Nia ya UKAWA kumshtaki Lipumba ni danadana za kisiasa na kutafuta umaarufu wa bei chee!

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,671
40,918
Malengo ya vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi Ukawa kumshtaki Lipumba kwa kudai kua hawamtambui kama mwanachama wa CUF, ni danadana tu za vyama hivyo, ikiwa ni katika jitihada za kutafuta media coverage!

Kwa namna yoyote ile, Ukawa sio mwanachama wa CUF, hivyo yanayofanyika CUF, hayana madhara ya moja kwa moja kwa UKAWA! UKAWA sio chama, ni muunganiko wa hiyari tu ambao hautambuliki popote kisheria.

Ili kwa mahakama kuweza kusikiliza madai ya mlalamikaji, kunahitajika kuonekana madhara ya moja kwa moja kwa mhusika. Kwakua hakuna madhara ya moja kwa moja kwa ukawa yanayotokana na Lipumba kua mwenyekiti wa CUF, UKAWA haina miguu ya kisheria kumshtaki Lipumba.

Chadema Blog: Maazimio 8 ya UKAWA ya kukabiliana na Prof. Lipumba na Msajili wa vyama vya Siasa
 
Ukawa ni sawa na MTU HEWA kisheria, hawana hata miguu ya kusimamia kumshitaki mtu yeyote, wanachofanya ni blaah blaah za kisiasa tu.
 
UKAWA ilijengwa kwa matope tena kipindi cha masika naona zinabaki fito tu. wajipange sana.
 
Ukawa ni sawa na MTU HEWA kisheria, hawana hata miguu ya kusimamia kumshitaki mtu yeyote, wanachofanya ni blaah blaah za kisiasa tu.
Bora umeliona hilo, mkuu, lakini wenyewe watatoka na kuwaambia wafuasi wao kua hilo linawezekana na watawaamini!
 
Mmekaaa weeee,mkafikiri weeeee mkaona sasa ukawa imewashika pabaya mkaamua kuja na cheap propaganda,SHAME ON YOU ALL
 
Malengo ya vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi Ukawa kumshtaki Lipumba kwa kudai kua hawamtambui kama mwanachama wa CUF, ni danadana tu za vyama hivyo, ikiwa ni katika jitihada za kutafuta media coverage!

Kwa namna yoyote ile, Ukawa sio mwanachama wa CUF, hivyo yanayofanyika CUF, hayana madhara ya moja kwa moja kwa UKAWA! UKAWA sio chama, ni muunganiko wa hiyari tu ambao hautambuliki popote kisheria.

Ili kwa mahakama kuweza kusikiliza madai ya mlalamikaji, kunahitajika kuonekana madhara ya moja kwa moja kwa mhusika. Kwakua hakuna madhara ya moja kwa moja kwa ukawa yanayotokana na Lipumba kua mwenyekiti wa CUF, UKAWA haina miguu ya kisheria kumshtaki Lipumba.

Chadema Blog: Maazimio 8 ya UKAWA ya kukabiliana na Prof. Lipumba na Msajili wa vyama vya Siasa
Hayo maazimio yatakufa kama ukuta.
 
Lipumba alishajiuzulu CUF. Kila mtu anafahamu hivyo. Kama kuna mtu anamhitaji amkaribishe katika chama chake..
 
...
....Uzi wako hautapata wachangiaji ..cheki Uzi wa katibu kubwaga manyanga unavyotembea kwa spidi ya Subaru...

Na log off
Lengo ni kuhabarishana, hayo mengine ni katika kuchagiza tu, unless wewe pia sio mchangiaji, maana tayari umeshachangia.
 
Back
Top Bottom