Ni wangapi wasingekuwa hapo walipo kama si msaada wa ndugu jamaa na marafiki?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Kusaidiana katika jamii ni muhimu sana, shida haina adabu wala haichagui. Sisi tunaoidhi Dar Mara nyingi tunapokea wagonjwa wanaokuja kutibiwa Muhimbimbili.

Mgonjwa ni mtoto wa jirani yenu kule Kaliua anamatatizo ya moyo na wamepewa barua waje Muhimbili. Familia haijiwezi na ili kupata nauli ilibidi wauze mbuzi wote na walimuendea mzee wako ili kuomuomba wafikie kwako.

Kwako unaishi kwenye chumba na sebule, ingawa mgonjwa amelazwa hospital lakini amekuja na wazazi wake wote wawili, mama yake mkubwa na shangazi yake.

Fikiria tu machungu wanayopitia hawa. Mama mkubwa na shangazi wamekuja kumsaidia mama mzazi kupika na kufua nguo za mgonjwa.

.
 
Aisee hata kama ndio kutoa msaada lazima kuwe na mipaka!
 
Msaada hauna mpaka kila muda kuwa na huruma usijiwekee hazina duniani Bali jiwekee mbinguni maana huko nondo hazipati kutu na wevi kuja kuiba hazina yako iliko ndiko na moyo wako utakapo kuwa
 
Nchi zilizoendela wana social security has funds sasa sisi wenyewe ndiyo social security funds wenyewe kwa wenyewe
 
Kweli kabisa, twaamini hivyo, kila mtu lazima alipata msaada kwa namna fulani kwenye maisha yake kupitia ndugu na marafiki, nasi tuna wajibu wa kusaidia pia..
 
Mkuu acha mawenge, ndio asili ya binadam kutegemeana, kwa maisha yako huwezi kujitosheleza kila jambo pasi na msaada wa MTU mwingine, uwe tajiri au masikini
Unajua tofauti ya neno "kutegemeana" na "kusaidiana"? Mwenye shida anaweza kupata msaada kutoka kwa mwenzake lakini sio kumtegemea mwenzake..hayo ni mawazoyangu , unapaswa kuyaheshimu hata kama hukubaliani nayo.
 
Tenda wema tu mkuu na kuna siku wanaamka hata nauli ya kwenda Muhimbili hawana
huko ni kuumizana tu mpendwa na binadamu tulivyokuwa hatuna shukrani wengine watageuza mchezo sasa. Mungu humpa mtu majaribu kwa kadri anavyojua huyo mtu anaweza kuhimili ila sio majaribu yote hutoka kwake...
 
Kweli kabisa, twaamini hivyo, kila mtu lazima alipata msaada kwa namna fulani kwenye maisha yake kupitia ndugu na marafiki, nasi tuna wajibu wa kusaidia pia..
huko ni kuumizana tu mpendwa na binadamu tulivyokuwa hatuna shukrani wengine watageuza mchezo sasa. Mungu humpa mtu majaribu kwa kadri anavyojua huyo mtu anaweza kuhimili ila sio majaribu yote hutoka kwake...
Ninaamini pia wageni hawa Mungu anatoa rizki yao kupitia kwako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom