Ni yeye David Kimche au mtu mwingine?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,912
30,253

Kushoto Netanyahu na David Kimche

Nimeikuta picha hiyo hapo juu katika group moja na chini yake huyo aliyeiweka akaandika maneno haya: ‘’ Duh! Watu muhimu sana hawa katika historia ya Zanzibar!’’

Picha hii naifamu na mtaalamu wa historia ya Zanzibar amepata kunieleza kuhusu huyo anaesemwa kuwa ni David Kimche kuwa si yeye.

Mtaalamu huyu akaongeza akanambia, ‘’Kimche hakai kupigwa picha, yeye anafanya mambo wanakuja watu kupiga picha.’’

Kwa wale wasiomjua Kimche, huyu alikuwa kachero mkubwa katika MOSAD Shirika la Ujasusi la Israel.

Lakini si kama Kimche hakufika Tanganyika na Zanzibar la hasha kafika kote wakati inafanywa mipango ya kupindia serikali ya Sheikh Mohamed Shamte.

Kimche alikuwa na watu wake Tanganyika wakijuana vizuri tu.

Kimche wataalamu walimpa jina, "Master of Disguises." Kwani alikuwa na uwexo wa kujibadili sura na umbo atajavyo.

Kimche alipofariki miaka michache iliyopita magazeti mashuhuri ulimwenguni yalitangaza kifo chake na kuandika taazia yake.

Turejjee katika maneno aliyoandika mweka picha, ‘’Duh! Watu muhimu sana hawa katika historia ya Zanzibar!’’

Katika picha ile ya watu kumi, wanane ni wananchi na katika hawa wanane watatu waliuliwa - Abdallah Kassim Hanga, Abdulaziz Twala na Abeid Karume.

Inawezekana umuhimu aliouona mweka picha ni hii hstoria ya kusikitisha ya mauaji.
 
Mzee Mohamed Said Je unaweza kutusaidia huyo wakati alikua ni nani?

Kwa ufahamu wangu Kimche alishaondoka Kwa kipindi ambacho ianonyeshwa hiyo picha ilipopigwa
 
Benjamin Netanyahu alifika Zanzibar haya maajabu ndio Yale ya Putin na samora masheli Tanzania kweli Hii nchi ilikuwa kiboko
 
Back
Top Bottom