Ni wakati wa watanzania kuamka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni wakati wa watanzania kuamka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by payuka, Jul 21, 2010.

 1. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hivi Karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la watanzania wanaoshiriki michezo mbalimbali ya bahati nasibu inayochezeshwa na hizi kampuni za simu ( Tigo , Vodacom, Zain na Zantel). Ni vigumu Kumbadili mtu mawazo yake asishiriki kwenye hii michezo hasa ukizingatia wapo watu wachache wanaoibuka washiri wa fedha, magari mapya na safari wanazokuwa wameahidiwa na waandaaji. Inasikitisha zaidi kuona mtu ana-spend hadi zaidi ya laki moja kwenye bahati nasibu ambayo mwisho wa siku hashindi kabisa.
  Ngoja nikupe mchanganuo wa kihesabu kidogo hapo chini ili tuweze kuelewa nia na dhumuni la waraka huu! Juzi tume ya mawasiliano tanzania ilitoa taarifa ya kwamba idadi wa watumiaji wa simu za mkononi hadi kufikia tarehe 30 june 2010 ilikuwa ni takribani milioni 19.

  Chukua mfano Vodacom inachezesha bahati nasibu ambayo mshindi atapewa RaV 4 Mpya kabisa ( let say gharama yake ni milioni 50- huu ni mfano). Mshiriki anatakiwa kutuma SMS yeno neno RAV 4 kwenda namba 1501, na kila gharama ya sms ni Tsh. 500. Endapo watumiaji wa simu milioni moja nchini kote watatuma sms moja moja Kampuni itakusanya kiasi cha Tshs. 500,000,000 ( milioni miatano).

  utaona ni jinsi gani makampuni ya simu yanajikusanyia fedha bila kutumia nguvu, na katika mchanganuo huo hapo huu nime-ignore baadhi ya vitu kama: makosa ambayo huwa yanatozwa pesa, watu wengine watatuma message zaidi ya moja.

  Wananchi wamekuwa wazito kuelewa kwamba bahati ya kushinda huwa ni ndogo mno, mfano katika watu milion moja mtu akiwa ametuma sms 3 kati ya sms milioni mbili nukta tano (1.5 Mil) zilizo pokelewa probability ya mtu huyo kushinda inakuwa ni sawa na asilimia 0.0002%. sasa unaweza kuona ni jinsi gani watu wanaamua kutumia pesa zao bila ya kufikiri kwanza.

  Haya tukiendelea mbele zaidi utagundua kuna unyonyaji mkubwa sana unaendelea Tanzania kupitia haya makampuni ya simu za mkononi, huku tukidanganywa na vimisaada wanavyo vitoa kwa jamii kupitia CSR programmes.

  Ukienda kiundani zaidi ni vichekesho vitupu, ulizia kodi wanayolipa serikalini. Nakumbuka niliwahi soma makala moja ya Sabodo kwenye gazeti la daily nyuzi akijaribu kuwafumbua watanzania macho, lakini ilipita ikaishia kimyakimya. Leo hii ni makampuni haya haya yanayopinga suala la kujisajili kwenye soko la mitaji.

  Kama una maoni au ushauri tuwasiliane kipitia: develo45@gmail.com

  " Hakuna mchawi , watanzania tunajimaliza wenyewe kutokana na umasikini wa kifikra"
   
 2. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mkuu.asante kwa makala yako.lakini km ulivyosema wa-TZ ndo tulivyo hatufikiri sana, kila mmoja anataka awe tajiri kwa siku moja tu!.
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160

  Kuna daa yangu humwambii kitu mbele ya hizi kamali, anaamini ipo siku ataibuka kuwamillionea kwa kupitia hizo kamali.
   
Loading...