao.....kila la kheri....
Nitajitahidi mkuu, naomba kwa Mungu pia afanye wepesi
 
Pia msisahau kupima HIV
Vipimo vyote tumepima zaidi ya mara moja, yupo sawa kiafya hana shida na zamani alikua hali kabisa ana mawazo ila nimejitahidi siku hizi amekuwa tofauti hata kujichanganya na kutabasamu tofauti na kabla ya hapo
 
Anachohitaji sasa huyo binti ni hakikisho la usalama wake binafsi na upendo wake.
Kutafuta haki ni sawa lakini haibadilishi chochote zaidi ya kulipiza kisasi.
kama unampenda tangaza nia, fuata njia sahihi, oa kwa utaratibu unaokubalika ili umfanye kuwa na uhakika na uhalali wa mahusiano. kuzaa au kuishi kabla ya ndoa halali, utakuwa hauna tofauti na huyo mbakaji, kwa sababu unaweza kumtenda na hili likamharibu zaidi kisaikolojia!
Kama una mpenda, You are the cure!

Habari za muda wakuu!? Nimekuwa member hapa kwa muda lakini kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wangu. Nimefungua ID mpya ili kuleta mada hii.

Leo nimeona niombe ushauri kwenu maana najua kuna watu waelewa, watu wazima wanaojua maisha yalivyo na waliopitia mengi. Nianze

Mimi ni kijana nina miaka 25 na nina mpenzi (miaka 24) na nipo nae sasa miaka miwili na nusu sasa. Tunapenda na kusaidiana kwenye shida na raha.

Huyu mpenzi wangu aliwahi kukumbwa na tatizo la kubakwa akiwa na miaka 12 (sad) wakati tuna date nae kuna siku alichukua muda kunieleza tukio lilivyokuwa na nini kilifuata baada ya hapo. Unfortunately hakuwahi kupata justice (kitu ambacho kinaniumaga sana). Yani aliefanya kile kitendo ni mdogo wa baba yake wa kambo na hakuchukuliwa hatua yoyote hata kufikishwa tu kituo cha polisi na yupo uraiani mpaka leo.

Kinachoniumiza ni mama wa huyu binti, hakuwahi kujali kuhusu ni namna gani lile tukio litaathiri maisha ya mwanae huyu siku zote za maisha yake. Kuna muda huyu mpenzi wangu nikiwa nae (nimekuwa nae mara nyingi ila sijawahi kushiriki nae mapenzi hata mara moja) muda mwingine huwa analia na kumlaumu mama yake (alimwacha na huyu kijana mlevi na kusafiri kwenda msibani wakati walijua tabia yake ya ulevi na mama mkubwa hakuwa anaishi mbali alikua na uwezo wa kumpeleka kwa dada yake mpaka atakaporejea).

Ubaya zaidi ni kuwa huyu binti akiwa still primary alikua analelewa na baba mzazi ambaye alifariki kwa ajali, ndipo huyu binti akahamia kwa mama yake ambae alikua ameolewa na mwanaume mwingine. Tokea amehamia kwa huyo mama haikupita hata miaka miwili ndio likatokea tukio la kubakwa.

Hebu fikiri tukio la kufiwa na mtegemezi wako namba moja hata halijaanza kufutika kichwani linakuja tukio jingine baya maishani mwako. Alafu wale wenye uwezo wa kukusaidia kupata haki yako hawachukui hatua yoyote. Inauma sana, huwa natokwa na machozi mara nyingi nikifikiria kuhusu huyu mtu aliefanya hivyo.

Simfahamu lakini natumaini kuna siku nitamfahamu na nitamsaidia huyu mpenzi wangu kuipata haki yake, hata kama hatutakuwa pamoja tena. Natumaini naweza kujitoa kwaajili yake. Haijalishi kitatokea nini. Mungu ndio atajua.

Nimeishi kwa muda na huyu binti na huwa kweli napata tamaa za kimwili ila nikifikiria tukio alilipitia huwa sitamani hata kumgusia kuhusu hilo swala, hajawahi kuwa katika mahusiano kabla yangu mimi (naweza kuthibitisha hilo). Kufikiria kugusia hilo mara nyingi naweza kusababisha kuibua Post Traumatic Stress ambazo huyu binti amezipata kutokana na tukio hilo.

Hali hiyo imenifanya niwe na chuki na wazazi wake hawa (mama na baba wakufikia) kiasi kwamba najiuliza kama huyu nataka kumfanya awe mke wangu nitawezaje kuwa face hawa watu? Pia imenifanya nimchukie huyo nisie mjua lakini nilieko kwenye harakati za kumjua.

Nia ya kueleza yote hayo ni kuomba ushauri nifanye nini? Nataka kuoa, au hata kabla ya kuoa nipate angalau mtoto naona umri unakwenda kwa kasi, niliwahi kumweleza akaniambia subiri, kila nikimkumbusha hunipa kalenda mpaka sasa aliniahidi angeisha na mimi kuanzia january 2018 lakini siku sio nyingi ameniomba nimwongezee miezi saba.

Je mtu kama yeye tunaweza kuwa na mahusiano yenye furaha? Maana sitaki hata siku moja nimuumize moyo wake. Je kuna siku kweli ataridhia kuwa mke wangu, au ataendelea kunipiga kalenda mpaka nikate tamaa?

Kiujumla sina nia ya kumwacha lakini naomba ushauri kwenu kuhusu hayo niliyoeleza hapo juu.

Najua kuna watu/mtu unaweza kuisoma hii ambaye umeshatokewa na matukio kama haya poleni sana.

Naombeni ushauri nipo njia panda. Ukiona ni sawa kukejeli hamna shida.
 
Anachohitaji sasa huyo binti ni hakikisho la usalama wake binafsi na upendo wake.
Kutafuta haki ni sawa lakini haibadilishi chochote zaidi ya kulipiza kisasi.
kama unampenda tangaza nia, fuata njia sahihi, oa kwa utaratibu unaokubalika ili umfanye kuwa na uhakika na uhalali wa mahusiano. kuzaa au kuishi kabla ya ndoa halali, utakuwa hauna tofauti na huyo mbakaji, kwa sababu unaweza kumtenda na hili likamharibu zaidi kisaikolojia!
Kama una mpenda, You are the cure!
Asante mkuu. Nitajitahidi kufanya hivyo.
 
MKUU AMETUMIA KIGEZO GANI KUKUPA MIEZI SABA?.KWANINI ISIWE MITANO ,ISIWE MOJA, NAULIZA HIV KWASABABU INAWEZA IKAFIKA MIEZI SABA IKAWA HAITOSHI KUMBE ILIBIDI MIAKA SABA.....
 
Aliniambia nimpe miezi saba apone kabisa.. Sikuelewa sana ila sikutaka kumbishia kwakuwa nampenda kwa moyo na nimesha invest muda wangu mwingi kwake hivyo miezi saba kwangu sio mingi. Hofu niliyo nayo ni baada ya huo muda kutimia je hataibuka tena na sababu?
 
Back
Top Bottom