Tanzania Bara hiyo kitu ni ngumu sana kutokea, Katiba yetu haijaweka hiyo kitu bayana, hivyo utekelezwaji wake utahitaji utashi wa wahusika kwa kiasi kikubwa na kwa ubinafsi wa CCM sidhani kama hilo litawezekana.
Katiba ya Znz inaruhusu hicho kipengele na nadhani hiyo sheria ilipitishwa na Baraza la Wawakilishi wakati ule kutokana na uwiano wa wabunge kwenye baraza la wawakilishi, CCM na CUF ile ya Seif walikuwa na idadi ya wabunge inayokaribiana, hili likawabana CCM ikabidi wakubali.
Japo CCM walikuja kulazimisha nafasi ya Makamo wa Pili wa Rais iwepo, baada ya Makamo wa kwanza wa Rais kuchukuliwa na Seif, hiyo ya pili akapewa Balozi Seif Ally Idd.
Lakini pia jambo jingine kubwa linalofanya uwepo wa serikali ya mseto kuwa ngumu Bara ni pale ambapo Katiba yetu inatamka mgombea yeyote atakayeshinda nafasi ya Urais, hata kwa tofauti ya kura moja, huyo ndie atakaetangazwa mshindi. Hili linapunguza kwa kiasi kikubwa uwepo wa serikali ya mseto Tanzania Bara.