Ni wakati wa kuwauliza viongozi wetu haya!

Kyachakiche

JF-Expert Member
Feb 16, 2009
983
207
Kama Watu tunao, Ardhi tunayo, Siasa safi tunayo, na Uongozi bora tunao, kwanini hatuendelei? Wadau kama mnakumbuka vizuri, enzi za Mwalimu tuliambiwa kuwa, ili tuendelee, tunahitaji vitu nilivyovitaja hapo juu. Sasa ni wakati wakuwauliza viongozi wetu, kama vyote hivyo tunavyo, kwanini hatuendelei???
 
Kilichokosekana ni uongozi bora. Mafisadi wameshika hatamu. Chukua mfano wa Uingereza, bwana David Cameron alivyochukua madaraka na kukuta hali ya uchumi ni mbaya, yeye na mawaziri wake wamepunguza mishahara yao. Ukija Tanzania, watawala hawataki kupunguza marupurupu yao bali ni kuyaongeza. Safari za nje ni kama kawa.
 
Mkuu nakubaliana nawe moja kwa moja hasa hapo nilikokoleza. Je, tufanye nini sasa?
 
Ili tuendelee tunahitaji mambo manne kwa wakati huu;

1. Kupunguza ongezeko la watu, Masikini mmoja akizaa watoto 5, umasikini umeongezeka mara 5 zaidi.

2.Kuwanyima ardhi wageni, ikiwa ni pamoja na kuwafutia mikataba wezi wa maliasili na gesi asilia. Kwa sasa wanaochimba na kuuza gesi ni wageni.(Makampuni yote yanahusika na maliasili yawe ya wazawa).

3.Kuwaondoa walanguzi, wezi, mafisadi na washirika wao kwenye siasa.

4. Kuchagua viongozi wanaowatumikia na kuwajali wananchi wa kawaida badala ya wanaotumikia, kushirikiana na kuwajali mafisadi.
 
Back
Top Bottom