Ni wanaharakati gani ambao sio wanasiasa ambao moto wao sio wa nchi hii?

DUBULIHASA

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
4,299
7,851
Habarini ndugu zangu kwenye jukwaa letu pendwa hili la siasa. Natumaini wote tunazidi kusongesha gurudumu la kimaisha. Kidogo leo nataka nijikite kwenye eneo hili la wanaharakati wanaopambania haki zetu.


Enzi hizo tunasoma sekondari kulikuwepo na wanafunzi ambao wao walikuwa ni frontline sana katika migomo ili kudai haki mbali mbali za wanafunzi. Pia hata vyuoni hali ilizidi kujitokeza kwa baadhi ya wanavyuo kuonekana wao ni wanaharakati wa kupigiwa mfano kwa kupambania maslahi ya wanafunzi pamoja na yoyote anayeonekana kuonewa. Kwa upande wangu nakumbuka kipindi nasoma Udsm migomo na maandamano yote yalishuhudiwa eneo flani lijulikanalo kama REVUTION SQUARE. Eneo hilo la REV SQUARE liliweza kushuhudiwa na wanaharakati wa kila aina ambao kwa sasa wengi ni watu maarufu ndani na nje ya nchi yetu.



Vilevile kwenye siasa tumewashuhudia wapambanaji wengi ambao mara nyingi wameweza kuhatarisha maisha yao au kwenda kinyume na msimamo wa vyama vyao kama Deo Filikunjombe, Tundu Lissu, Mzee mtikila na wengine wengi.


Lakini leo ningependa tuwazungumzie wanaharakati au wapambanaji ambao sio wanasiasa ila wameweza kupambana bila kurudi nyuma na kuweza kujizolea umaarufu mkubwa kwenye jamii zote. Hapa tunaweza wajadili wanaharakati ambao walijizolea umaarufu au wanaendelea kujizolea umaarufu nchi zima. Wafuatao kwa upande wangu ndio walionikosha zaidi pia na wewe taja unaowafikiria na ikiwezekana toa na sababu


(1) Ananilea Nkya
(2)Steven Ulimboka
(3) Deus Kibanda
(4) Mzee Mkinga
(4) Mama Hellen Bisimba
(5) Ole Ngurumo

HIYO NDIO TANO BORA YANGU, TAFADHALI NAWE WAWEZA TOA MAONI YAKO KWA LUGHA YA STAHA.
 
Huyo namba mbili mbona tangu alipokutwa na bwana pepsi, haonekani tena, yupo kimya

Hii inamaanisha kile alichokuwa akipigania kilipatikana,
 
1.Jenerali ulimwengu.2.Johnson Mbwambo. 3.Maggid Mjengwa. 4 Shekh Mselem Ali
 
Back
Top Bottom