Kichaa Msafi
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 1,090
- 2,141
Nisiwachoshe wakuu kama mada isemavyo,kuna makundi matatu ya watu wasemao ukweli daima nayo ni;
1. Vichaa: hawa watu ukisikia wanakuambia kitu usikipuuze huwa hawana desturi ya kudanganya japo watu wengi tunawapuuza sana siku zote.
2.Walevi: Hawa nao wanaingia kwenye kundi hili pale wanapokuwa wameutwika kweli kweli iwe kwa bahati mbaya, au kwa kudhamiria kwamba leo nakunywa ili nikampe ukweli wake yule jamaa, au baba, mama, mke, mume, rafiki, au ndugu ukiwa mchawi, mwizi jambazi malaya mnafiki au mwongo huyu drunker akikunywea wewe ujue mambo yako yote yatakuwa hadharani, nayo yatakuwa ya ukweli mtupu, watu hawa nao huwa tukiwadharau tukisema aaah hizo ni pombe tu, ndugu zanguni huo msemo wa huyu mlevi tu ni kujifariji tu ili kuua soo, lakini huwa anakuambia ukweli mtupu.
3.Mtoto mdogo: Huyu kama kashuhudia kitu atakisema kama kilivyo bila kupepesa macho wala kutikisa masikio, hata ukimwambie arudie mara buku atahadithia kama ilivyo, ila tu awe ameshuhudia na sio kwa kufundishwa ili aseme uongo, kwani hata ukimwambia arudie mara kumi hataweza.
My take.
Sasa wewe unayesema kila siku msema kweli mpenzi wa MUNGU sijui nikuweke kundi gani kati ya hayo.