Ni wapi Rais Magufuli yuko sawa lakini wasaidizi wake wanamkwamisha kwa bahati mbaya au kwa kukusudia?

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,467
2,861
Salam za upendo kwa Watanzania wote wakati tunasheherekea Noel kuadhimishia miaka zaidi ya 200o ya kuzaliwa Yesu Kristo ambae ni Bwana na Mwokozi wa maisha ya wanadamu.

Mwaka 1997 Rais Mkapa alizindua dira ya maendeleo ya Taifa 2025 na mission ya dira ya Taifa 2025 ni kuwafanya Watanzania wawe na middle class income earners. Nomba kugusia viashiria vitatu vya uchumi wa kati kwa mujibu wa andiko na muono wangu. Natambua tafsiri hii inaweza isikidhi matarajio yenye kukidhi expectations za kila mtu

High quality Livelihood (Inapimwa kwa mtu kuweza kumudu mahitaji ya kijamii kama kugharamia elimu bora, huduma za afya, maji umeme, usafiri ikiwemo)

A well Educated and Learning Society (jamii kuwa na uwezo wa kujielemisha kupitia taasisi za ndani nan je zenye kutoa elimu bora inayotupa nguvu ya kukabili changamoto za maadui ujinga, maradhi, umasikini, ukosefu wa ajira.. n.k)

A strong and Competitive Economy (Uchumi imara na uchumi shindani unaojumuisha Watanzania kwenye mambo mengi ambayo yako ndani ya uwezo wetu na kama hatuna uwezo kuwa na ubia na makamouni ya nje ili nasi tujenge uwezo huko mbele, mambo yafanywe na Watanzania)

Uchumi mzuri katika jamii yoyote duniani, ni mfumo wa uchumi jumuishi (inclusive economic system) unaoruhusu watu wengi kuhusika katika ukuaji wa bishara na huduma.

Mathalani, nchini Israel mwaka 2010 kulikuwa na vijiji vya ujamaa takribani 270 (wao wanaita kibbutzim). Vijiji hivyo vilikuwa na viwanda na mashamba ambayo yanachangia 9% ya bidhaa zinazozalishwa viwanda Israel, bidhaa hizo zikiwa na thamani ya US$8 billion (sawia na TZS 18.4 trilion) Mfano halisia mwaka huohuo 2010 kijiji cha Sasa (Kibbutz Sasa) kilichokuwa na wakazi 200 (kwa sasa kina wakazi zaidi ya 400) kilitengeneza US$850 million (sawa TZS 1.96 tril)na ) kwa kuuza bidhaa za plastic jeshini. Achilia mbali mauzo ya vitu vingine. Kama tikichukua uwiano wa hiyo product moja waliyouza na wakaamua kugawana revenue, ina maana kila mmoja alikuwa entitled kuweka kibindoni billion TZS 9.755

Kwa mujibu wa UN, Israel wako "Very Highly Developed” na kwa kipimo cha Human Development Index, wana-enjoy a higher standard zaidi ya nchi nyingi za Ulaya Magharibi.

Nataka Watanzania tutambue kuwa maendeleo yanatakiwa kuwa very inclusive. Niwaombe kwa nia njema tu wenzetu mlio serikalini ambao mnafursa ya kufanya maamuzi kwa niaba ya Watanzania million 55 tuna wajibu kuwashirikisha Watanzania ili private sector inayoshikiliwa na Watanzania pia ikue na ilete mchango endelevu unaogusa Watanzania wengi.

Tunajenga miundombinu (barabara, umeme, reli, meli, bandari, airports) na huduma za kijamii (shule, maji, hospitali, huduma za ugani) ni jamb jema, pamoja na hayo kuna uhitaji wa ku-finance development projects ambazo zinafungua mianya kukua kwa biashara na huduma ili kutengeneza fursa za ajira.

Ukosefu wa ajira tunawajibika kuukabili kwa pamoja. Jana Mhe. Rais katujuza kuwa Naibu Waziri kawaombe nduguze 11 ajira polisi. Jana tumesikia graduate wa UDSM kajiua kwa kukosa ajira. Si jambo la mzaha, tunawajibika kushirikiana. IKumbukwe huko nyuma tulipata habari wakubwa waliwaombea watoto wao kazi BOT kwa vyeti vya form 4. Kelele zilipigwa then tukanyamaza. Maana hapakuwa na namna, nao ni Watanzania ila ilitokea baba zao ni akina “mbate mbate”. Miaka 4 iliyopita, vigogo wa Idara ya Uhamiaji nao wakaingiza watoto wao, ikaonekana wamecheza “offside trick” refa akachungulia (goal line technology) goli likakataliwa. Sijui wako wapi watoto wa hao vigogo.

Haina maana kuwa na uchumi mkubwa wa viwanda na biashara kama South Africa na kuwaacha watu wengi wasiwe sehemu ya mfumo wa kukuza uchumi. Eventutally, itazaa uhalifu kama ilivyo South Africa sasa au kundi la wasomi matapeli kama Nigeria na Senegal.

The best way to predidict the future is to create it… Abraham Lincoln…The best way to increase tax base is to create avenue for industry, business, trade and services to sprout. Itatulipa tu huko mbele.

Tukiwa na strong & competent private sector, serikali ni mbia kwa kufaidika na makuzi ya private sector. Mishahara ya wafanyakazi kuna kodi ya serikali. Expenditure ya kununua huduma kama maji, umeme, airtime, TBS, NEMC, OSHA, TFDA kote huko kwa upande mmoja au mwingine serikali inapata fedha.
Corporate tax 30% au 25% ya annual net profit kwa waliosajili kwenye soko la hisa inaingia serikalini.
Mauzo ya bidhaa na huduma kwa walaji 18% moja kwa moja inaingia serikalini.

Nitoe mifano hai, bila shaka tuatelewa kwanini tuikuze private sekta yetu, maana tunachangia mara kwa mwara private sector ya wenzetu hasa wazungu.

Tunanunua magari mapya ya TOTOTA VX V8, Toyota GXR V8, NISSAN Patrol, Nissan Hardbody, BMW, Benz kwa ajili ya viongozi wetu na taasisi za serikali (by default) tunakuza private sector ya Japan, Ujerumani na kwingineko na kupanua tax base ya hizo nchi, kuwapa ajira watu wao.

Tumenunua ndege ambalo jambo jema kabisa (by default) tunakuza private sector kwa kampuni kama Boeing ya Marekani na Bombadier ya Montreal Canada na kupanua tax base ya hizo nchi, kuwapa ajira za watu wao...

Tumenunua mfumo mpya wa passport za kielectroniki... tumepeleke hela zetu nje kwa private sector ya Jamhuri ya Ireland kupitia kampuni zao za HID Global na DLRS Group...the list goes on.

Toka awamu ya 5 imeingia, imelazimisha wakusanya ushuru na tozo mbalimbali za malipo ya serikali kutumia Electronic Fiscal Devices (EFD) na kuachana na stakabadhi za makaratasi… jambo jema kabasa, ila tuna-export dola za kutosha kununua technology at expense ya kukuza private sector ya wenzetu, kupanua tax base ya serikali za wenzetu na kukuza fursa za ajira kwa wenzutu
Consider economic battle kati ya Xi Jing Ping and Donald Trump, japo wanasiasa ndiyo walikuwa players, wafaidika au waathirika ni Privates sector ambayo ndiyo inahusika na biashara na huduma kati ya China na Marekani.

Profesa Mpango usisikitike kukosa vijisenti vya wazungu kusaidia bajeti yetu… tukae tafuta fursa tukae chini sisi na wewe tuibue miradi ya kibiashara ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu itakayoruhusu kukuza viwanda na biashara kwetu ili tuki-saturate soko la ndani ya SADC na kuuza nje, kuna a potential increase ya tax base throght surplus ya balance of trade and balance of payment.

JPM ashasema na Watanzania tunaweza. Tukiacha kuhujumiana na kubaguana kwa kuwa-undermine Watanzania.

Nitoe mifano michache ya hivi karibuni na kale jinsi ambavyo kuna watu wametoka nje ya mifumo rasmi wakawa na mchango mkubwa katika mifumo rasmi ikiwa na public and private.

Wilbur and Orville Wright (maarufu kama the Wright Brothers) waligundua technology ya kurusha ndege wakiwa hawana any college certificate. Wakati huo huo Prof. Samuel Langley aliepewa US$50,000 mwaka 1900 na wizara ya Ulinzi Marekani nae aje na suluhisho la kurusha ndege na hakufanikiwa. Prof. Langley alikuwa na kila kitu (fedha na watu mahiri) kumfanya afanikiwe. With the team he had gathered and ample resources, his success was guaranteed but he did not.

Leo hii Marekani na dunia nzima inafaidika matumizi ya simu, computer na other gargets ambazo mgunduzi wake ni Steve Jobs ambae mpaka anafariki hakuwa kuwa na shahada ya chuo kikuu duniani. Apple imeajiri wafanyakazi 123,000 full-time inaendeesha maduka 504 retail stores

Facebook ilizaliwa kama masihara bwenini kama social network kwa vijana Havard leo imekuwa na kampuni kubwa ya biashara yenye thamani kubwa ikiwa imetoa ajira moja kwa moja wa staff 25,105 imamilikiwa na kijana wa miaka 33.

Daudi na Goliathi ni story tumeisoma na kusikia sana makanisani na kwingineko. Inafahamika, Daudi hakuwa askari aliesajiliwa na experienced trained kama wengine. Ila baada ya wote kuwa waoga, alipopewa nafasi akaonyesha tofauti ya kumuangamiza Goliathi. Je, Watanzania kuna wakati huwa tunawapa nafasi pale wanapokuja na mifumo mbadala ya utatuzi wa matatizo yanayoisumbua nchi hii?

Farao toka Misri, hao jamaa tuliowapa wajenge Rufiji Hydropower. Farao aliota ndoto na hakujua tafsiri. Ndoto sawa tunaweza kusema ni suala la mambo ya kiroho. Mungu and roho zaweza kujua nini tafsiri ya ndoto. Ila Yusuf aliefanikiwa kutoa tafsiri alikuwa na 7years human possible intervention food security project. Utunzaji wa chakula cha kutosha kulisha watu miaka 7 na nchi jirani, that was a human intervention.

Watanzania tukiwa inclusive, we will all win. Wasaidizi wa Farao, walijenga mazingira Yusuf asikizwe na Farao alimsikiza Yusuf bila kujali experience yake kwenye food security project. Wasaidizi wa Mfalme Sauli walilazimika kumpeleka Daudi kwa Mfalme na baada ya kusmsikiza alimruhusu Daud ku-neutralize threat katika Israel.

Well, hatuwainglii watu wenye fani zenu na hatutalazimisha, ila, seriously kama akina Mark Zuckberg walivyo leo, hata hapa kwetu kuna Watanzania wapo ambao wanaweza kuwa sehemu ya inclusive economic growth towards middle class earning country, ambayo, itamfaidisha kila mmoja.

Sometimes tunaumia kwa kuona mambo hayaendi, kuna watu wanajulishwa nini kifanyike wanapuuza. JPM ataondoka baada ya muda wake kikatiba kuisha, ila anatakiwa ajivunie alikuwa sehemu ya kucheza na Watanzania wanaomsaidia ndoto yake ya uchumi wa kati ambayo ni jumuishi.

Nawatakieni Heri za Krismas na Mwaka mpya 2019
 
Kwanza wewe ni nani? with all this long story! Jielekeze kuondoa udikiteita, human rights violation, freedom of expression, oppresive laws and the like, currently Tanzania is undergoing. The after that lete story za development!
 
Umeandika hoja za msingi ila awamu hii ni ya miundombinu!Uchumi wa mtu mmoja mmoja kila mtu apambane na hali yake!
 
Umeandika mada nzuri 'constructive' ila, kuna vitu 4 umechanganya ndo ikawa ndefu zaidi na hatuna utamaduni wakusoma vingi.....but you look knoledgable and resourceful. ungechang'anua:
# Kilimo chetu peke yake
# Agro industry peke yake
# Govenment strategic planning na
# Poor governance and lavish expenditure of JPM.....
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Kwanza wewe ni nani? with all this long story! Jielekeze kuondoa udikiteita, human rights violation, freedom of expression, oppresive laws and the like, currently Tanzania is undergoing. The after that lete story za development!
Development kwanza democracy baadaye mkubwa
 
Freddie Matuja tuvumilie Kwanza hadi tutakapopokea Ndege zingine mpya mbili Kesho ( Jumapili ) basi kuanzia Jumatatu na kuendelea tutakuwa katika nafasi nzuri ya Kukujibu hizi ' Hoja ' zako. Binafsi ninazo kama 73 hivi na nitatiririka na kuserereka nazo zote.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Kesho Airbus inaingia.
Braza..
Binafsi nampongeza sana mkuu wa kaya kwa maamuzi ya kununua Airbus, Bombadier, Boeing et al...
Shauku yangu ni kuona Watanzania tunakuwa sehemu ya kudandia airbus kama huduma. Inawezekana kama tuna mifumo jumuishi.
Kama nilivyosema, hela ya ndege ni kodi yetu ambayo imekuza private sector na kukuza ajira Canada. Sasa, we can do something for the course of win win situation in Tanzania setting.
Tuna imani wakubwa tuliowapa nafasi ya kuongoza ni wasikivu na watafanya jambo
 
Freddie Matuja tuvumilie Kwanza hadi tutakapopokea Ndege zingine mpya mbili Kesho ( Jumapili ) basi kuanzia Jumatatu na kuendelea tutakuwa katika nafasi nzuri ya Kukujibu hizi ' Hoja ' zako. Binafsi ninazo kama 73 hivi na nitatiririka na kuserereka nazo zote.

Tunaweza kusubiri ifike, lakini kwa kuwa iko njiani na itafika salama bin Salmini, we should think ahead of time namna gani mimi nawe tuwe sehemu ya kudandia Airbus.
Ni kweli mifumo yetu ya elimu haikutupa namna ya ku-think ahead of time. Ila kwa kuwa tumefika hapa, ni vyema kuanzia hapa hapa by deliberate effort of creating our future
 
Tunaweza kusubiri ifike, lakini kwa kuwa iko njiani na itafika salama bin Salmini, we should think ahead of time namna gani mimi nawe tuwe sehemu ya kudandia Airbus.
Ni kweli mifumo yetu ya elimu haikutupa namna ya ku-think ahead of time. Ila kwa kuwa tumefika hapa, ni vyema kuanzia hapa hapa by deliberate effort of creating our future

Naona umenipiga ' Dongo ' kiana mahala hapo Mkuu. Haya bhana leo mshindi Wewe!
 
Mwanao huyo wa Kike hajambo lakini? Mkeo bado yupo Ofisi ile ile au amehama?
Boss,
What you have asked is very personal and I don't think it is worth of responding public. By the way, it is out of content as per the matter in floor
 
Boss,
What you have asked is very personal and I don't think it is worth of responding public. By the way, it is out of content as per the matter in floor

Nilitaka tu ujue kuwa nakujua kuliko unavyojijua. Haya nikutakie Siku njema na Maandalizi mema na Sikukuu za mwisho wa mwaka. Ila nisalimie sana Mkeo tafadhali.
 
Nilitaka tu ujue kuwa nakujua kuliko unavyojijua. Haya nikutakie Siku njema na Maandalizi mema na Sikukuu za mwisho wa mwaka. Ila nisalimie sana Mkeo tafadhali.
Well, labda nitoke nje ya mada ili kuweka kumbukumbu sawa. Bila shaka wanafahamu kwa jina ila unaweza kuwa na ufahamu wa masuala machache sana kuhusu mimi hata kama unafahamu sehemu ya wanafamilia wangu.

Nikupe mfano rahisi tu kihistoria. Mama wa Mwl. Nyerere hakuwahi kujua full potential ya mwanae. Alifikia wakati kuwa na wasiwasi alipomwona Mwl. anaacha kazi na kuingia mstari wa mbele kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ukisoma biblia, hata ndugu wa Yusuf ambae alikuja kuwa sehemu ya utawala wa Misri nao hawakumjua vya kutosha ndugu yao. Hata walipokwenda Misri walishamsahau kabisa.

Mungu pekee wa Mbiguni ndiye mwenye details za kila mwanadamu. Tuishi kwa kuheshimiana na kumwona kila alie mbele yatu ni bora na anaweza kuwa sehemu ya kuboresha jamii niliyopo.

nakutakia sherehe njema na baraka za Noel na heri za mwaka mpya 2019
 
Well, labda nitoke nje ya mada ili kuweka kumbukumbu sawa. Bila shaka wanafahamu kwa jina ila unaweza kuwa na ufahamu wa masuala machache sana kuhusu mimi hata kama unafahamu sehemu ya wanafamilia wangu.

Nikupe mfano rahisi tu kihistoria. Mama wa Mwl. Nyerere hakuwahi kujua full potential ya mwanae. Alifikia wakati kuwa na wasiwasi alipomwona Mwl. anaacha kazi na kuingia mstari wa mbele kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ukisoma biblia, hata ndugu wa Yusuf ambae alikuja kuwa sehemu ya utawala wa Misri nao hawakumjua vya kutosha ndugu yao. Hata walipokwenda Misri walishamsahau kabisa.

Mungu pekee wa Mbiguni ndiye mwenye details za kila mwanadamu. Tuishi kwa kuheshimiana na kumwona kila alie mbele yatu ni bora na anaweza kuwa sehemu ya kuboresha jamii niliyopo.

nakutakia sherehe njema na baraka za Noel na heri za mwaka mpya 2019

Mkuu Kulikoni nimekugusa tu padogo lakini umeshaanza ' Kuweweseka ' hivi? Nimesema usijali na wala hamna shida ila nisalimie sana Mkeo au nimekosea labda? Kama labda unahisi pengine ' nimetembea ' nae ondoa shaka sina huo Ungumbaru ( Ujinga ) / Upopoma ( Upumbavu ) bali naheshimiana nae mno na namchukulia kama Dada yangu. Kuwa na amani tu Mkuu.
 
Back
Top Bottom