Ni wakati wa kuyashitaki makampuni manne ya simu

Kuna mmoja alikuja kwa mbwembwe tena mwanasheria akasema anayashitaki lakini akaishia kutoa mrejesho mmoja tu baada ya hapo akaingia mitini inaelekea walimpooza kitu kidogo
 
NI WAKATI WA KUYASHITAKI MAKAMPUNI MANNE YA SIMU.

Niwakati Sasa wakuyashitaki Makampuni ya simu Tigo, Airtel, Vodacom na Halotel. Kwa mujibu ya Sheria Namba 12/2003 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania mashtaka ya aina hii yanatakiwa kuaandikiwa makampuni hayo taarifa kuyataka yarekebishe ndani ya siku 30 ninachokilalamikia.

Nitaomba mambo sita nikifungua kesi hii.

JAMBO LA KWANZA,
Vifurushi vyote havipaswi kuexpire. Kitu pekee ambacho kinapaswa kumaliza kifurushi inatakiwa iwe ni wewe kuongea hadi dakika zako zikaisha.

Si haki kukata kifurushi cha mtu ambaye dakika zake za kuongea,za data, au sms bado zipo kwa kigezo cha kuexpire au muda wake wa wiki, masaa12, nk kuisha. Lazima kitu hiki kiondoke.

Mathalan, umejiunga kifurushi cha 1000 na umepewa dakika 10 ndani ya masaa 12. Umetumia dakika 3 tu ambazo thamani yake kifedha ni shilingi 300, na masaa 12 yameisha. Maana yake kwenye 1000 yako zilibaki dakika 7 ambazo thamani yake kifedha ni shilingi 700, ambazo hizo sasa shilingi 700 kampuni ya simu inajirudishia kwa kigezo cha muda kuexpire. Nachelea kuiita huu wizi lakini initoshe kusema hii haiwezi kuwa haki na haikubaliki.

Lakini pia ninapolipa 500 na wewe ukaniuzia kifurushi si nimekulipa hela yako yote na wewe hunidai. Sasa kwanini tena unachukua kilekile nilichonunua kwako na hela yako yote nimeshakulipa.

Ni hivi,unaponunua kifurushi ni sawa na umenunua bidhaa, na ukishanunua bidhaa hakuna mtu mwingine yeyote, akiwemo aliyekuuzia bidhaa hiyo, mwenye haki ya kuichukua tena bidhaa hiyo yote au sehemu yake isipokuwa wewe uitumie mpaka iishe.

Tizama Tanesco na LUKU. Tanesco ikishakuuzia umeme/units ukamlipa basi hatma ya units zako ni utumie mpaka umalize.Hawezi kuikata na kujirudishia kwasababu anajua alikuuzia bidhaa na wewe ukamlipa na hivyo una haki ya kutumia bidhaa yako mpaka umalize. Hii ndiyo HAKI.

Kinachofanywa na makampuni ya simu ni sawa ununue soda dukani na mwenye duka umlipe hela yake yote. Halafu mwenye duka huyohuyo akwambie kwamba usipoinywa soda yote kufikia jioni au ndani wiki au mwezi nitakuja tena kuichukua nyumbani kwako, na aje kweli aichukue iwe mali yake tena kwa mara ya pili.

Zaidi ya hayo,ukweli halisi ni kuwa kifurushi kwa muundo wake si bidhaa inayoexpire. Ukinunua soda ikiexpire utauona, utaona kabisa kwa macho kadhalika bidhaa nyingine zenye sifa ya kuexpire. Lakini kifurushi kwa uhalisi wake si bidhaa inayoexpire au yenye sifa ya kuexpire.

Hili neno kuexpire limetengezwa ili kuficha neno kupora au uporaji. Ukweli ni kwamba kifurushi kinaporwa makusudi kwa kigezo hovyo kabisa na dhahania cha kuexpire, sijui masaa yako 12, sijui wiki yako, sijui mwezi wako umeisha nk. Kifurushi kinaishaje kabla dakika zangu nilizolipia kwa ukamilifu sijazitumia zikaisha?

Yapo haya nayo lazima yaeleweke, mtu amejiunga lakini yuko safarini hawezi kutumia mda wake , mwingine alipo hakuna network, mwingine hajatumia mda wake alikuwa bize na kazi zake, mwingine simu haikuwa na chaji siku nzima, mwingine umeme ulikatika alikosa mawasiliano nk nk, hawa wote pesa zao walizolipia na hawajazitumia au wametumia kidogo zinakatwa na makampuni ya simu yanajirudishia pesa hizo bila kujali.

Ninataka nifunguwe kesi kuondoa unyonyaji huu .Hatuwezi kuendelea kuwa viwanda vya kutengeneza ukwasi wa makampuni ya simu.

JAMBO LA PILI
Haki ya kutochanganyiwa kifurushi na muda wa kawaida wa maongezi bila ridhaa.

Nitatoa mfano, unakuta mtu ameweka shilingi 1000 kwenye simu ambapo anajiunga 500 na 500 inabaki kama muda wa maongezi wa kawaida. Wakati anapokuwa akizungumza au akitumia data kupitia ule muda aliojiunga na ukaisha basi simu haikatiki bali inaunganisha moja kwa moja na ile 500 ya muda wa maongezi wa kawaida ambayo alikuwa hajajiunga.

Hii si sawa hata kidogo na ni vitu ambavyo vinatengenezwa maksudi ili kujipatia fedha bila kujali mtumiaji anaumia kiasi gani. Ni hivi, mtu anapoamua kujiunga 500 na akabakisha 500 bila kuiunga ana maana yake kubwa tu.Hakushindwa kuunganisha 1000 yote.Amechagua 500 kwa maksudi maalum. Sasa iweje unamlazimisha kutumia akiba yake ya 500 hata bila ridhaa yake.

Inatakiwa kuwe na chaguo (option) iwapo mtu anahitaji huduma ya aina hiyo au hapana. Au inatakiwa muda wa kifurushi ukiisha simu ikate halafu kama anataka kuendelea kutumia muda wa kawaida achague mwenyewe kuendelea kuutumia na sio kampuni ya simu kumchagulia.

Au kama anataka kujiunga na hiyo 500 iliyobaki basi ajiunge. Isiwe biashara ya kuviziana kama ilivyo sasa. Hili nalo lazima waliondoe.

JAMBO LA TATU, Haki ya kujua matumizi ya kifurushi. Malalamiko ya vifurushi vya watu kuliwa isivyo kawaida ni mengi mno.

Unanunua dakika 20 unaongea 10 unaambiwa kifurushi kimeisha, unabaki kushangaa. Ni lazima waweke mfumo wenye kutoa taarifa sahihi na za wazi(transparency) ili kumwezesha mtumiaji kumonita matumizi ya kifurushi chake.

Malalamiko ya watu ya kutumia vifurushi chini ya kile walichonunua yanaongezeka siku hadi siku. Kuwaachia makampuni ya simu wao wawe ndio wauzaji wa vifurushi, na wao hao hao ndio wakueleze umetumia nini,kama umemaliza au hujamaliza, huku wewe mteja ukiwa kipofu/gizani ukisubiri kupokea lolote wanalolisema wao, kupigwa hakuwezi kukwepeka.

Waweke mfumo ambao wao pamoja na mteja watamonita matumizi ili mteja aweze kuhoji. Teknolojia imekua hili ni dogo sana.

JAMBO LA NNE Haki ya kuhamisha kifurushi.

Nimesema hapo juu kifurushi ni mali yako na ndo maana unailipia pesa na hivyo kuwa na haki ya kuitumia kwa uhuru.

Kwa msingi huu makampuni ya simu ni lazima yaweke mfumo unaomwezesha mtu kumhamishia mtu mwingine kifurushi kama ilivyo kwenye muda wa kawaida wa maongezi. Maana yake nikinunua kifurushi cha 1000 labda dakika 10 za maongezi, Mb 100, na sms 50.

Niwe na uwezo wa kumgawia yeyote ninayemtaka kiasi cha muda wangu wa maongezi,sms au Mb. Na hii ninaamini inawezekana kabisa kugawiana watu wa mtandao mmoja.Tunahitaji uhuru huu kwetu.

JAMBO LA TANO.Haki ya kupewa tahadhari kuhusu kifurushi au muda wa hewani unapokaribia kuisha. Kuna makampuni wana huduma hii lakini wanaitoa kwa hiari sana na wengine wameacha kabisa. Wengine wanatoa tahadhari muda unapoisha na sio unapokaribia.

Tunataka watoe unapokaribia ili mtu ajipange. Ni haki mtu kupewa tahadhari wakati akizungumza,akiwa kwenye mtandao, au sms, kuhusu dakika zake kukaribia kuisha. Sio sahihi wala ustaarabu simu kukatika ghafla bila tahadhari.

Na wanafanya hivyo maksudi wakijua unapokatakiwa na mawasiliano ghafla ni lazima tu utakuwa hujamaliza haja yako na hivyo utalazimika kuongeza vocha ili umalizie na wao wapate mauzo zaidi.

Wanajua ukipewa tahadhari unaweza tu kufupisha mazungumzo yako na wakati simu inakatika ukawa tayari umemaliza na hivyo usihitaji tena kuongeza vocha. Tabia za hovyo kabisa za kuviziana.

Unawezaje kunipa tahadhari ya muda kuisha ukashindwa kunipa ya muda kukaribia kuisha. Hili nalo tunataka lifanyiwe kazi.

Sita: unakuta umenunua kifurushi labda Cha siku au wiki halafu unakuta kunatatizo la mtandao na tatizo nilao unakuta mtu anapoteza kifurushi chake na hafidishiwi mtumiaji anakuwa amepoteza huku kampuni ikinufaika hili nalo lazima likome

SHERIA ya Mambo haya kwa ujumla wake ni kinyume na Katiba ya JMT Ibara ya 18( c ) inayotaka uwepo wa mawasiliano bila kuingiliwa, lakini yanakiuka Kanuni za Kielektroniki na Mawasilano ya Posta kuhusu viwango vya Tozo GN. No 22/2018 hasa Kanuni ya 4 ( 1na 2) inayotaka viwango vyote vya tozo za simu kuwa vya haki na kadri(just and reasonable), yanakiuka Kanuni ya 4 ya Kanuni za Kielektroniki na Mawasiliano ya Posta GN No.61/2018 kuhusu kumlinda mlaji inayotaka mlaji kupewa taarifa kwa usahihi ya matumizi ya huduma muda wote, yanakiuka Sheria ya Ushindani namba 8/2003 inayotaka mtoa huduma kutoa huduma kwa kuzingatia zaidi maslahi ya watu wa hali ya chini, na sheria nyingine nyingi zimekiukwa.

Na tuelewane vizuri hapa, hakuna kitu kinaitwa VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA. Sheria iko wazi kuwa neno,maneno,sentensi au msemo wowote wenye lengo la kusigina haki ya mtu/watu ni batili.

Basi nitaviomba vyombo vya maamuzi vitusaidie kuyaweka sawa haya sita.nawasiliana na wana sheria wangu wa LIS Low chembers kwa ushauri zaidi ili haki iten deke.

Naomba tushirikiane kutetea haki ya wanyoge.
Ndio maana huwa nafurahi sana serikali ikiwapiga mafaini ya mabilioni,huwa naamni ni kutokana na wizi wanaotufanyia, hivyo pesa zetu hurudi kwa njia hiyo ,kwani serikali hupeleka fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo
 
Kweli mkuu wanatutesa sana
 
Kuhusu changamoto ya vifurushi na mabando kupanda bei na kuwahi kuisha, kama nilivyowahi kusema hili jambo tunaendelea kulifanyia kazi na tutatoa kauli ya Serikali Tar 28 Mwezi huu.
Wananchi watuvumilie kuna mambo tunachakata lengo ni kupata suluhu ya kudumu-Waziri
 
mkuu hoja nzito sana.mim leo nimezinduka.hiv kwel.unalipa halaf wanakwambia utumir usipotumia wanakata.ndio mana wanatajirika.
data ya halotel buku ile ya wik hata sielew jana laeo naaambiw kimeisha gb
 
Tunasubiri kauli ya Waziri, alituambia jana mwisho wa Mwezi Tarehe 28 Feb watatoa kauli ila kimya kimetawala.
 
Mnatafuta kupozwa tu, wakili yakub alikuja hivyo hivyo sasa sijui alipozwa simsikii tena
 
mkuu hoja nzito sana.mim leo nimezinduka.hiv kwel.unalipa halaf wanakwambia utumir usipotumia wanakata.ndio mana wanatajirika.
data ya halotel buku ile ya wik hata sielew jana laeo naaambiw kimeisha gb
Kweli mkuu wizi umekithiri
 
Hao jamaa ni matapeli sana, voda wanaiba sana vifurushi. Unajiunga 1GB unaperuzi tu bila kupakua kwa muda wa masaa mawili kifurushi kimeshaisha, kinachoonekana ni kwamba hiyo 1Gb wanayoiandika inakua ni kwa ajili ya bluffing tu na uhalisia pengine ni 200Mb.
 
Hakika umenena Mkuu, kimsingi ukinunua kitu ni chako. Iweje mwingine awe na right ya kuchukua mali yako na kwamba harudishi hela yako.

Uko sahihi Sana Mkuu.

Jambo la sita la kuwafungulia mashitaka.

Ukituma pesa mitandao mw
ingine kimakosa, huwezi kurejesha. Mfano umemrushia mtu wa Airtel na wewe ni Vodacom, hakuna huduma ya kurejesha ile hela, hapa pia ni ukakasi, Kama wameweka utumaji kwenda mitandao mingine, iweje wakunyime haki ya kurejesha.?
 
Mwanasheria wa utopoloni kwanini watupimie muda wa kifurushi wakati tumeshamalizana...? Achana na locus stand hii issue sio.
Mkuu...sidhani kama umefanya homework yako vizuri kwenye hilo.

Kifupi ni kwamba ukiwaambia bando lisiexpire watakuuzia mb 50 kwa 1000 utakaa nayo muda gani? ref halichachi inavyo apply.

Halafu kujiunga ni option na ni kama promotion tu bt unaweza tumia muda wako wa maongezi tu kupiga simu,kutuma msg na kusurf bila ku expire,unless una hoja nyingine Ila kwa hizo huna locus stand.
 
Kwa tuloanza kwa mtandao wa buzz kwa wakati huo sasa tunaona full burudani tu, kulikuwa na mfumo wa kuweka vocha na kuongea pasipo option za jiunge hela zilikuwa zinatafunwa hivi hivi unaona palikuwa hapahitaji hata salamu ni kwenda moja kwa moja kwenye lengo lililopelekea upige simu otherwise utabaki unaongea peke yako salio lisha kwisha kitambo.
 
Mwanasheria wa utopoloni kwanini watupimie muda wa kifurushi wakati tumeshamalizana...? Achana na locus stand hii issue sio.
Ungeuliza swali bila kufanya kebehi ungepungukiwa nini mkuu? nikuelewi vipi sasa ndo mjanja sana au msela sana?
 
Back
Top Bottom