Ni watu wa aina gani usiowapenda au kuvutiwa nao?

Sheillah Sheillah

JF-Expert Member
Jun 17, 2020
583
1,478
Habari.

Ulishakutana na mtu ambae kila kitu kinachoongelewa ni either kilishamtokea yeye au kilishamtokea ndugu yake au rafiki yake?

Yeye anajua kila kitu.? Hamna story utaleta asidakie "hata mimi ..." " baba yangu nae hivyo hivyo...".?
Leo nilikuwa saloon kama kawaida story zinapigwa. Kuna dada daah kila kitu yeye anakijua yaani. Kama ni vya aibu anasema rafiki yake kilimtokea au alifanya, kikiwa ni cha kishujaa anasema kafanya yeye.

Nikaona huyu ngoja nimjaribu nikasema "Juzi nilikula nyama ya mbwa" bishost nae huyoo kadakia na yeye alishakula nyama ya mbwa ila hakujua akaja kujua baadae. Sikuweza kuvumilia huo ujinga nikatoka zangu nje.

Watu ambao wanajidai kila kitu wanajua na kilishawatokea siwapendi. Ni aina gani ya watu ambao hauwapendi?
 
Mimi sichukii yote namchukulia mtu alivo, ni Kama udhaifu wake na siwezi mchukia kikubwa kwenye jamii naamini watu hatufanani.
 
Kumchukia mtu, ni sawasawa na kulima kwa kutumia mpini usio na jembe, mwishowe unachoka na kupoteza nguvu nyingi bila mavuno yoyote.
 
Kila mtu huwa na madhaifu yake, haina haja ya kumchukia maake hata wewe unaweza kuwa na madhaifu yako ila watu huwa wanakuchukulia kawaida na hawakuchukii,
 
Back
Top Bottom